Nini kimempeleka Mbowe huko South Africa?

Nini kimempeleka Mbowe huko South Africa?

Nadhani ameenda huko ili kujipongeza kwa kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa mwenyekiti wa Chadema.
 
Maandamano yapo wapi kamanda tufahamishe, Mbowe ni msanii wa kisiasa anachotaka yeye ni mtaji wa kisiasa watu wapigwe risasi apate agenda mpya.


Wachangiaji wengi zaidi wanashadadia habari ya watu kupigwa risasi, kuumizwa na maelezo ya jinsi hiyo kama kwamba ni jambo sahihi sana kufanyika. Swali na mshangao wangu ni kuwa kwa nini mnaona kuwa kuna uhalali wa watu (hata ingekuwa Mbowe au Kikwete), wapigwe risasi au kuumizwa kwa kisa kipi? Kuna uhalali wa kufanya hivyo! Kuandamana tu ndio mbinu itumike ya kuua au kuna agenda nyingine! Kuna kitu serikali ya Tanzania inaficha au kukwepa ambacho kinatokana na maandamano?
Najiulizaga bila jibu maswali haya. Wanafunzi wa vyuo wakiandamana kudai haki ni hayo hayo, si serikali iwapatie wananchi haki zao ili wasiandamane?
Hayo ndio madhara ya kujisifia sifa usiyokuwa nayo, ooh Tanzania nchi ya amani, mara nchi ya demokrasia- matokeo yake hata polisi hawana demokrasia, wanalazimika kuua na kuumiza hata kama hawapendi na hawana faida na mauaji hayo
 
Back
Top Bottom