Ufaulu wa darasa la nne, kidato cha pili na nne umepaishwa ili kuwafurahisha wapiga kura; ushahidi huu hapa

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
17,412
11,026
Watanzania tumerogwa; yaani tunafurahia matokeo feki huku elimu yetu ikizidi kushuka kila mwaka. Aliyeturoga kafa. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya matokeo ya darasa la nne (SFNA), kidato cha pili (FTNA) na kidato cha nne (CSEE) kutolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) hivi karibuni na kuonyesha kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia mbili (2%) ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2020.

Baada ya kufuatilia namna mitihani inavyotungwa na kusahihishwa kwa muda mrefu nimegundua kadri miaka inavyokwenda mbele mitihani inazidi kurahisishwa ili wanafunzi wengi zaidi wafaulu. Hii ni sera ya serikali kuongeza ufaulu kwa wanafunzi kila mwaka ili wapate cha kusema mbele za wazazi (wapiga kura) kila baada ya miaka 5 ya uchaguzi.

Nikianzia kwenye suala la utunzi wa mitihani, siku hizi mitihani inatungwa kwa urahisi sana na kwa njia ya ajabu. Tangu serikali ilipoanzisha mitihani ya kubashiri (kubet) wanafunzi wengi wasiojua kusoma wala kuandika hufaulu kujiunga na shule za sekondari na wanaendelea hivyo hivyo hadi kidato cha nne.

Wanafunzi hawa wakifika kidato cha nne, serikali tena hutunga mitihani rahisi ili wengi wao wafaulu kujiunga kiadato cha tano kwa ubwete. Utafiti wangu umeonesha kwamba kadri miaka inayoenda mbele mitihani ya kitaifa kwa ngazi zote imekuwa ikirahisishwa kwa makusudi ili kuwafaulisha wanafunzi kisiasa. Tazama mtihani wa Biology wa NECTA 1996 ulinganishe na mtihani wa NECTA 2017 utapata jibu mwenyewe. Zamani kupata divisheni wani halikuwa jambo la mchezo. Lakini kwa maswali mchekea kama haya (2017) hata mkulima ambaye hakwenda shule hakosi kupata divisheni wani!

NECTA 1996
1643126834598.jpeg

NECTA 2017
1642443271019.png

Hali ni hiyo hiyo hadi kwenye mitihani ya kidato cha sita (ACSSE) ambapo wanafunzi vilaza hupenya hadi kuingia vyuo vikuu. Na huko vyuo vikuu, mchezo ni uleule…..kazi inaendelea. Tazama mtihani wa uliotungwa kwa wanafunzi wa mwaka wa pili kutoka chuo kikuu kimoja hapa nchini Tanzania. Hali inatisha kwa kweli.
1642443384391.png

1642443635261.png

Mtihani gani wa kijinga kama huu? Unampima nini mwanafunzi wa chuo kikuu kwa mtihani wa kizembe kama huu? Tuache masikhara jamani; huu mtihani hata ukimtungia mwanafunzi wa darasa la nne atapasua pasi na shaka. Sasa iweje wanafunzi wa chuo kikuu tunaowategemea kuja kulitumikia taifa baada ya kuhitimu watungiwe mtihani wa ovyo kama huu? Inasikitisha sana, ten asana.

Jambo jengine ambalo serikali imeamua kulifanya kwa makusudi ni kuondoa penalty kwa wanafunzi wanaofeli hesabu (Mathematics) tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma. Pia somo la Bible Knowledge siku hizi linajumlishwa kwenye ufaulu ili kuwaboost wanafunzi wengi zaidi wapate divisheni wani za magumashi kisiasa. Tazama kielelezo kifuatacho:

1642444066249.png

Ndugu wadau wa elimu, sio mimi tu ninayelalamikia uchakachuaji wa elimu hapa nchini. Kila mtu ni shahidi juu ya uhuni unaoendelea katika kudidimiza kiwango cha elimu na kuwafanya watanzania wavivu wa kufikiri ili watawalike kirahisi. WanaJF wengine pia wamewahi kuguswa na jambo hili na kuliongelea kwenye nyuzi zifuatazo:

Wahadhiri vilaza huzalisha wasomi vilaza

Kwanini wahadhiri hawapelekwi tena kusoma 'postgraduate degrees' kwenye vyuo vyenye hadhi kubwa duniani kama ilivyokuwa zamani?

Nini kifanyike?
Nchi hii imefika mahali pabaya sana kielimu na endapo mchezo huu utaendelea, elimu ya nchi hii itaingia kaburini. Kumbuka kama tutakaa kimya, sisi na kizazi chetu chote tutaangamia pamwe! Je, nini kifanyike kurejesha elimu yetu kwenye reli? Karibu tujadiliane.​
 
History-Victory

JF-Expert Member
Sep 11, 2021
332
719
Tuanze kwanza na uongozi mzima kuanzia waziri mpaka huku chini kubadilisha mfumo..wakae watu wenye mawazo chanya watakao weza badili mfumo ila tatizo sisi watanzania kila mtu ana njaa na mwizi wakifika hapo wanajisahau wanafanya baishara ya elimu.
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
17,412
11,026
Wanaua Mfumo Wa Elimu Kisa Siasa.

