Nini Lengo la kuoa au kuolewa?

Nini Lengo la kuoa au kuolewa?

Mimi kama Padri wenu mtarajiwa nawaleteeni mafundisho haya kuntu ili yawafae na Mungu awabariki.
1. Kwa manufaa yenu ninyi mnaooana kusudi kuepuka vishawishi na tamaa mbalimbali. Kimsingi, kila mmoja anaoa ili amfae mwenzake na kujitoa kikamilifu kwa ajili ya mwenzake. Mnaoana kwa sababu mnajotoa kimasomaso kwa ajili yenu. Waweza hapa kurejea maandiko Matakatifu kidogo Mwanzo 2:23.
2. Kuzaa na kulea watoto. Walioamua kuoana huishi pamoja wakitarajia kupokea zawadi ya watoto kama baraka kutoka kwa Mungu. Kukosa watoto hakufanyi mapendo yenu kuwa batili au pungufu. Mnapata watoto ili mshirikiane na Mungu kuendeleza kazi yake ya uumbaji.
Nakushukuru Padri mtarajiwa kwa ufafanuzi/mchango wako mzuri,lakini pamoja na maelezo yako mazuri, ningependa ufafanue zaidi pointi yako ya pili kwani katika utafiti wangu nimegundua kuwa wanandoa wengi waliooana kwa muda mrefu bila kupata watoto, ndoa zao huwa zinayumba sana hata wakati mwingine kupelekea kutengana.Mara nyingi vijana wanapooana matazamio yao hasa ya awali huwa ni kujiepusha na tamaa za mwili kama mtume Paulo alivyowambia Wakorintho , nanukuu "Ni bora kuoa kuliko kuwaka tamaa" Lakini baada ya kukaa Mwaka Wa 1, Wa 2 Wa 3 Wa 4 n.k bila kupata watoto malalamiko huanza mara oooh nataka mtoto mara ooh wewe hunifai hali ambayo hupelekea msongo mkubwa wa mawazo kwa wanandoa na hata amani kukosekana ndani ya ndoa! Je,nini ushauri wako kwa wanandoa inapotokea incidence kama hii,itapendeza zaidi pia kama utatoa reference kutoka kwenye Maandiko matakatifu ya Biblia!

Karibu Paroko mtarajiwa!
 
Unajua Linkedin, watoto ni zawadi itokayo kwa Mungu na huwezi kumlazimisha Mungu akupe zawadi mpaka atakapopenda na kuona kwamba inafaa akupe hiyo zawadi kwa sababu unahitaji kweli. Kwa hiyo mimi naona hivi, kwanza kabisa, wanandoa wanapotaka kutengana kwa sababu eti ya kukosa mtoto, ni lazima kwanzaa waangalie nafasi ya Mungu katika kuwajalia huyo Mtoto. Rejea maandiko Matakatifu habari ya Abrahamu na Sarah. Mwanzo 21. Mungu aliwajalia mtoto kwa wakati aliopenda yeye mwenyewe. Watoto ni zawadi tu kutoka kwa Mungu na inafaa wanandoa wakaelewa hivyo. Soma Zaburi 127:3. Vilevile kupata watoto kunaendana na kuwapa malezi sahihi na kuwakuza katika tunu njema za kiutu kusudi waweze kuifaa jamii na wazazi wao happ baadae. Ndugu Linkedin, kwa kifupi ni kwamba watu wanapoingia kwenye ndoa waingie ili kutekeleza na kuyakubali mapenzi ya Mungu, siyo mapenzi yao wenyewe. Sijui nimejaribu kukujibu au vipi
 
Sasa mfano umri wa kuoa umefika na muda uunaruhusu pia uwezo nnao kwanini nisioe na ikiwa sina sababu ya kuishi bachelor?mi nnavyofahamu mke ni msaidizi wangu,mlezi wa wanangu atakao nizalia.
 
Wengine wanaoa ili kutuliza mapepo ya ngono kwa sababu nivitombi kweli sasa akioa kidogo swansea yake inapunguza kusukuma zipu ya suruali.
 
