Nini kilikuwa kinakusukuma uende shule?

Asante mkuu.
je unakumbuka mkiwa mmejipaga asubuhi,unaweka kioo chini alafu unakisukuma na mguu mpaka katikati
ya miguu yake,hapo unaanza kupata video ya bure

au mnasogeza viti, msichana akitaka kukaa ananguka walio mbele wanapata video ya bure
 
Mi nilikuwa naenda shule kwa fosi ya dingi, nakumbuka siku moja alitoka mapema sana akasema anaenda kuhudhuria kikao nami niikaamua kuitumia chansi ile kutokwenda shule kwa imani kuwa mpaka muda anarudi muda wa kutoka shule utakuwa umefika, lakini ikawa tofauti. Unaweza ukabashiri kilichotokea.
 
afu unaanza kutangaza
kavaa ya njano, au nyekundu

dah, na kipindi hicho ilikuwa ni mwendo wa rangi za bendera ya taifa plus nyekundu na nyeusi tu

Asante mkuu.
je unakumbuka mkiwa mmejipaga asubuhi,unaweka kioo chini alafu unakisukuma na mguu mpaka katikati
ya miguu yake,hapo unaanza kupata video ya bure
 
Mdingi alivyokuwa mnoko
anakupeleka shule hata kama ni saa saba
anaomba paredi ya emergence
anakutandika mbele ya shule

iwe fundisho kwako na vizazi vyako

 
bahati mbaya alikuwa rafiki wa walimu karibu wote, hivyo kudanganya ilikuwa risk kubwa zaidi,
hayo walifanya kaka zangu, lakini adhabu walizokuwa wanapata pia zilikuwa hamasa kwangu kutokudanganya.
Dah kazi ulikuwa nayo, mi bwana nilikuwa namuingiza maza chaka sana na hata wakati mwingine anajua kabisa huu uongo but inabidi aukubali coz nakuwa macho makavu
 
Dah huyo jamaa inabidi umtafute umuone alivyokuwa siku hizi. Hata mi nisingerudi tena
 
Mfueni wa hatari, halafu ulikuwa ukibaki kwenye mazingira hayo unakuwa na hofu kutwa nzima na karibu siku tatu nzima unahisi atagundua hukwenda shule
 
huyu labda
atakuwa alikuwa na matatizo
hasa ya kunyanyaswa
na wanawake kama mama wa kambo, shangazi ikampelekea kuwachukia wanawake

 

Kuepuka KERO za Mama wa Kambo!
 
Mimi mtaani kwetu watoto wengi walikuwa hawaendi shule, lakini mm nilienda kwa kuogopa mikwara ya baba. Siku aliyonikuta ninacheza sikwenda shule...duh!
Alinikamata sikio na kuniburuza mpaka shule, njia nzima kofi moja kila baada ya dakika 5 +/-. Kufika shule alinitaka nimwoneshe darasa langu. Tulipoingia kulikuwa na kiti kimoja kitupu, changu. Akaenda kukaa pale na kusema:

"Wewe rejea nyumbani ukacheze mimi nitabaki hapa kusoma kwa niaba yako". Nikiwa ninalia na kuona siondoki, alichukua bakora ya mwalimu na kuanza kunicharaza nazo. Sio kwa maumivu ya bakora tu, ile ilikuwa aibu nisiyoweza kuisahau. Kuanzia hapo sikuwacha tena kwenda shule hata kama nilikuwa mgonjwa.
 
Iko,hii nyingine iliyutokea kwenye kipindi cha kiswahili.Mwalimu alikuwa akija darasani
anakusimamisha na anakuambia useme methali kisha wengine mnajibu.
Kuna jamaa alikuwa mtundu sana alipo ambiwa atoe methali akasema"Kapigwa chini kavimba juu"
Sisi tukakaa kimya kuogopa kujibu,jamaa akaambiwa na mwalimu ajibu methali yake,alipo kataa kujibu
alpigwa fito ile mbaya.
 
Nice lesson
 
Dah umenikumbusha siku moja nasikiliza kipindi cha watoto Radio One, wakati wa methali dogo mmoja akaibuka akauliza hilo "Kapigwa chini kavimba juu"
 
Nimeipenda hii lol!
 
mi viboko ndo vilikuwa vinanipeleka na kunifanya niwahi kuhesabu namba. nisipo enda shule napigwa viboko halafu napelekwa nimefungwa mikono na babu. nikienda nikachelewa nachapwa viboko coz sijahesabu namba. nikaona bora tu hata kama kuna baridi niende hivyo hivyo nalia bila kupigwa coz nlikua naona ni adhabu. nlikuwa naenda roho inauma. Mia
 
mm sikumbuki kugoma kuenda shule coz nlikua asubuhi naamshwa kwa upendo, maji nshaekewa bafuni, nguo nshapigiwa pasi ni kuoga kuvaa na kwenda shule. Kwetu sisi ilikua kucheza ndani tu so hata sikuwa na ham ya kusema nibaki ili eti nichee na mimi ndo nlikua mdogo so sina hata wa kucheza nae. Bora niende shule napata marafiki wa mastori na kucheza nao. Halafu pia nlikua napenda kusoma vitabu so nkiweko home kutwa nasoma vitabu vya stori za wtt au mashairi au naangalia picha vitabu vya vyakula. Mpk leo hobby zangu ni kupika na kusoma novels
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…