NEMA 1993 Ilikumbusha TANU 1954

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,263
Picha zilizopo katika makala haya nilipiga Ukumbi wa Arnautoglo 1993 wakati chama cha National Emancipation Movement (NEMA) kinahakiki wanachama wake 1993 ili kupata usajili wa kudumu.

April 1953 katika ukumbi huu palifanyika Uchaguzi wa Mwaka Abdul Sykes na Nyerere waligombea nafasi ya President wa TAA.

Nyerere alikuwa anaomba kura kwa watu mfano wa hawa katika picha ambao yeye hawajui na wao hawamjui.

Nyerere alishinda uchaguzi ule kwa kura chache sana.

Alishindaje mtu mgeni Julius Nyerere dhidi ya mwanamji Abdulwahid Sykes?

Kisa ndani ya historia ya uchaguzi huu kinasisimua sana.
Nimekieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Kuna mengi ya kuzingatia katika historia hii na mafunzo muhimu sana.

Fungua kitabu chochote cha historia hukuti mahali imeelezwa uchaguzi huu au kueleza kuwa Nyerere alipokea uongozi wa TAA 1953 kutoka mikononi kwa Abdul Sykes.

Nyerere mwenyewe katika hotuba maarufu ya Diamond Jubilee Hall alimtaja Abdul na TAA akasema kuwa anadhani Abdul alikuwa Secretary wa TAA.

Maana yake hana hakika na nafasi ya uongozi wa Abdul Sykes katika TAA.
Kidogo inastaajabisha.

Baada ya uchaguzi ule wa March, ilipofika June, makao makuu ya TAA, New Street yalitangaza kamati yake ya utendaji: J. K. Nyerere (Rais), Abdulwahid Sykes, (Makamu wa Rais); J. P. Kasella Bantu (Katibu Mkuu); Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, (Makatibu wa muhtasari); Wajumbe wa Kamati: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo na Patrick Aoko (Tanganyika Standard, 19 th June 1953).

Alipofariki Abdul Sykes magazeti ya TANU The Nationalist na Uhuru hayakuandika chochote kuhusu Abdul Sykes ukitoa kueleza kuwa Julius Nyerere kuhudhuria maziko yake.

Tanganyika Standard kupitia Sunday News 13 October, 1968 wakachapa taazia iliyomweleza Abdul Sykes kama chanzo cha kuundwa kwa chama cha TANU 1954.

1696740813021.jpeg

1696740895582.jpeg
1696740939541.jpeg
1696740984121.jpeg
 
Ka Nyerere bana. Sijui kwa nini kaliamua kuwapotezea wazee wako akina Sykes. Afadhali umewapigania na sasa wanajulikana!

Kongole kwako!
Ndaga...
Napenda kuandikiwa kwa kuzingatia adabu na heshima.

Huu ni mjadala muhimu katika kurekebisha historia si mjadala wala mahali pa kukejeli kwani umewagusa waasisi wa taifa letu.
 
Nyerere was born to lead, alichopanga Mungu huwa,ilishapangwa Yeye kuwa Rais wa nchi hii mengine ni kijipa presha,siku hazirudi nyuma, Nyerere ndio stering hao kina Sykes ni minor characters au stunts towards independence, pata oicha Sykes angekuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika,wasaliti walioungana na mjerumani kumpiga Mkwawa, To hell!
 
Nyerere was born to lead,alichopanga Mungu huwa,ilishapangwa Yeye kuwa Rais wa nchi hii mengine ni kijipa presha,siku hazirudi nyuma,Nyerere ndio stering hao kina Sykes ni minor characters au stunts towards independence,pata oicha Sykes angekuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika,wasaliti walioungana na mjerumani kumpiga Mkwawa,To hell!!!
Mdukuzi,

Mazungumzo ya Julius Nyerere kutiwa katika uongozi wa juu wa TAA yalifanywa nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio, Ukerewe.

Mazungumzo hayo yalikuwa kati ya Mwapachu, Abdul Sykes na Ali Mwinyi Tambwe na wakakubaliana kuwa Nyerere asaidiwe kuchukua nafasi hiyo na mwaka unaokuja 1954 TANU iundwe.

Ali Mwinyi alikuwa katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Historia hii imefutwa.

Nimeweka rejea kwa wanafunzi wa historia wazione.

Hakuna suala la kujipa presha yoyote.
Naiweka sawa historia ya uhuru isipotishwe.

Kuwa Sykes Mbuwane babu yake Abdul Sykes alikuwa mamluki ndani ya jeshi la Wajerumani likiongozwa na Hermann von Wissman lililopigana dhidi ya Abushiri bin Salim na Mtwa Abdallah Mkwawa ni kweli.

Haya ndiyo madhila ya ukoloni.

Sykes hawakuwa "minor."

Kleist Sykes ni katibu muasisi wa African Association 1929 na katibu muasisi wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933.

Naona umeghadhibika na lugha imekuwa ya ukali.

