Nini kilichangia Wachungaji kupigwa 9-2 na Mapadri?

Nini kilichangia Wachungaji kupigwa 9-2 na Mapadri?

Nehemia Kilave

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
1,530
Reaction score
3,422
Katika maazimisho ya miaka 50 ya Askofu Isack Amani wa Arusha na kuimarisha umoja baina ya watumishi wa Mungu , kulichezwa mechi muunganiko wa wachungaji vs mapadri wa Arusha .

Kiukweli wachungaji walizidiwa sana ,wachambizi wa JF nini kilipelekea hiki kipigo cha 9-2 ?

View: https://youtu.be/HqJZ_SlZ1JE?si=ke4H6FmNEvY7N3OH
 
Katika maazimisho ya miaka 50 ya Askofu Isack Amani wa Arusha na kuimarisha umoja baina ya watumishi wa Mungu , kulichezwa mechi muunganiko wa wachungaji vs mapadri wa Arusha .

Kiukweli wachungaji walizidiwa sana ,wachambizi wa JF nini kilipelekea hiki kipigo ?
View attachment 3399209

View: https://youtu.be/HqJZ_SlZ1JE?si=ke4H6FmNEvY7N3OH

Ndicho kilichobaki kwa hao mapadre na wachungaji baada ya kazi za kanisani kuwashinda wakaona wakimbilie matamko ya siasa .Baada ya kuona huko nako kumewashinda wamegeukia kwenye kucheza soka
Baada ya Soka nini kinafuata?
 
Wengi wanaojiita wachungaji ukifuatilia historia zao zina mambo mengi. Huyu alikuwa konda, mwingine dalali, huyu kibaka yaani Kiufupi historia zao na wanachokifanya kwa sasa ni vitu viwili tofauti, na ndio maana hawakosi kuwahubiria waumini wao shuhuda kila siku. Tunaweza kusema katika maisha yao ya ujana wengi hawajawahi kupata muda wa kushiriki michezo.

Tofauti na mapadre wengi maisha yao yamenyooka hawajaibukia kwenye upadre tu. Shule wanazosoma zina viwanja vya michezo mbalimbali, hivyo wanapata muda wa kutosha wa kufanya mazoezi na kushiriki michezo ya aina mbalimbali.

Wachungaji kufungwa hizo goli 9 bado ni chache sana. Na hata hizo mbili walizopata bila shaka itakuwa wafungaji ni kutoka KKKT au mapadri walijiunga.

🤔
 
Back
Top Bottom