Nini kimemkuta Dkt. Dorothy Gwajima hajawa mbunge?

Nini kimemkuta Dkt. Dorothy Gwajima hajawa mbunge?

Watu wengine sijui mna ubongo wa aina gani. Mnajadili hawa wauaji kuwa ni serikali? Hivi wewe kwa akili zako za kawaida unaona watu wote waliouawa na kutekwa na hizi kesi za uhaini zinazofungulia kila kona ya nchi, mambo yako sawa mpaka uanze kuongelea teuzi? Hujui unahalalishi mauaji na unyama wote uliotokea? Mpaka likupate jambo gani ndiyo utajua kuwa hatuko kwenye kipindi cha kawaida.
Kwamba usipojadili ndio haya mauaji yanaishia yenyewe automatically...???

Kijana unatakiwa kufikiri na kujitambua kisha kuchukua hatua..

Haki huwa haiji kama kikombe cha chai bali hupambaniwa...
 
Nasikia hakugombea ubunge Jimbo lolote.

Kwenye uteuzi wa wabunge wa viti maalum (KE) pia hayumo..

Alikosea wapi huyu mama mchapakazi wa wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum?
Muda bado japo lolote linawezekana
 
Nasikia hakugombea ubunge Jimbo lolote.

Kwenye uteuzi wa wabunge wa viti maalum (KE) pia hayumo..

Alikosea wapi huyu mama mchapakazi wa wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum?
Watu waadilifu, waaminifu, wazalendo kama Slaa,Gwajima wanaondelewa na Samia.

Anahitaji mafisadi, majambazi kwenye nafasi zote muhimu.
 
Kwamba usipojadili ndio haya mauaji yanaishia yenyewe automatically...???

Kijana unatakiwa kufikiri na kujitambua kisha kuchukua hatua..

Haki huwa haiji kama kikombe cha chai bali hupambaniwa...
Nakubaliana na wewe ila wewe hukujadili mauaji bali uteuzi wao wa kihuni.
 
Yule ni Daktari. Wanasiasa walimtoa kwenye wizara ya afya wakampa vyeo.

Hataki kugombea cheo chochote
 
Labda alikuwa ana leak information kwa shemeji yake Gwajima
 
Huyu maza anapendwa sana
Hutakiwi kupendwa kuliko bosi kubwa, huyu nafikiri ndio waziri pekee aliyeweza kupost mambo instagram na X bila kufunga comments na kuwasiliana na raia katika hali ya utulivu....ngoja tuone kama atarudishwa au ndio imetoka
 
Ingawa huyu mama hana elements za uchawa ninatamani ateuliwe kwani kawatetea sana wanawake na watoto walionyanyaswa kijinsia kila mtu aliona
 
Mwanzo aliteuliwa na raisi kuwa mbunge labda atateuliea kwenye viti 10 vya rais,kwa maoni yangu Bora hata asiteuliwe kwenye hii serikali ya mchongo
 
Nasikia hakugombea ubunge Jimbo lolote.

Kwenye uteuzi wa wabunge wa viti maalum (KE) pia hayumo..

Alikosea wapi huyu mama mchapakazi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum?
Akili zingine, hivi mtu asiposhiriki hata tu zile kura za maoni..hupati tafsiri ya kufanya hivyo hadi unauliza..? au hdi atamke kwa mdomo HATAKI!
 
Back
Top Bottom