Amani Iwe Juu Yenu!
Poleni na mihangaiko ya hapa na pale kwa ajili ya kujitafutia riziki! Nisiwachoshe sana,ngoja niende moja kwa moja kwenye mada! Kuna siku mwezi uliopita nilikuwa mtaani,nikawakuta vijana wanajadili juu ya maisha ya ndoa! Walikuwa wanamjadili mwanamama fulani hivi mtaani let say tumwite X! Mmoja akasema yule mama X mpaka saizi hajapata mtoto na yuko around 40+ na yuko kwenye ndoa muda mrefu tu! Mwingine akasema usiwaone watu wanatembea barabarani, wanaendesha magari mazuri, wana maisha mazuri kumbe katika mioyo yao wana misukosuko mingi sana! Nilichukua muda kuwasilikiliza michango yao nami kutafakari juu ya hayo mawazo yao kwani ni mengi waliongea, kisha nikawauliza kwani MTU anapoamua kuoa au kuolewa, lengo lake au matazamio yake makubwa huwa ni nini! Mmoja alisema ni kurahisisha upatikanaji Wa lile TENDO kihalali na kwa muda unaotaka wewe. Wengine wote walisema lengo la kwanza kabisa huwa nikupata watoto, mengine haya ni mbwembwe tu! Leo nimeikumbuka hii mada nikaona niilete na kwenu pia ili mjaribu kutoa mawazo ambayo kwa namna moja au nyingine yatawasaidia wale walioko kwenye ndoa na wale tunaojiandaa kuingia!!
Karibuni kwa michango!!