Watoto hao wa darasa la nne ukienda kufatilia vizuri wengi hawajui kusoma na kuandika vizuri.

Tatizo la kuwa na viongozi wanapambania chama kuliko wananchi.
Ni Tanzania pekee ambapo wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wanafaulu mitihani ya kubet kwenda sekondari. Hii ni nchi ya kusadikika :oops: :oops: :oops:
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
17,412
11,026
Tuanze kwanza na uongozi mzima kuanzia waziri mpaka huku chini kubadilisha mfumo..wakae watu wenye mawazo chanya watakao weza badili mfumo ila tatizo sisi watanzania kila mtu ana njaa na mwizi wakifika hapo wanajisahau wanafanya baishara ya elimu.
Umeongea kweli 100% mkuu; hatuwezi kuwa na elimu bora ikiwa wachumiatumbo wataendelea kuwa watunga sera na wasimamizi wa sera zetu.
 
fasols

Member
Nov 7, 2013
39
35
Ni kweli kabisa NECTA hata mwaka huu matokeo wameyachakachua sana,elimu imekua biashara-watoto wengi wanapewa ufaulu wa qualification ya D nne ili wakawe masoko kwenye vyuo vya certificates hilo limejitokeza sana mwaka,
Elimu imekua siasa NECTA imeleta siasa kwenye elimu kiasi ambacho hata wasahishaji wa hiyo mitihani hawapewi thamani yeyote kimaslahi,haiwezekanai mwalimu ana mark form 2 na form 4 alafu anapewa laki 4,hivi unategemea mwl ata mark kwa weledi
Hata huko kwenye marking walimu wanaambiwa wafanye soft marking,ukikaza sana kwenye marking unafukuzwa
 
Artificial intelligence

JF-Expert Member
Jan 28, 2021
1,232
1,978
Watanzania tumerogwa; yaani tunafurahia matokeo feki huku elimu yetu ikizidi kushuka kila mwaka. Aliyeturoga kafa. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya matokeo ya darasa la nne (SFNA)....​
Kumbe hata zamani mitihani ilikuwa ni myepesi muno, sema zama hizo hapakuwepo na sources of referencing materials kama leo, huo mtihani ulioweka wa 1997 ni mwepesi sana pia. Kwahiyo acheni kuwananga watoto waliofaulu nyinyi wenyewe itakuwa mlikuwa vilaza tu.
 
blogger

JF-Expert Member
Mar 13, 2012
7,123
7,002
Tunaomba wastani wa 30 urudishwe badalanya divisheni katika mtihani wa upimaji kidato cha pili
Hata ukírudishwa watawapa marks za bure. Kumbuka mabeberu wanatoa mabílion kufadhilí elimu na. Hawataki failures
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
17,412
11,026
Watafeli wengi mzee.
Na pia darasa la 4 na 7 wapewe hesabu za kukokotoa achana na za majibu ya kuchagua
Hii mitihani ya kubet ndiyo hupelekea wanafunzi kufaulu kwenda sekondari ilhali hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu. Aliyeanzisha hii mitihani ya kubet alaaniwe hadi ukoo wake wote.
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
17,412
11,026
Ni kweli kabisa NECTA hata mwaka huu matokeo wameyachakachua sana,elimu imekua biashara-watoto wengi wanapewa ufaulu wa qualification ya D nne ili wakawe masoko kwenye vyuo vya certificates hilo limejitokeza sana mwaka,
Elimu imekua siasa NECTA imeleta siasa kwenye elimu kiasi ambacho hata wasahishaji wa hiyo mitihani hawapewi thamani yeyote kimaslahi,haiwezekanai mwalimu ana mark form 2 na form 4 alafu anapewa laki 4,hivi unategemea mwl ata mark kwa weledi
Hata huko kwenye marking walimu wanaambiwa wafanye soft marking,ukikaza sana kwenye marking unafukuzwa
Mkuu umeongea jambo la kweli kabisa. Kuna jamaa yangu huchaguliwa kwenda marking kila mwaka; wanaelekezwa kabisa kufanya soft marking, ukijifanya kukaza, wanakufukuza jumla na hawakuiti tena. Hii nchi ni ya ajabu sijapata kuona.
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
17,412
11,026
Watanzania tumerogwa; yaani tunafurahia matokeo feki huku elimu yetu ikizidi kushuka kila mwaka. Aliyeturoga kafa. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya matokeo ya darasa la nne (SFNA), kidato cha pili (FTNA) na kidato cha nne (CSEE) kutolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) hivi karibuni na kuonyesha kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia mbili (2%) ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2020.

