Nini lengo la serikali kubadili namna hii jina la mtihani wa kidato cha pili?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Malengo halisi ya mtihani Wa kidato cha enzi zetu yalikuwa ni kuwachuja wanafunzi. Mtihani huu ulijulikana kwa jina la "FORM TWO NATIONAL EXAMINATION".

Huu mtihani nakumbuka tuliuheshimu sana kwa kuhofia kurudia darasa!
Lakini sasa hivi mambo ni tofauti kabisa, mtihani huu hauna nguvu tena. Sasa hata sielewi kwanini wameamua kuupa jina hili jipya "FORM TWO NATIONAL ASSESSMENT".
********************************
e74150b7512c17ca1ba086922959eefc.jpg

Sasa Mayai Visa tuyakusanya wenyewe halafu tunakuja kuyatumbulia form six! Hili ni Bomu tunaliandaa kubwa kuliko hata tungewapunguza hukuhuku chini;
Faida ya kuwapunguza wanafunzi Kwa kuwachuja
1. Tutaepuka kuwapotezea mda.
2. Tunauwa vipaji vyao, wengine wangejua mapema kuwa shule hawaiwezi basi wangejiajiri na kuanza mikakati mingine mapema kama kilimo, mziki na ujasiliamali n.k (wengi wanaofika Form six na kufel huona aibu kufanya shughuli kama hizi tena)
3. Gharama kubwa ya kusomesha vila.**za inachangia umasikini katika familia na taifa..ambapo Pesa nyingi zinatumika wakati zingetumika Kwa wachache wenye faida na kuwahudumia vizuri.
4. Lundo kubwa la wanaotemwa ni janga kiusalama wanaweza kuwa vibaka.

Naomba kuwasilisha.
 
duh ni kweli unasema mkuu? kabla sijachangia embu weka taarifa sawa kam kweli tumefika uko?
 
Chekecheka hadi darasa la 12 ni elimu msingi, na elimu msingi maana yake nzuri ni kwamba kila mtu anatakiwa kuwa nayo walau. Sasa ukishaufanya mtihani wa ngazi yoyote iwe la 4, la 7, ama la 10 uwe mgumu na wa kuchuja ni wazi utakuwa umeharibu maana ya elimu msingi ambayo ni "universal", ndo maana unaona mambo yako yako tu ilimradi ...tunapima tu ila hatuchuji ili kila mtu apate elimu msingi

Nafikiri umenipata mkuu.
 
Sasa nimeanza kugundua kwanini Ndalichako alifukuzwa NECTA, pia nimegundua kwanini JK Alisema tutamkumbuka.

Miongoni mwa watu waliopendekeza Ndalichako apewe wizara HAPA Jf ni Mimi. ila najuta kufanya UJINGA kama Huo, Mola nisamehe bure. Wana jukwaa Naomba mnisamehe
 
Sasa nimeanza kugundua kwanini Ndalichako alifukuzwa NECTA, pia nimegundua kwanini JK Alisema tutamkumbuka.

Miongoni mwa watu waliopendekeza Ndalichako apewe wizara HAPA Jf ni Mimi. ila najuta kufanya UJINGA kama Huo, Mola nisamehe bure. Wana jukwaa Naomba mnisamehe
KATUBU MBELE ZA HAKI USAMEHEWE MAANA NI DHAMBI KUBWA SANA ULIFANYA ILA 2020 NA YEYE ATAISOMA NAMBA
 
wiki 1 au 2 zilizopita mtoto wa mpangaj mwenzang wa darasa la pili, aliniambia ametoka kufanya mtihan wa taifa wa darasa la pili, ckuelewa vzur. cku iz kuna mtihan wa taifa darasa la pili? jaman
 
Huwa ni professor ila sijawahi kumuelewa ngoja nimpe muda maana walimu kawasahau kabisa wao wanacheza na kutanua magoli, kuondoa ma-rise men, kumnyang'anya refa kadi kipyenga na kutafuta penati za dk za majeruhi.
Hatuwezi kwenda kwa mwendo huu
Hawataki kudeal na tatizo wao ni kubatiza majina tu changamoto changamoto oooh changamoto changamacho mara changa la jicho
Serikali za misamiati hizi
 
Aisee ht sijui jamani tunaenda wapi, anaejua tunakoelekea aniambie maana kila kona upepo mbaya tu.
 
Hili swala ni kweli na mitihani bado inaendwlea saasa nauliza kama kweli serikali inatumia garama kubwa kuandaa na kuratibu na kusimamia na kusahisha mtihani ambao ni assessment hauna mchujo kwann garama zote hizi. Na ukweli wengi wa watoto wa shule za msingi za serikali ambao mtihani ni wa kushade kwa sasa hutahiniwa na kusahishwa kwa computer na ndio maana wanao feli darasa la saba siku hizi ni wachache sana ,kazi inanzia wakienda sekondari tena za kata form 1 hajui kusoma wala kuandika kiswahili fasaha halafu ndio mtaala wa kimombo kama biology watoto hawa ndio kuna mwaka wapita kidato chapili bila mchujo mazero yakafyatia form balaaa sasa naona mkakati umeurudisha ili yale mazero yaongezeke form 4 na watakao enda kidato cha 5 wachache sana na vyuoni wawe wachache na serikali iwape mkopo wachache huko vyuoni wataofika wachache.mkumbuke kuna elimu bure inamkuna kichwa mkuu ni hizo hela sio mkopo km chuoni hizi hazirudi kabisa.
 
Kinachonisikitisha ni kuwa watoto wote waende tu form three hata kama ana wastani wa mbili
 
wiki 1 au 2 zilizopita mtoto wa mpangaj mwenzang wa darasa la pili, aliniambia ametoka kufanya mtihan wa taifa wa darasa la pili, ckuelewa vzur. cku iz kuna mtihan wa taifa darasa la pili? jaman
Mkuu upo mtihan hata mi nmeshangaa sana sa darasa la pili wale watoto hata wasipochujwa maan hua wanabukua sana
 
Hata ule mtihani wa drs la nne sasa hivi hauitwi mtihani unaitwa UPIMAJI WA DARASA LA NNE.
 
Sasa nimeanza kugundua kwanini Ndalichako alifukuzwa NECTA, pia nimegundua kwanini JK Alisema tutamkumbuka.

Miongoni mwa watu waliopendekeza Ndalichako apewe wizara HAPA Jf ni Mimi. ila najuta kufanya UJINGA kama Huo, Mola nisamehe bure. Wana jukwaa Naomba mnisamehe

Naamini Prof. Ndalichako amekuta sera ya elimu ya 2014 imepitishwa na iliandikwa wakati wa awamu ya nne.
 
Elimu ya tz imekufa kabisa na sasa tunaizika mipango imeingiliw kila mtu anajua tungoje wahitimu matahira miaka ijayo
Na viongozi watakuwa matahirapia
 
Ni kweli ndo walivofanya
ase sijui watakuwa na shida gan,lada ndo mambo ya elimu bure,kwamb lengo la kusomesha bure hadi kidato cha nne linatimia au kam sivyo ni kuwaangusha weng watakapofika kidato cha nne ndo uwe mwisho wao na hapo bado kwamb ndani ya hyo tena kuna suala la masomo ya sayansi kuwa lazima,sasa sijui tutawapima vp au kuwa na wanafunz ambao ni competent au wamepata elimu bora.
 
Back
Top Bottom