Ndiho
JF-Expert Member
- Feb 23, 2013
- 2,306
- 1,536
Tatizo humu jukwaani watu huwa wanachukulia vitu kwa msimamo mkali utasema dini, ukienda against tu unaonekana upo upande wa pili kiitikadi wakati kinachotakiwa ni kuangalia kwa jicho la kawaida na umuhimu wa safari ya mheshimiwa nje ya nchi maana kama alitangaza ingekuwa vyema na yeye akawepo na kwa vyovyote hiyo safari sio dharula hivyo kulikuwa na possibility ya kuangalia kufanya maandamano kwa siku za usoni baada ya yeye kurudi. (akingefanya hivyo ingewapa hamasa zaidi wananchi na wafuasi wake, hasa wale waliojitokeza bila kuitwa juzi kati wakati anakwenda kuhojiwa mpaka ikapelekea wakapigwa pamoja na waandishi wa habari)
Sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana. Wewe unakandia, kisha wakati huohuo unashauri na kujaribu kuelekeza. kwani wafuasi wa Mbowe na Chadema ni lazima wafurahi au kufanya vile unataka wewe? Sometimes kujifanya unajua kwa mambo yasiyokuhusu ni "UMALAYA WA MDOMO" Mbowe kusafiri au kutosafiri, kushitiki au kutoshiriki maandamano ni isue ya Wanachadema wenyewe, wewe inakuhusu nini?