Baada ya kufuatilia namna mitihani inavyotungwa na kusahihishwa kwa muda mrefu nimegundua kadri miaka inavyokwenda mbele mitihani inazidi kurahisishwa ili wanafunzi wengi zaidi wafaulu. Hii ni sera ya serikali kuongeza ufaulu kwa wanafunzi kila mwaka ili wapate cha kusema mbele za wazazi (wapiga kura) kila baada ya miaka 5 ya uchaguzi.

Nikianzia kwenye suala la utunzi wa mitihani, siku hizi mitihani inatungwa kwa urahisi sana na kwa njia ya ajabu. Tangu serikali ilipoanzisha mitihani ya kubashiri (kubet) wanafunzi wengi wasiojua kusoma wala kuandika hufaulu kujiunga na shule za sekondari na wanaendelea hivyo hivyo hadi kidato cha nne.

View attachment 2085385
Wanafunzi hawa wakifika kidato cha nne, serikali tena hutunga mitihani rahisi ili wengi wao wafaulu kujiunga kiadato cha tano kwa ubwete. Utafiti wangu umeonesha kwamba kadri miaka inayoenda mbele mitihani ya kitaifa kwa ngazi zote imekuwa ikirahisishwa kwa makusudi ili kuwafaulisha wanafunzi kisiasa. Tazama mtihani wa Biology wa NECTA 1996 ulinganishe na mtihani wa NECTA 2017 utapata jibu mwenyewe. Zamani kupata divisheni wani halikuwa jambo la mchezo. Lakini kwa maswali mchekea kama haya (2017) hata mkulima ambaye hakwenda shule hakosi kupata divisheni wani!

NECTA 1996
View attachment 2095342

NECTA 2017
View attachment 2085333
Hali ni hiyo hiyo hadi kwenye mitihani ya kidato cha sita (ACSSE) ambapo wanafunzi vilaza hupenya hadi kuingia vyuo vikuu. Na huko vyuo vikuu, mchezo ni uleule…..kazi inaendelea. Tazama mtihani wa uliotungwa kwa wanafunzi wa mwaka wa pili kutoka chuo kikuu kimoja hapa nchini Tanzania. Hali inatisha kwa kweli.
View attachment 2085338
View attachment 2085340
Mtihani gani wa kijinga kama huu? Unampima nini mwanafunzi wa chuo kikuu kwa mtihani wa kizembe kama huu? Tuache masikhara jamani; huu mtihani hata ukimtungia mwanafunzi wa darasa la nne atapasua pasi na shaka. Sasa iweje wanafunzi wa chuo kikuu tunaowategemea kuja kulitumikia taifa baada ya kuhitimu watungiwe mtihani wa ovyo kama huu? Inasikitisha sana, ten asana.

Jambo jengine ambalo serikali imeamua kulifanya kwa makusudi ni kuondoa penalty kwa wanafunzi wanaofeli hesabu (Mathematics) tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma. Pia somo la Bible Knowledge siku hizi linajumlishwa kwenye ufaulu ili kuwaboost wanafunzi wengi zaidi wapate divisheni wani za magumashi kisiasa. Tazama kielelezo kifuatacho:

View attachment 2085344

Ndugu wadau wa elimu, sio mimi tu ninayelalamikia uchakachuaji wa elimu hapa nchini. Kila mtu ni shahidi juu ya uhuni unaoendelea katika kudidimiza kiwango cha elimu na kuwafanya watanzania wavivu wa kufikiri ili watawalike kirahisi. WanaJF wengine pia wamewahi kuguswa na jambo hili na kuliongelea kwenye nyuzi zifuatazo:

Wahadhiri vilaza huzalisha wasomi vilaza

Kwanini wahadhiri hawapelekwi tena kusoma 'postgraduate degrees' kwenye vyuo vyenye hadhi kubwa duniani kama ilivyokuwa zamani?

Nini kifanyike?
Nchi hii imefika mahali pabaya sana kielimu na endapo mchezo huu utaendelea, elimu ya nchi hii itaingia kaburini. Kumbuka kama tutakaa kimya, sisi na kizazi chetu chote tutaangamia pamwe! Je, nini kifanyike kurejesha elimu yetu kwenye reli? Karibu tujadiliane.​
Zamani tuliaminishwa kwamba SIASA NI KILIMO lakini sasa hivi SIASA NI ELIMU. Taifa lolote linalochemekea siasa ndani ya elimu hilo ni taifa mfu na mfilisi. So, Tanzania ni mufilisi kielimu.
 
The MoNA

JF-Expert Member
Sep 19, 2014
1,729
3,230
Sijui kifanyike nini kuondoa mfumo wa mitihani ya sasa iwe kipimo cha mwisho cha kujua alichoelewa mwanafunzi.

Kuna upande wenye nguvu sana huo ukipunguzwa nguvu huenda mengine yatawezekana...

Sent from my Pro_Max11 using JamiiForums mobile app
 
BUKOBA LAND

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
7,292
14,523
Mtoa post , unabid uombe kwamba Elimu iwe ya vitendo zaidi kuliko theory how comes kufananisha vitu vya kijinga hata huo mtian wa 1996 was autodated.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

6 Reactions
Reply
Top Bottom