Nini kimeyakumba mabasi ya mwendokasi

Dec 13, 2018
30
140
NINI KIMEIKUMBA MABASI YA MWENDOKASI.

Leo 13:15pm,09/04/2019.

Leo nilikuwemo katika gari ambayo imejaa hadi imeshindwa kwenda,mipira ya matairi ikaanza kunuka kuungua ikabidi dereva aombe gari nyingine ije kupunguza watu,Basi nyingine ikaja watu wakapungua ile basi ikajaa na bado hii basi iliyogoma kwenda ikawa bado imejaa,Unaweza kutambua ujazo ulikuwa mara tatu ya basi.

Mimi ni muumini mzuri wa Mabasi ya Mwendokasi maana yamenisaidia sana,Hatuamki tena saa kumi toka Mbezi kuja Posta, hatuamki tena saa kumi na moja toka Kimara kuja Posta au Kariakoo,jioni hatufiki majumbani saa tatu usiku,hatuchukui masaa matatu hadi manne toka Posta hadi kimara,Mwendokasi imetufanya kutumia nusu saa toka Posta hadi Kimara.

Tuliyoyatarajia kwenye Mwendokasi sio tunayoyapata sasa, Unakaa kituoni Saa nzima, basi moja linakuja kituoni baada ya nusu saa. Msururu wa watu wanagombea kuingia katika basi wakitumia mwendo wa kasi kupita mlangoni. Watu wanatoka bila viatu maana ukiinama kuokota kiatu chako basi watu wanakukanyaga,Hakuna Ustaarabu tena, Jasho la mwenzako linakuwa jasho lako, kupumuliana humo humo, hewa ya mwenzako inakuwa hewa yako,kama umetoka Kariakoo ukanunua nyanya kwa ajili ya nyumbani basi wakati wa kugombania watu watazibinya nyanya zako, zikianguka chini watu watazikanyaga kanyaga, Ukitoka kivukoni basi mtu aliyebeba Samaki atakupaka na shombo lote la Samaki, maji maji yote ya Samaki yatakuwa yako.

-Kwa nini watu wanajazana kwenye basi moja.

Kama gari ingekuwa inafika kituoni kila baada ya dakika tano,basi watu wasingegombania vile kiasi cha kuhatarisha maisha, Kama gari ingefika kituoni kila baada ya dakika tano basi utamaduni na ustaarabu wa kusubiri basi lingine ungejengeka katika jamii ya watu. Watu wasingejazana kwenye basi moja kiasi cha kusababisha basi kushindwa kwenda.

-Mwendokasi sasa ni Mwendokusubiri na kugombania.

Nashukuru kuwa nimewahi kutumia usafiri wa umma (public transport) wa nchi mbili tatu nilizojaaliwa kutembelea.

Nashukuru Usafiri wa Umma wa viwango vya mwendokasi kwa hapa Tanzania mbao umetupa fursa ya kwenda route ndefu ya mwendokasi kwa gharama nafuu, mfano wa Gerezani-kimara-mbezi bila kuunga unga na kwa kutumia muda mchache.

Unaweza kujiuliza kwanini uchome mafuta kutumia gari binafsi na kuna mwendo kasi,Unaweza kukubaliana nami kutumia mwendokasi kuokoa muda na mafuta.

-Kizaazaa na adha.

Kizazaa na adha utayokumbana nayo kwa kutumia usafiri huu wa Mwendokasi kwenda na kurudi ni tofauti na usafiri wowote wa umma unaoweza kutumia kwingine duniani na sidhani kama utarudia kwenda na mwendokasi.

Ikanikumbusha enzi za msemo daladala haijai na usafiri wa masaa matatu toka posta hadi kimara,

Tulianza kwa kutumia kadi,hivi sasa mashine za tiketi hazifanyi kazi.Ukipita na risiti ya kuchana hilo basi sasa, unangoja mpaka saa nzima na ukipata la kugombania,ingia mfano mikanda ya kujizuwia unaposimama mibovu. Basi la kugombania wakati wa kupanda. Basi linajaza kupita kiasi (mminyano kama enzi za uda). System za kuongoza vituo hazifanyi kazi. Dereva nae kimya hatangazi kwenye PA system yake. Basi ndani joto na hewa ni nzito sana kwa watu kujazana.