Basi na tukomee hapa.
 
Pole sana mzee,maumivu ya kizidi muone daktari.
Jiwe...
Wewe ndiyo wa kupewa pole.

Mimi hapa mwalimu naisomesha historia ya uhuru natoa elimu bila khiyana wala choyo.

Wewe mtu wa matusi.
Umenitukana sana.

Sasa nani ampe pole nani?
Asomeshae na kuelimisha au mtukanaji?
 
Nyerere kama aliweza kumshinda Abdul aliyekuwa mwandamizi ndani ya TAA bila shaka alikuwa na kitu Cha ziada katika uongozi
 
Nyerere aliwazidi ujanja na maarifa babu zake@mohamed said
Mdukuzi....
Sisi ni waungwana hatujiingizi katika yale yatakayotuharibia ihsani za wazee wetu.

Wenyewe walisubiri kimya hadi umauti ulipowafika.

Miaka mingi ikapita.

Leo historia ya kweli ndiyo hii wewe unaisoma.

Haitokuwa sawa mimi kuichafua kwa maneno yasiyofaa.
 
Nyerere kama aliweza kumshinda Abdul aliyekuwa mwandamizi ndani ya TAA bila shaka alikuwa na kitu Cha ziada katika uongozi
Luta...
Ni kweli Nyerere alikuwa kawazidi wenzake na hili walilitambua.

Ukisoma vipi alichaguliwa kuwa Rais wa TAA utayakuta mengine makubwa na muhimu kushinda hayo.

Ile nafasi ilitakiwa ishikwe na Mkristo ili kuleta umoja wa wananchi wote dhidi ya Waingereza.

Walihofia isiwe harakati za uhuru zimetawaliwa na Waislam hili lingeweza kuingiza fitna katika jamii.

Waingereza wangewashawishi Wakristo kuunda chama chao.

Tanganyika ingeingia katika kudai uhuru ikiwa na vyama viwili vinavyokinzana.

Huu umoja uliopo leo usingekuwapo.

India iliingia katika mtego huu.

Leo wanapewa uhuru kesho Wahindu na Waislam wanapigana.

Umepata kusikia maaskofu walipigania uhuru au kuuza kadi za TANU makanisani au kuona wamepiga picha na Nyerere wakati wa kupigania uhuru?

Hujiulizi kwa nini?

Picha zote Nyerere kazungukwa na Waislam.

Soma kitabu cha Abdul Sykes utajifunza mengi.
 
Mdukuzi....
Sisi ni waungwana hatujiingizi katika yale yatakayotuharibia ihsani za wazee wetu.

Wenyewe walisubiri kimya hadi umauti ulipowafika.

Miaka mingi ikapita.

Leo historia ya kweli ndiyo hii wewe unaisoma.

Haitokuwa sawa mimi kuichafua kwa maneno yasiyofaa.
Nakubali wewe ni muungwana sana ila ukweli ndio huo,nyerere alikuwa mbele ya wakati kulinganisha na hao wazee wako
 
Nakubali wewe ni muungwana sana ila ukweli ndio huo,nyerere alikuwa mbele ya wakati kulinganisha na hao wazee wako
Mdukuzi,
Mbele ya wakati kwa vipi ilhali 1924 Kleist Sykes anzungumza na Dr. Kwegyir Aggrey kuhusu kuasisi umoja wa Waafrika wa Tanganyika?

1929 Kleist anaasisi African Association na 1933 Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na kuanzisha Muslim School ambayo ndiyo shule alisoma baba yangu na akina Abdul Sykes na watoto wengi wa Dar es Salaam wa miaka hiyo.

Kleist akajenga ofisi ya African Association na jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ambalo lipo hadi leo lau kama serikali imelitaifisha.

Mbele vipi wakati 1940s Erica Fiah anaanzisha gazeti ''Kwetu,'' kwa ajili ya Waafrika wa Tanganyika na miaka baadae Ramadhani Mashado Plantan anafuata nyayo za Fian na yeye anaanzisha gazeti ''Zuhura?''

Ushasoma tahariri za Fiah alizokuwa akiandika nyakati hizo?

Mbele ya wakati vipi wakati Hamza Mwapachu katika pengine 1930s anamsoma Karl Max na katika makataba yale alikuwa na tolea la 1924 la Das Kaptal?

Mbele ya wakati vipi wakati 1948 Abdul Sykes anaongoza Dar es Salaam Dockworkers Union kama General Secretary?

1950 Abdul Sykes anakutana na Jomo Kenyatta na viongozi wa KAU akina Peter Mbiu Koinange, Bildad Kaggia, Kun'gu Karumba, Achieng Aneko kwa kuwataja wa chache katika mkutano wa siri Nairobi.

Agenda ya mkutano kuunganisha nguvu kupambana na Waingereza hadi wametoa uhuru.

Unaijua historia ya Madaktari Watano wakijiita Action Group: Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Luciano Tsere, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Michael Lugazia na Wilbard Mwajisi na mchango wao katika TAA hata Nyerere hajafika Dar es Salaam?

