Kama wanawake wana huruma si aende kumwangukia aloponda nae maisha??? Au yeye si mwanamke?
Ndio maana tunapenda wanaume wafunguke...wanaona ugumu gani kuwaangukia hao nyumba ndogo zao? Ni kipi kinachowafanya wapate ujasiri wa kurudi kwa wake zao macho makavu after so many years?
Labeka BADILI TABIA, nimekuitika kwa kuwa kuna mtu kanambia unaniita....loh....
Nimeamini ndoa ngumu..... Na inahitaji haswa mkono wa Mungu.... Na nashukuru Kongosho umenifungua macho haswa....
Ila nashangaa Asprin ruttashobolwa Bishanga nitonye Judgement Erickb52 Dark City Mbu Mtambuzi na wengineo siwaoni hapa, waje kutueleza kinachowafanya kukimbia familia zao ni nini? Kwa nini wabadilika vichwa vyao vina nini humo ndani.......
Labeka BADILI TABIA, nimekuitika kwa kuwa kuna mtu kanambia unaniita....
Maadam kwa kuwa mie sina mpango wa kumkimbia mke wangu mpendwa, ee Mungu nisaidie:
Na kwakuwa sina sababu yoyote ya kumkimbia mke na familia yangu, ee Mungu nisikilize:
Na kwakuwa sina nia wala uwezo wa kumkimbia mke wangu, ee Mungu nihurumie,
Mimi ODM nasikitika kukufahamisha kuwa siwezi kuchangia lolote kwenye huu uzi kwa kuwa sina mpango wa kuwashauri wanaume mabaradhuli wenye tabia mbaya kama soli ya kiatu cha Mugabe.
Baada ya kusema hayo, naomba uzifikishe salamu zangu za upendo toka moyoni kwa wake zangu Yummy na cacico. Ukimuona Kongosho naomba umwambie ntamuoa tena na tena na tena mpaka atakaponiambia yatosha.
Narudi mapangoni Chechnya.
Ntawamisi sana.
Nakubaliana na wewe100%.. Imewai kumtokea babaangu mkubwa. Yeye alikua ni dereva wa magari makubwa akisafiri nchi kadhaa kupeleka mizigo,bahati nzuri mwanzoni mwa ndoa yeke alikua ni mtu mwenye malengo ya maisha akabahatika kujenga nyumba mbili nzuri,Moja alijenga katikati ya mji na nyingine pembeni kidogo. ya mjini ndio alikua anaishi na familia yake yenye watoto wadogo wawili ambapo mkubwa alikua ni miaka takribani mitano..sijui shetani gani alimpitia ndoa yake ikaanza kusumbua,familia yake ilikua mbeya alikua akitoka dar anapitiliza hadi zambia au Congo hivyohivyo akitoka Congo mpaka dar bila kuijulia hali familia yake..ikaja kungundulika baadae kuwa tayari anabi-mdogo zambia ambae anaishi nae kama mkewe. Mkewe baada kusikia hizo habari suku moja akamhoji. ikawa balaa,ulizuka ugomvi mkubwa sana... Siku moja mke hana hili wala lile alijikuta anaambiwa nyumba wanayoishi imeuzwa hivyo wahamie nyumba ya pembeni ya mji ambayo aliipangisha,na kumwambia kuwa hiyo ndio itakua nyumba yake hivyo wasijuane, mama mkubwa alijua utani, akashangaa miaka inakatika mmewe hakanyagi nyumbani,kuulizia jamaa zake wanasema yupo na anafanya safari zake kama kawaida ila mke wa Zambia ndio kama mkewe rasmi....amekuja kurudi mwaka jana huku akiwa amepooza upande mmoja wa mwili na kumpigia magoti mkewe kwamba anaomba msamaha maana huko Zambia bi-mdogo wametibuana, ni baada ya kuona jamaa anaumwa na hana uwezo tena wa kufanya majukumu kama awali akaamua kumtelekeza...baba mkubwa alirudi na kabegi tu kenye nguo chache huku hata hele ya kujiuguza hana....mke alijaribu kumkataa lakini vikao vya familia vilisaidia kumrudisha kwe mstari akakubali kumpokea kwa masharti kuwa atapewa chumba chake binafsi kama msaada huku familia ikichangishana kuhusu matibabu yake..mtoto aliemwacha na miaka mitano anarudi mwaka jana yupo kidato cha kwanza.!!
So sad. Ndio maana nasema hao dawa yao ni kuwatimua wauguzwe na ndugu zao.
Kama mama yake yuko hai akamuuguze...si alijifanya mjanja. Je angemkuta mkewe kaolewa?
Mkiama muwege na plan B. Na plan B yenyewe isiwe wife ulomtelekeza.
Paloma,
inasikitisha sana.....
Unamsamehe mtu, anakuja kukuambukiza maradhi!!!!!!!
Hapa unakua umeokoa nini? Ndoa? Na watoto kuwaachaje?
Hii inadhihirisha ubinafsi wa wanaume, hivi mwanaume ameathirika, anarudi kwa mkewe na anafurahia tendo la ndoa na kumuangamiza mkewe, ni mzima kweli upstairs?
Labeka BADILI TABIA, nimekuitika kwa kuwa kuna mtu kanambia unaniita....
Maadam kwa kuwa mie sina mpango wa kumkimbia mke wangu mpendwa, ee Mungu nisaidie:
Na kwakuwa sina sababu yoyote ya kumkimbia mke na familia yangu, ee Mungu nisikilize:
Na kwakuwa sina nia wala uwezo wa kumkimbia mke wangu, ee Mungu nihurumie,
Mimi ODM nasikitika kukufahamisha kuwa siwezi kuchangia lolote kwenye huu uzi kwa kuwa sina mpango wa kuwashauri wanaume mabaradhuli wenye tabia mbaya kama soli ya kiatu cha Mugabe.
