Nini kirefu cha L.L.B na L.L.M

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Jan 2, 2011
303
154
Wanajamii, nimekuwa nikijiuliza muda mrefu sasa na pia nimeuliza hata wa wasomi a sheria kirefu na asili ya abbreviation L.L.B(shahada ya kwanza ya sheria) lakini huwa sipati jibu. Ukiuliza wanafunzi na wanazuoni wa sheria woe wamekuwa wakipata kigugumizi.
Sasa nalibwaga swali hili jamvini, nini maana yake? Maana tunajua ukisema B.A ni Bachelor of Arts. BSc ni Bachelor of science
 
LLB
abbreviation Latin Legum Baccalaureus (Bachelor of Laws)



The American Heritage® Dictionary of the English Language, 4th edition Copyright © 2010 by Houghton Mifflin Harcourt Publishing Company. Published by Houghton Mifflin Harcourt Publishing Company. All rights reserved.


pia angalia maana ya baccalaureate ktk kiingereza ni An academic degree conferred on someone who has successfully completed undergraduate studies this is according to wordweb Dictionary najaribu kufananisha na hilo neno la kilatin naona ni maneno yenye maana moja. please usiulize swali hata mimi nimekuwa nikijiuliza kirefu chake lakini nimetafuta kwenye net sasa hivi kama nilivyokupa references na kutokeo hapo tunaweza pata picha halisi walau ingwaje wanazuoni wa sheria wanaweza kutusaidia pia nadhani legum itakuwa inamaanisha kitu kama legal kwa hiyo ktunaweza sema ni latin legal law may be! sasa kwanini watumie hiyo? kwani wanasoma latini legal law! sasa kwa mtizamo wangu labda ni Ktindo tu au mazoea kama vile tunavyosema Daladala ingawaje ni kweli zamani ilikuwa sababu ya nauli sh Tano basi mabsi haya ya abiria yakaitwa Daladala lakini sasa mbona nauli ni sh250 tena imeongezwa 300 na bado tuanaita Daladala!


Nadhani hayo mazoea labda ndiyo yamepelekea hata degree ya sheria kuitwa LLB sababu wao labda walikuwa wa mwanzoni sana kutoadegree hiyo au ndiyo iliyoheshimika sana enzi hizo. hayo ni mawazo yangu tu lakini.
 
Zote ni Shahada . Maana zake ni


LL.B = Bachelors of Law
LL.M - Masters of Law

B.P (2011)
 
Wanajamii, nimekuwa nikijiuliza muda mrefu sasa na pia nimeuliza hata wa wasomi a sheria kirefu na asili ya abbreviation L.L.B(shahada ya kwanza ya sheria) lakini huwa sipati jibu. Ukiuliza wanafunzi na wanazuoni wa sheria woe wamekuwa wakipata kigugumizi.
Sasa nalibwaga swali hili jamvini, nini maana yake? Maa tunajua ukisema B.A ni Bachelor of Arts. BSc ni Bachelor of science
Mbavu za Mbwa, hakuna L.L.B wala L.L.M. Kilichopo ni LL.B na LL.M zinazosimamia digrii ya kwanzana ya pili ya sheria
 
Si kweli kwamba umewauliza wanafunzi na wanazuoni wa Sheria. Lazima ungepata majibu haya hapa chini:

Shahada ya kwanza ya Sheria inaitwa kwa kilatin Legum Baccalaureus
Shahada ya pili ya sheria ni Legum Magister
Legum Baccalaureus and Legum Magister are abbreviated LLB and LLM respectively.
The abbreviations LLB and LLM are accepted and used worldwide, although they are "technically incorrect"
 
kwani wanasoma latini legal law! sasa kwa mtizamo wangu labda ni Ktindo tu au mazoea kama vile tunavyosema Daladala ingawaje ni kweli zamani ilikuwa sababu ya nauli sh Tano basi mabsi haya ya abiria yakaitwa Daladala lakini sasa mbona nauli ni sh250 tena imeongezwa 300 na bado tuanaita Daladala!

daladala ilikuwa nauli ya wakati moja kutoka magomeni moja kwa moja kwa mabasi madogo ambayo wakati huo yalikuwa hayaruhusiwi (yalikuwa yanasanya) kwa sababu ruksa ya kusafirisha abiria ilikuwa ni kwa DMT tu na baadaye UDA peke yake. Wakati huo DMT/UDA walikuwa wantoza senti 30 (shilingi moja = senti 100) lakini mabasi madogo (vipanya) yakitoza Dollar (senti 50) kwa safari ya express.

macinkus
 
Kumbe kilatini.
Nilifikiri hiyo L nyingine wameiongeza bahati mbaya.
 
Kwa kilatini na lugha nyengine zenye asili ya kilatini, wanaruhusu kurudufu herufi ya mwanzo katika baadhi y majina yenye maneno mawili, kwa hivyo ni sawa Legum Baccalaureus kuifupisha kwa LL.B
 
Si kweli kwamba umewauliza wanafunzi na wanazuoni wa Sheria. Lazima ungepata majibu haya hapa chini:

Shahada ya kwanza ya Sheria inaitwa kwa kilatin Legum Baccalaureus
Shahada ya pili ya sheria ni Legum Magister
Legum Baccalaureus and Legum Magister are abbreviated LLB and LLM respectively.
The abbreviations LLB and LLM are accepted and used worldwide, although they are "technically incorrect"

ongeza iwe Legis Legum Baccalaureus kwa LL.B na LL.M LEGIS LEGUM MAGISTER
 
An LL.B. is the award of the degree of Bachelor of Laws. LL.B. is a Latin word. It stands for ‘Legum Baccalaureus’, signifying 'Bachelor of Laws'. In Latin abbreviations, the plural form of a word is indicated by doubling the letter- hence ‘LL.’ is short for Laws.
 
Back
Top Bottom