Ni maumbile siyo binaadamu tu ndiyo wenye wenza wa maisha kuna wanyama na hata ndege wenye wenza wa maisha yote kwa hiyo tunaoa na kuolewa kama hatua katika maisha watoto ni majaaliwa zamani ilikuwa vigumu sana kujua mwanaume ana matatizo ya uzazi kwa sababu kwa baadhi ya makabila ilikuwa ruksa kusaidiana ktk tendo
 
Unajua Linkedin, watoto ni zawadi itokayo kwa Mungu na huwezi kumlazimisha Mungu akupe zawadi mpaka atakapopenda na kuona kwamba inafaa akupe hiyo zawadi kwa sababu unahitaji kweli. Kwa hiyo mimi naona hivi, kwanza kabisa, wanandoa wanapotaka kutengana kwa sababu eti ya kukosa mtoto, ni lazima kwanzaa waangalie nafasi ya Mungu katika kuwajalia huyo Mtoto. Rejea maandiko Matakatifu habari ya Abrahamu na Sarah. Mwanzo 21. Mungu aliwajalia mtoto kwa wakati aliopenda yeye mwenyewe. Watoto ni zawadi tu kutoka kwa Mungu na inafaa wanandoa wakaelewa hivyo. Soma Zaburi 127:3. Vilevile kupata watoto kunaendana na kuwapa malezi sahihi na kuwakuza katika tunu njema za kiutu kusudi waweze kuifaa jamii na wazazi wao happ baadae. Ndugu Linkedin, kwa kifupi ni kwamba watu wanapoingia kwenye ndoa waingie ili kutekeleza na kuyakubali mapenzi ya Mungu, siyo mapenzi yao wenyewe. Sijui nimejaribu kukujibu au vipi
Ni kweli Padri mtarajiwa, nimekuelewa vizuri kabisa kuwa watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Ukifuatilia vizuri Maandiko matakatifu utagundua kuwa kusudio kubwa kabisa la ndoa ni kuondoa UPWEKE, Rejea Mwanzo 2:18,si vema MTU huyu awe PEKEE yake, nitamfanyia msaidizi Wa kufanana naye. Kumbe Mungu aliona Adamu atakuwa mpweke kwahiyo akaona amletee msaidizi ambaye ni Eva.

Baada ya kumletea Msaidizi aliwabariki akawaambia nendeni mkazae muongezeke mkaitiishe dunia, Rejea Mwanzo 1:27-28. Kwa Maandiko haya Paroko tunajifunza kuwa Kuzaa au watoto ni baraka tu au zawadi kutoka kwa Mungu, ni sawa na MTU akanunua bandle la dakika 30 za airtel lakini baada ya kununua akapewa bonus ya MB 100,lakini lengo lake hasa ilikuwa ni muda Wa maongezi. Kwahiyo hata Mungu alitupa hiyo kama bonus au zawadi. Vilvile hakuishia hapo tu,alitupa pia mamlaka ya kuvitawala viumbe vingine vyote vilivyomo duniani yaani nchi kavu na majini, hii nayo naweza kusema ni bonus, ni nafasi ya pekee tuliyopewa.

Kwahiyo kitu cha msingi
Paroko kama ulivyosema ni watu tu kutokutambua kusudio la Mungu juu ya ndoa, Mungu hupokea maombi ya kila MTU lakini hujibu kwa wakati wake, huwezi kumlazimisha. Nikuombe kitu kimoja, wewe kama Padri mtarajiwa, utakapokuwa Padri/ Paroko kamili utoe hii elimu kwa wanakondoo wako, maana tunakoelekea changamoto za uzazi zinaongezeka hali ambayo itapelekea ndoa nyingi kuwa na migogoro kwa sababu ya utasa/ugumba!

Nikushukuru sana kwa mchango wako, na pia nikutakie masomo/malezi mema kwa ajili kututumikia hapo baadae!
 
Back
Top Bottom