Nini kimemsukuma Msigwa wa Ikulu kuposti picha hizi mtandaoni siku ya leo akidai ni kumbukumbu?


..hoja yako ina ukweli 50%.

..kitu ambacho hukukizungumzia ni mwenendo wa ccm tangu Magufuli awe mwenyekiti wa chama.

..ccm ya Magufuli imefichama ndani ya dola na mahakama na ndiyo maana unaona ktk u
awamu hii vyama vya upinzani vinasumbuliwa na polisi / vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na mahakama kila wakati.
 
Nadhani anamaanisha Mh. Rais Magufuli ni mtu wa watu, anawapenda watu bila kujali mlengo wa kisiasa. Yaani hana ubaguzi.
 
Africa hawajui kinachoitwa upinzani. Africa wanajua kiongozi ni mfalme na hapaswi kukosolewa. Hii dhana inawasumbua sana viongozi (watawala) wetu.

Tazama hata bungeni ni kuviziana ni nani anajadili nini !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ukweli mkuu..afu anafanya maigizo pale jumapili kanisani...
 
Wapo wabunge wanatofautiana vyama na wenziwao, pia wapo waume na wake zao wanatofautiana dini na maisha yanaendelea.
 
Ni picha moja tu isiyoweza kuwekwa hapo hata kama ipo.

Ni ile ya Tundu Lissu.
 
Hiyo michango mngenipa hata mie kuliko vile.

Siasa haina uadui wa kudumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mnatumia hii misemo ya watu vibaya na kupotosha maana yake.

"Siasa haina uadui wa kudumu" - akikuua kwa siasa bado utasema siasa haina uadui wa kudumu?

Anakupa kilema cha maisha bado unaimba "siasa haina uadui wa kudumu"?

Hiyo ni akili toka wapi kama sio matope.
 
katika muda ambao viongozi wetu hawaishi kuitwa mahakamani. katika nyakati ambapo viongozi wetu wanapigwa na kujeruhiwa kiasi cha kulazwa.

hizi status za msemaji wa Ikulu twitter zina maana gani?
 
Maendeleo hayana vyama!

Hii kauli ina ukakasi mkubwa Sana!
Magufuli anazuia Wapinzani kutofanya mikutano na vikao vya ndani hasa CHADEMA....! Lakini pia ananyanyasa Wapinzani kwa kuwakamata na kuwafungulia kesi za KUWAKOMOA!!!

Kwa maana ya kauli hii ya Magufuli MAENDELEO NI YA CHAMA CHA CCM!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…