Kwa ufupi, wahusika wote wanaousimamia kuuendesha huu usafiri wameshindwa kabisa,Naamini ni kukosa Management yenye weledi kuendesha mradi huu.

Kwa ninayoendelea kuyaona kwenye Mwendokasi na Wakuu wamekaa wanamsubiria Mh Rais aje kutatua, hii si sawa kabisa, bado tuna safari ndefu sana ya kwenda.

-Je Watanzania tunashindwa kuendesha miradi mikubwa.

Hivi bado tunasubiri wazungu au Wakenya waje watuendeshee makampuni yetu?Je tatizo ni la kuwapa makampuni hawa watanzania makanjanja janja janja..wengi wamebinafsishiwa kwa kutumia janja janja kwa pesa ya kutupa.

Katika biashara naona inalipa ni hii ya mwendokasi.Kama usimamizi utakuwa mzuri, ikiendeshwa inavyostahili ni biashara yenye abnormal profit. Sijui kwanini Serikali na mdau mwekezaji pacha hawaoni hili. Ni aibu sana kufikiri kama tungejaribu kuwapa mabeberu waundeshe hata kwa mwaka mmoja tu halafu tujifunze kwao.

Mradi ni mizuri sana na unastahili kila sifa. Ubovu ni uendeshaji na kwa Sisi Watanzania hili ni toka enzi za Nyerere hallijaanza leo wala jana.

Tuna tatizo kubwa sana halihusiani na vyama,hii ni tatizo la vinasaba vyetu ambavyo vimeshindwa kupata exposure na kuacha wachina, Wahindi, wazungu waje hapa kwetu wakiwa na shati na suruali na dola mia mfukoni lakini baada ya mwaka ana bilioni moja kwenye account ya benki, ni wakati wetu sasa Watanzania kuonyesha tunaweza na tuisaidie nchi yetu, si kusubiri Wakenya waje na ukanjanja wao na kiingereza nusu na kujifanya mkoloni wa pili,haiwezekani.

-Nauguza jeraha la mwendokasi hapa.

Kukaa kituoni masaa mawili unasubiri basi lisilo na vurugu upande ni uvumilivu wenye ujinga ndani yake,Unachekewa kazini inakupasa ugombanie, Mke wangu ni wiki ya pili anauguza jeraha la mwendokasi baada ya kuminywa na watu wenye miguvu wakati wakigombania kupanda Mwendokasi, Jioni ya leo nikaenda kupandia kituo cha Gerezani, nilikuta watu wengi mno na basi takribani ishirini zimepark pembeni, Wananchi wanajiuliza wenyewe wanajijibu wenyewe kuwa mabasi hayo ni mabovu, kuna moja likaja wananchi wanapata amani sasa basi linakuja lakini basi lile likaenda kupark kwenye msururu wa mabasi yanayosemwa ni mabovu, dereva kazima kashuka kasahau kufunga mlango, Nikaona Wananchi wanakimbilia, dereva kutahamaki basi limejaa hadi mlangoni,ikamlazimu dereva kuingilia dirishani na kuwasha basi kupeleka abiria Kimara. Kwa nini iwe hivi, Wamama na Wababa baada ya kugombania wananung'unika wanasema haya ndio maisha tuliyoyachagua, kweli jamani!!? Naamini Uongozi wa Mwendokasi unataka kuikomoa Serikali, hii si sawa.

Nimalizie kwa kusema Mradi ni mzuri sana na unastahili kila aina ya sifa. Ubovu ni uendeshaji wa mradi huo na kuwakwaza wasafiri ambao Mwendokasi ndio tegemeo lao kwa sasa, Niitie moyo Serikali iendelee na Mwendokasi phase two na three lakini itafute mwekezaji mwingine, pengine Emirates atatufaa zaidi, Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kuibariki Tanzania, tupe neema ya kuzitumia vyema baraka ulizotujaalia.

Nikiishia hapa, Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.
 
