Nini kilikusaidia kupata kazi?

Mkuu, wewe ni introvert au extrovert??

Asee mm ni introvert kwa 80%+ napata shda sana kufahamiana na watu wapya na kutengeneza connection mpya. Yaan kila ikija ajira/mchongo wa pesa unaohitaji mtu fulan aku recommend najikuta nakosa huyo mtu bcoz skutengeneza connection mapema.
Mkuu pole sana

Introvert...! Da'Vinci mshauri mwenzako afanyaje...!

Lo...huu upande ingawa na-enjoy ila kwaa namna fulani kutengeneza connection kuna ugumu. Ila kwa kusoma vitabu najikuta najiamini sana...!
 
Omba Mungu sana, kuajiriwa hakuna ujanja, ni Mwenyezimungu akiamua tu unapata, kuna jamaa yangu mmoja hivi alijitolea Kinyerezi 2, miezi 10 hakupata ajira, kipindi anajitolea akaitwa tena kujitolea TPA(seap program) mwaka mzima uliisha na ajira zikitoka yupo pale lkn alikuwa hapati ajira, ingawa alikuwa analipwa 1M kwa nwezi. juzikati ajira za TBA wakaitwa watu 280 huku wakiwa wanatafuta mtu mmoja akachukuliwa yeye (Mechanical Engineer 2).

Kuna mdogo wangu kamaliza mwaka huu AUTOMOBILE ENGINEERING, kapata kazi TOTAL bila connection walienda kuomba kurecruit watu wa automobile wanamchukua kisa ana gpa nzuri, kuna jamaa humu jamii forum, nilimkonect tu mahala wanatafuta maintenance engineer haikuchukua hata week 2 akaitwa kazini, na niliwapa watu wengi email watume maombi lkn ye aliitwa faster. .

Ukisikia mtu kapata kazi wala sio ujanja wake, bali nimuda tu umefika.
Hii safi
 
NAOMBEN MSAADA JAMAN KATK AJIRA PORTAL KUNA NAFAS ZIMETOKA ILA NIKIAPLY NIKIINGIA AJIRA PORTAL HYO NAFAS SIIONI KBSA
 
Volunteer Ministry of Water (& Irrigation).

Then Utumishi wakatoa ajira (before 2015).

Nikapita Written, Oral ikanibeba sana walipouliza Tell us about yourself...
Hongeraaa mad max,m Ilo swali niliulizwa ila ckuchaguliwa , Kwa niaba ya Wana jf tusaidie namna ya kujibu.
 
Wakuu mwenye conection ya kazi naomba jamani elimu yangu form four nlishafanya kazi kama cashier, receptionist kwenye mahotel, naombeni msaada wenu hali ni tete jamani
 
Sina chama.

Ila nataka kujua kwanini wasomi tunaotegemea walete mabadiliko kwenye kada za science,technology na mambo ya tiba au kutengeneza ajira wao ndio wanaomba kazi.

Kwanini wanaomba kazi?

Hapo tunarudi kwenye nini lengo la elimu.
Tatzo msingi, tatizo bills za kila siku....wengi tu mawazo makubwa ya kutengezea project za mamilion lakini kama unadaiwa kodi ya nyumba, unatakiwa ule nk....unajikuta unatafuta angalau kazi kwa ajili ya kusettle bills na mitaji ya kuanzia kuwekeza kwwnye hizo project.
 
Wewe IT kuajiriwa halmashauri ni kula mema ya nchi?

1. Kamati za madiwani zikushukie
2. CMT ikukomalie
3. Defaulters wa mapato wakutoe jasho kwa DED
4. Payer ID zaidi ya moja zikuzalishie hoja.
5. MUSE ikuchanganye.

Hivi kabisa halmashauri Kuna bata?

#YNWA
Halmashauri ni hakuna hela,njaa Tu sio kwamba Nina dharau🤣
 
Naomba namimi nicomment after kumaliza chuo nilienda TRA kuomba nafasi ya kujitolea nikapenya moja kwa moja hadi kwa HR na bahasha zangu pale posta Stesheni walinicheka na kunidharau sana hatimae nikafukuzwa mule ndani hata barua zangu hazikupokelewa.

Ila kabla ya huu mwaka kuisha ntarudi kutoa mrejesho naamini ntakua tayari mwajiriwa wa TRA.

Mungu ni wetu sote .

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Tumeliwa kichwa kwenye mkeka wa sensa, mapambano yanaendelea.

Mwenye kuweza kunipatia kazi ama connetion ya kazi yoyote halali katika maendeo ya dar es saalam au dodoma.

Elimu: Bachelor's degree in procurement and logistics management.

Ujuzi mwingine
Computer skills (Ms office)
Video editing (Adobe premier & adobe after effects)
3d animation (blender)
Music production (ujuzi siyo mkubwa katika eneo hili)

Natanguliza shukrani.
 
Msaada jamani hali mbaya mtaani, mwenye connection ya kazi nina bachelor ya environment planning na diploma ya rural development planning, nipo morogoro ila kokote niko tayar kwenda
 
mimi pia nipo MOROGORO asee, nimemaliza 2020, Banking and Finance pale IFM + GPA nzuri but mpaka Sasa naona chenga tu. Mtaani kunabore for sure.
 
Tumeliwa kichwa kwenye mkeka wa sensa, mapambano yanaendelea.

Mwenye kuweza kunipatia kazi ama connetion ya kazi yoyote halali katika maendeo ya dar es saalam au dodoma.

Elimu: Bachelor's degree in procurement and logistics management.

Ujuzi mwingine
Computer skills (Ms office)
Video editing (Adobe premier & adobe after effects)
3d animation (blender)
Music production (ujuzi siyo mkubwa katika eneo hili)

Natanguliza shukrani.
betting unafanya?
 
Moja kwa moja kwenye mada...

Vijana wengi wanamaliza vyuo kila mwaka ilihali wengine bado tuko mtaani hawajui hatima ya maisha .

Kwa interview baadhi yao wanaitwa lakini nyingi ni kama danganya toto tu walio na iyo kazi wapo tayari wengine wanapoteza tu muda..n

Sasa wandugu wewe uliwezaje kupata kazi tushirikiane mbinu tulizotumia kwa manufaa ya wengine
Eleweni Afrika wasomi ni wengi kuliko wingi wa ajira, siyo msome mkidhani kuja kutafuta kazi, someni kama kupiga msasa akili zenu maana mlikubali elimu iliyojaa misingi ya kigeni mnadhani na ajira zitakaa kigeni? Wao wanafundisha watoto wao kuvumbua mambo, ninyi mnafundishwa matumizi ya walivyo vumbua wao, hamtumii akili??
 
Back
Top Bottom