Baada ya kusema hayo, naomba uzifikishe salamu zangu za upendo toka moyoni kwa wake zangu Yummy na cacico. Ukimuona Kongosho naomba umwambie ntamuoa tena na tena na tena mpaka atakaponiambia yatosha.
Narudi mapangoni Chechnya.
Ntawamisi sana.
BADILI TABIA hawa hawakurudiana kiasi cha kuendeleza unyumba!
Yule mama mmoja alipata taarifa kuwa mzee yupo taabani. kwenda kumuona ndio ikabidi amhamishie hospitali ambapo after some time alifariki. Kwa hiyo huyu mama alimsindikiza hadi mauti wakati nyumba ndogo alimuacha akiwa hana kitu -NIL!
Huyu aliyepigiwa simu yeye aliambiwa tu mumeo kalazwa wodi flani kauguze! Akaenda siku ya kwanza kumuona, siku ya pili anaambiwa kavuta kamba! akamuandalia makazi yake ya milele (mazishi)
swali, why hao nyumba ndogo hawako committed kama kweli wanataka mume? why dont they escort those guys to their death days?!?! Why hawa wamama ndio wabebe mizigo ya kuwasindikiza mautini? NI upendo, huruma au nikitu gani hii?
Nakubaliana na wewe100%.. Imewai kumtokea babaangu mkubwa. Yeye alikua ni dereva wa magari makubwa akisafiri nchi kadhaa kupeleka mizigo,bahati nzuri mwanzoni mwa ndoa yeke alikua ni mtu mwenye malengo ya maisha akabahatika kujenga nyumba mbili nzuri,Moja alijenga katikati ya mji na nyingine pembeni kidogo. ya mjini ndio alikua anaishi na familia yake yenye watoto wadogo wawili ambapo mkubwa alikua ni miaka takribani mitano..sijui shetani gani alimpitia ndoa yake ikaanza kusumbua,familia yake ilikua mbeya alikua akitoka dar anapitiliza hadi zambia au Congo hivyohivyo akitoka Congo mpaka dar bila kuijulia hali familia yake..ikaja kungundulika baadae kuwa tayari anabi-mdogo zambia ambae anaishi nae kama mkewe. Mkewe baada kusikia hizo habari suku moja akamhoji. ikawa balaa,ulizuka ugomvi mkubwa sana... Siku moja mke hana hili wala lile alijikuta anaambiwa nyumba wanayoishi imeuzwa hivyo wahamie nyumba ya pembeni ya mji ambayo aliipangisha,na kumwambia kuwa hiyo ndio itakua nyumba yake hivyo wasijuane, mama mkubwa alijua utani, akashangaa miaka inakatika mmewe hakanyagi nyumbani,kuulizia jamaa zake wanasema yupo na anafanya safari zake kama kawaida ila mke wa Zambia ndio kama mkewe rasmi....amekuja kurudi mwaka jana huku akiwa amepooza upande mmoja wa mwili na kumpigia magoti mkewe kwamba anaomba msamaha maana huko Zambia bi-mdogo wametibuana, ni baada ya kuona jamaa anaumwa na hana uwezo tena wa kufanya majukumu kama awali akaamua kumtelekeza...baba mkubwa alirudi na kabegi tu kenye nguo chache huku hata hele ya kujiuguza hana....mke alijaribu kumkataa lakini vikao vya familia vilisaidia kumrudisha kwe mstari akakubali kumpokea kwa masharti kuwa atapewa chumba chake binafsi kama msaada huku familia ikichangishana kuhusu matibabu yake..mtoto aliemwacha na miaka mitano anarudi mwaka jana yupo kidato cha kwanza.!!
habari zenu wapendwa,
binafsi hili ni swala ambalo nimeliona likitokea ila sijalipatia jibu. Sijui kama lilishajadiliwa humu au la na kamchina kangu hakawezi kusearch.....
Ni hivi inakuwaje kwa wanandoa, hususan mwanaume anatelekeza familia yake miaka kadhaa, hata kumi..... Ila akishafika uzee/utu uzima anarudi kwa mkewe?
Na inaiuwaje mke, mume anaporudi miaka kumi-ishirini baadae unampokea? Na mnaendeleza gurudumu?
Saa nyingine mume akiumwa hoi hoi hurudi kwa mkewe na mke huyu humuuguza mkewe?
Wanaume nini kinawaondosha kwa wake zenu? Na ninu kinawarudisha?
Wanawake mnawaza nini mnapowapokea tena waume zenu? Nini kinawasukuma kuwapokea?
Je hili lina madhara gani kwa watoto? Haiwaadhiri? Huwajenga au huwabomoa?
Natarajia majibu toka kwenu........
hata mie natamani wajibu, lakini na uhakika hawana jibu la mantiki.
Hivi unadhani wanaweza kwenda angukia nyumba ndogo? Hata kama nyumba ndogo hazijawafukuza, hivi kuna mwanamme anakubali msiba wake ufanyike kwa nyumba ndogo?
Wewe hawakuudhi, mie wananiudhi hadi nataka kupasuka ila basi tu.
Hapo ukute nyumba kubwa itaambiwa imeroga.
Hii statement hii
Utakuwa umeisema tu kama mfano
Lakini mie nimeona kwa macho yangu
Ni story ndefu lakini ndio huwa hivyo