Dr. Vedasto Kyaruzi na Abdul Sykes ndiyo walioingia katika uongozi wa TAA 1950 kama vijana President na Secretary kuondoa uongozi wa wazee Mwalimu Thomas Plantan na Clement Mohamed Mtamila.

Wawili hawa walileta mabadiliko makubwa katika TAA kupitia TAA Political Subcommittee.

Hii ndiyo historia ambayo ilifutwa nami nikairejesha katika kitabu cha Abdul Sykes.

Tafadhali sana soma kitabu cha Abdul Sykes kuna historia kubwa ndani yake na utapata maarifa mengi sana.

1696778649116.png

Kulia nyuma waliosimama Dr. Joseph Mutahangarwa, kushoto mwisho Dr. Luciano Tsere na mbele ni Dr. Vedasto​
 
Kw
Mdukuzi,
Mbele ya wakati kwa vipi ilhali 1924 Kleist Sykes anzungumza na Dr. Kwegyir Aggrey kuhusu kuasisi umoja wa Waafrika wa Tanganyika?

1929 Kleist anaasisi African Association na 1933 Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na kuanzisha Muslim School ambayo ndiyo shule alisoma baba yangu na akina Abdul Sykes na watoto wengi wa Dar es Salaam wa miaka hiyo.

Kleist akajenga ofisi ya African Association na jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ambalo lipo hadi leo lau kama serikali imelitaifisha.

Mbele vipi wakati 1940s Erica Fiah anaanzisha gazeti ''Kwetu,'' kwa ajili ya Waafrika wa Tanganyika na miaka baadae Ramadhani Mashado Plantan anafuata nyayo za Fian na yeye anaanzisha gazeti ''Zuhura?''

Ushasoma tahariri za Fiah alizokuwa akiandika nyakati hizo?

Mbele ya wakati vipi wakati Hamza Mwapachu katika pengine 1930s anamsoma Karl Max na katika makataba yale alikuwa na tolea la 1924 la Das Kaptal?

Mbele ya wakati vipi wakati 1948 Abdul Sykes anaongoza Dar es Salaam Dockworkers Union kama General Secretary?

1950 Abdul Sykes anakutana na Jomo Kenyatta na viongozi wa KAU akina Peter Mbiu Koinange, Bildad Kaggia, Kun'gu Karumba, Achieng Aneko kwa kuwataja wa chache katika mkutano wa siri Nairobi.

Agenda ya mkutano kuunganisha nguvu kupambana na Waingereza hadi wametoa uhuru.

Unaijua historia ya Madaktari Watano wakijiita Action Group: Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Luciano Tsere, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Michael Lugazia na Wilbard Mwajisi na mchango wao katika TAA hata Nyerere hajafika Dar es Salaam?

Tafadhali saba soma kitabu cha Abdul Sykes kuna historia kubwa ndani yake na utapata maarifa mengi sana.
Kwenye riadha anayefika wa kwanza ndio mshindi,hao wazee spidi yao haikuwa ile inayotakikana mpaka nyerere alipoibuka
 
Kw

Kwenye riadha anayefika wa kwanza ndio mshindi,hao wazee spidi yao haikuwa ile inayotakikana mpaka nyerere alipoibuka
Mdukuzi,
Si kweli.

Nimekuwekea hapo historia kwa mukhtasari na kukueleza kuwa historia hii imefutwa.

Wewe unakuja na spidi.

Nyerere hajaeleza spidi yeye alipozungumza Diamond Jubilee kazungumza historia yake ambayo baadhi ya mambo kasahau pengine kwa muda kuwa mrefu umepita.

Napenda kukueleza kuwa katika harakati zile kuelekea kuundwa kwa TANU wazee siyo waliokuwa mstari wa mbele.

Lakini Mwalimu yeye anaeleza habari za wazee bila ya kutaja majina ya hao wazee.

Baraza la Wazee siku zote lilikuwapo TAA watatu walikuwa katika TAA Political Subcommittee: Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo na John Rupia.

Waliobakia wote walikuwa vijana: Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu na Steven Mhando na ukipenda unaweza ukamtia Earle Seaton aliyekuwa mwanasheria wa TAA akishauri katika masuala ya Mandate Territories.

Historia ya uhuru imeandikwa na hivi karibuni kimetoka kitabu cha maisha ya Mwalimu Julius Nyerere haya ninayokueleza mimi muhimu katika maisha ya Nyerere hayamo.

Iko siku nitakuelezeni safari ya Mwalimu UNO na mkakati aliopanga Abdul Sykes, Nyerere asidungwe chanjo (vaccination) kwa kuhofu asije akadhuriwa na Waingereza.

Vaccination Certificate ilipatikana lakini Nyerere hakuchoma sindano yoyote si ya Yellow Fever nk.

Jitulize usome historia ya harakati za uhuru kwa utulivu.
 
Back
Top Bottom