Badala ya kua suluhisho la tatizo la Usafiri hapa Jijini .Mwendokasi imekuwa Ni MwendoShida kwa kweli.Ni iombe mamlaka inayo Shughurikia Usafiri huu hapa jijini Wajipange upya kwani kumekua na matatizo makubwa sana kwenye Usafiri huu.Kwanza ni mabasi kujaza abiria kupita kiasi .(2) Ni waombe waondoe utaratibu wa Express.kwani huu utaratibu huu umekuwa Ni mwanya kwa madereva wa mabasi haya kupita vituo vidogo hata kama yapo tupu na wakati kwenye vituo hivyo wapo abiria .(3),Kwenye mabasi haya pale malangoni kuna eneo limeandikwa si ruhusa kusimama hapa.lakini eneo hilo utakuta wame simama Watu zaidi ya Kumi.kwa maana hiyo kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria kwenye mabasi haya(4)Vifaa Vingi katika mabasi haya kwa sasa havitumiki ipasavyo kama Vipaza sauti madereva awavitumii kabisa na hata yule dada anesema kituo kinachofata siku hizi asikiki zaidi ya Siku kama Simba Sc inacheza ndio utawasikia washabiki wa timu hiyo wakisema huko mitaani .(5)Vituoni kumekuwa na uvujaji mkubwa wa mapato .na haswa huu mtindo wa ukinunua tiketi na kuchanwa pale na wale wahudumu pale kwenye kigeti cha mwisho .sasa awa Wahudumu sio malaika tiketi zingine azichanwi matokeo yake zinarudi dirishani kuuzwa tena .(6) ni dhuruma tuliyo fanyiwa sisi tuliouziwa kadi .sasa kadi hizi aziwezi kununua huduma matokeo yake zimekuwa ni mapambo kwenye Waleti zetu na kwenye mikoba .tuwaombe wafanye mpango wachukue kadi zao wazipeleke jumba la makumbusho.Na Mwisho kabisa ni lugha mbaya kwa wahudumu wa Vituoni unapotoa Noti ya shilingi Elfu kumi au tano.Utazania Umetoa pesa ya kuzimu kwa maneno utakayotolewa na muhudumu .matokeo yake utangandishwa pale mpaka chenji ipatikane .Kusema kweli kuna mambo mengi sana kwenye Usafiri huu wa Mwendo Shida mwendo tabu .niwaombe askari wa Usalama barabarani waanze kukagua haya mabasi waone uvunjifu wa sheria kwenye mabasi haya .ni vizuri kuzuia kuliko kutibu.Asante naomba kuwakilisha
Sent using
Jamii Forums mobile app