Nini kilikusaidia kupata kazi?

Kwangu mie ilikuwa ni kama bahati tu kupata kazi (kuajiriwa). Sijawahi kufanyiwa serious interveiw na wala sikuwa na connection yeyote hapo awali. Nilienda hospitali kwa ajili ya matibabu (ilikuwa 1994), na hapo nikakutana na Professor mmoja akaniuliza ninasomea nini (nilikuwa mwaka wa pili chuo then). Nikamwelezea ninachosoma na akasema ana research projects zake kama niko interested kumsaidia kazi. Nilianza kazi huku bado nikiwa chuo. Since then bahati za kupata masomo ya ziada na kazi zaidi zilifuata. Namshukuru Allah kwa kunifanyia wepesi kwenye haya. Najua wengi wamehangaika kupata kazi na kuna ambao bado wanahangaika kupata kazi. Mungu awajalie waweze kufanikiwa katika ndoto zao.
 
Amina....Mungu ni mwema
 
Lesson nzuri sana hii brethren.
 

amazing grace
 
Nilimtanguliza Mungu kumwamini na kumtegemea kwa asilimia zote kuanzia mwanzo wa mchakato mpaka mwisho na maandalizi yangu yalikuwa ni mazuri kwa maana ya kusoma na kufanya mazoezi ya vitendo(Practical) ,saasa nimefanikiwa kupata kazi nzuri kuliko nilivyokuwa nafikiria, ni Mungu tu wa kumtanguliza na kumwamini na kumtegemea kwa asilimia zote,ukweli kwa kwa akili yangu mwenyewe nisingeweza sababu ushindani ni mkubwa sana. MTANGULIZE MUNGU MBELE, KATIKA MAMBO YAKO YOTE UTASHINDA....BARIKIWA
 
Yaani scenario yako inanifanya nizidi kuipenda jamii forum , maana hii ni nyumba ambayo watu wanaishi humu hawajuani si sura tu ila hata majina lakini utu ni tunu yao .
 
Hongera
 
Uzi mzuri hasa unatuhusu sisi tuliopo vyuoni, ninasoma diploma in procurement and logistics management semester ya mwisho ( mwezi wa sita off). Kiukweli sielewi wapi pa kuanzia, Ila kupitia comment za wadau mbalimbali nimepata mwanga kidogo. Pia Kama kuna yoyote mwenye ramani anisaidie nipo tayari.
 
Karibu kitaa kiongozi
 
Well done, umetisha sana
 
Kuna wakati unaweza kudhani kuna vigezo mahsusi vya mtu kupata kazi, ila unajiuliza mbona wengi wana hivyo vigezo lakini hawana kazi? Unakubaliana na uwepo wa "bahati" kwa kila mtu, lakini ikiwa utaamini hivyo basi jua kuwa bahati haibahatishwi, unahitajika uitafute.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…