Dear_me_

Member
Dec 31, 2022
31
76
In 2008, mfumuko wa bei ulifikia viwango vya juu sana, na kusababisha dola ya Zimbabwe kupoteza thamani yake na serikali kuiacha mnamo 2009. Tangu wakati huo, dola ya Marekani na sarafu nyingine za kigeni zimekuwa zikitumika sana katika uchumi.

Juhudi walizofanya wakiamini wataweza kuirudisha thamani hela yao

Katika jitihada za kurekebisha kushuka kwa thamani ya sarafu ya Zimbabwe, Benki ya Kuu ya Zimbabwe iliongeza tu juhudi zake za kuchapisha pesa na kuzipa sarafu zake thamani mpya kutoka kwa noti za Z$5, Z$10, na Z$20 hadi kuwa noti za Z$100,000,000 na Z$200,000,000. Iliendelea kuchapisha na bila ku update viwango vya ubadilishaji wa sarafu za kigeni (foreign exchange) au inflation rates na kutangaza mfumo mpya wa sarafu bila kushughulikia sababu za msingi za mfumuko wa bei.

Hali iliyozidisha kupungua kwa imani ya raia katika uthabiti wa sarafu hiyo.

Mabadiliko haya yalienda mbali hadi noti za Z$100,000,000,000,000 (Trilioni Moja) zilipoingizwa kwenye mzunguko.😂😂😂

Hii ilifanya dola ya Zimbabwe kupoteza thamani kabisa, ikawalazimisha watu kubadilishana bidhaa (nipe😂 nikupe)au kutumia sarafu za kigeni kwa ajili ya miamala. Kwa sababu hiyo, Black market ikawa njia ya kawaida ya kupata bidhaa na huduma za msingi kwa thamani iliyokuwa na unafuu kidogo, licha ya matumizi ya sarafu za kigeni kuwa illegal

KUMBUKA TRILIONI 100 KWENDA USD NI 40 cent au 1,088 TZS
 
Attachments

  • IMG_4781.jpeg
    IMG_4781.jpeg
    197.2 KB · Views: 5

Suala la Uchumi wa nchi ni la kisayansi zaidi, pale Wanasiasa Uchwala wasiokuwa na upeo wowote ule wa akili, Wanasiasa wasio na maono yoyote yale wanapokuwa na Mamlaka yote kabisa makubwa kuhusu hatma ya Uchumi wa nchi bila ya kuwashirikisha Wananchi wengine wenye upeo mkubwa katika mambo mbalimbali, Basi matokeo yake huwa ndio kama hayo yaliyoikumba Zimbabwe.

Sayansi daima huwa inakuwa na misingi yake ambayo daima inapaswa kuzingatiwa, hivyo, ukiizingatia misingi hiyo, matokeo chanya lazima utayapata, na usipoizingatia misingi hiyo, matokeo hasi lazima pia utayapata. Kwa hiyo Uamuzi ni wako, na kupanga ni kuchagua.
 
Hata enz za jiwe mambo alipona yanakua magumu akataka kufyatua pesa nyingi kwenye mzuguko wa fedha eti fedha zipatikane kwa wingi mtaani nkaona kazi ipo.
 
Back
Top Bottom