Mtafiti77
JF-Expert Member
- Oct 31, 2011
- 1,843
- 2,272
Mtafiti...
Nimeandika historia ya wazee wangu katika kukabiliana na ukoloni.
Vyanzo vyangu katika mwanzo wa kuunda African Association ni mswada alioandika Kleist Sykes kabla hajafariki.
Mswada huu upo Maktaba ya Chuo Kikuu Chs Dar es Salaam East Africana na uliwasilishwa na Daisy Sykes mjukuu wa Kleist kama seminar paper mwaka wa 1968.
Seminar paper ikawa katika kitabu kilichohaririwa na John Iliffe, "Modern Tanzanians," mwaka wa 1973.
Pamoja na mswada huo nilifunguliwa Sykes Papers zenye historia ya TAA na TANU kuanzia miaka ya 1920 hadi uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961.
Pamoja na hao tena nilifanya mazungumzo marefu familia ya Sykes na wakanieleza yale waliyofanya wakati wa kuunda TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.
Nilipita mikoani ambako nilizungumza na wazalendo waliokuwa hai na nilikusanya nyaraka na picha na kupata maelezo ya historia ya uhuru.
Unajua ipo hivi. Katika kuandika mambo kama haya unapaswa kuwa makini sana. Hapa unagusa hisia za watu. Pamoja ni jambo jema wewe kukiri kuwa unaandika historia ya babu/ndugu zako, hii si leseni ya wewe kuwa mkweli. Nimeona ukijinasibu mara kwa mara kuwa unaandika vya kwenu, hii inasabisha mtu yeyote critical awe makini kuangalia ujenzi wako wa hoja.
Aidha, haimaanishi eti kwakuwa wewe nasaba na hao wanaharakati basi usemacho ni kweli. Mtu asiye na nasaba anaweza kuandika ukweli zaidi kuliko wewe. Itategemea tu kila mmoja ana malengo gani.
Hata wanaokupinga hapa, haimaanishi wao ni wakweli kihivyo. Si ajabu wanatumia udhaifu wako wa kujenga hoja kukushambulia. Binafsi, kujigamba kuwa una undugu na hawa wapiganaji basi usikilizwe ninaona ni udhaifu. Shusha facts, wewe kaa kando.