Maendeleo hayana chama. Gharama za chaguzi zote za marudio za madiwani na wabunge wa upinzani zingetosha kununua magari ya kutosha ya mwendokasi na kutanua huduma hii temeke, mbagala na bunju. Lakini wapi, tumebaki kulishana matango pori kuwa demokrasia ina gharama zake.
 
Sasa unatuuliza sisi tena???

Sio umuulize muhusika unaemsifiaga??

Sisi haituhusu

Sent using Jamii Forums mobile app
Inasikitisha sana maana mamlaka husika imeshindwa kusimamia huu mradi pamoja na ahadi zisizotekelezeka za kumleta mbia mwingine. Hii habari tumenza kuisikia tokea mwaka jana lakini hadi sasa no one cares. Hata hili nalo linamsubiri Mh. Rais aseme jamani?
 
Inasikitisha sana maana mamlaka husika imeshindwa kusimamia huu mradi pamoja na ahadi zisizotekelezeka za kumleta mbia mwingine. Hii habari tumenza kuisikia tokea mwaka jana lakini hadi sasa no one cares. Hata hili nalo linamsubiri Mh. Rais aseme jamani?
Huyo raisi si ndio one player, hatoi pasi kwa wengine, ndio maana wameacha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili linadhihirisha hatuna uwezo wa Ku simamia miradi kama hii, kuamzia kwenye mchakato wa kupata mtoa huduma na hadi usimamizi kwa waliopewa mamlaka ya kusimamia mtoa huduma, wapo wanalipwa mishahara kwa kodi zetu lakini hawafanyi kazi yao ipasavyo, niliwahi kuwaza kwa nini Udart, Dart na yeyote anayehusika asiwajibishwe mapema, je ni nani anayeogopeka kwenye mradi unaohusu watu zaidi ya laki mbili kwa siku, ?

Tafadhari wahusika kama ni TAMISEMI au SUMTRA au DART wahurumieni wakina mama, kinababa, wanafunzi, walemavu na wagonjwa ambao Mwendokasi ndio njia pekee ya usafiri waliyo nayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh, hapo ndio Robert Kisena amelifikisha Mwendokasi, kaipora kwa wizi wizi, sasa ana case sijui yuko ndani au wapi..!! Serikali ichukue 100% ya hii mwendokasi iweke watu very serious kusimamia kama mm Jay One..!!
 
Mwafrika anaweza kujitawala katika maneno yake,lkn kujisimamia ni tatizo.
Miundo mbinu ya mwendokasi ni rafiki sana kwa sababu kuna mkono wa mzungu,uendeshaji wa mradi ndiyo tatizo kuu.
Wala hakuna jipya hapo,tulikuwa na UDA sijui kaburi lake liko wapi.
Tulikuwa na TTC,ATC,RTCs,KAMATA,TRC,TAZARA,na makampuni mengine ya uma,yote yako kaburi.
Serikali haiwezi kufanya biashara.
Mh Magu hakushauriwa vizuri. Kazi ya serikali si kufanya biashara,ni kuendesha serikali kwa kuweka miundo mbinu rafiki na kujiendesha kwa kutoza kodi. Biashara waachiwe wafanya biashara.
Kwa sasa hawa ndugu hawaelewi,basi waangalie hata historia ya makampuni ya uma niliyoyataja.
Mi naangalia tu jinsi hiyo reli ya kisasa wanayoijenga,itakapokamilika! Wataiendeshaje? Ili hali hawana uwezo wa kuiendesha?
Itakufa kifo cha kawaida kama vifo vya mashirika na makampuni yaliyotangulia.
Yetu macho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo Rais aliwaambia wasiwe wanafanya kazi hadi awepo yy?

We think too small, like the frog at the bottom of the well. He thinks the sky is only as big as the top of the well. If he surfaced, he would have an entirely different view.

Uwepo wa taasisi imara zilizojengwa kiufanisi huleta ufanisi wenye matokeo chanya kwenye jamii nzima..

Uwepo wa taasisi zilizoundwa kisiasa huleta matokeo chanya kwenye siasa na kwa wanasiasa..
 
Back
Top Bottom