#COVID19 Nini kifanyike kuondoa taharuki kwa wanafunzi wanaokimbia ovyo waonapo wageni au magari shuleni?

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
667
1,795
Sasa ni taharuki kwa wanafunzi wa shule za msingi wakiwa shule waonapo wageni au magari yakiingia shuleni basi huanza taharuki na kukimbia ovyo.

Taharuki hiyo imesababishwa na wazazi wanaowambia watoto wao kuwa serikali inataka kuwachoma chanjo ya Corona kitu ambacho si sahihi.

Wazazi hao wamewambia kuwa wakiona viashiria vya chanjo wakimbie shule hali ambayo imesababisha watoto kuzua taharuki na kukimbia waonapo wageni au gari linaingia shuleni.

Kufuatia hali hiyo ambayo wanafunzi wamepoteza utulivu shuleni hasa kipindi hiki tunaitaka serikali itoe tamko kuhusu hali hiyo au nini kifanyike?

Pia, soma:
- #COVID19 - Geita: Wanafunzi wakimbia hovyo wakiogopa chanjo, Kaimu Mkurugenzi ataka waelimishwe chanjo ni hiari
 
Hyo ipo tangu zamani huko vijijini ikija gari na wageni watoto wanatimka mbio
 
Kuna dhana mbili hapa;
1. Wananchi wa vijijini waliaminishwa chanjo inaua na kwa kwakuwa aliyesema n rais wao, wakamwamini na kuiishi imani ile.
Hii inawatesa hadi sasa
2. Ni propaganda zza sasa kuwa chanjo itafanya watu wageuke mazombi. Watoto wanajua wakichanjwa watakuwa zombie wa gwajiboy

Cha kufanya;
Wazazi ndio wenye kuaminiwa zaidi na watoto wao, kisha walimu. Hivyo hawa ndio wanapaswa kuwafuta huo ujinga watoto wao

Changamoto ya hili;
Wazazi haohao ndio wasioamini chanjo, waliaminishwa unalenga kufunga vizazi vyao na kuwaua. Hivyo wanapata ugumu kubadilisha fikra zao

Mwendazake acha aendezake tu, ametuletea taifa la wajinga
 
Nani anakumbuka taharuki za nyonya damu shuleni,wanafunzi wanakurupuka darasani wanatimua mbio,kisa eti wameona gari ya nyonya damu,gari za wagonjwa ndo zikatafsiriwa ni gari za nyonya damu.

Suluhisho ni tours,wanafunzi wawe wanatoka wanatembea kwenda kujifunza,hata mzazi kama unakijinafasi kidogo wakati wa likizo unamtoa out mtoto maeneo tofauti kujifunza,ikiwezekana hata nje ya mkoa au nje ya nchi,kama ukiwa na uwezo,kama huna basi.
 
Kuna dhana mbili hapa;
1. Wananchi wa vijijini waliaminishwa chanjo inaua na kwa kwakuwa aliyesema n rais wao, wakamwamini na kuiishi imani ile.
Hii inawatesa hadi sasa
2. Ni propaganda zza sasa kuwa chanjo itafanya watu wageuke mazombi. Watoto wanajua wakichanjwa watakuwa zombie wa gwajiboy

Cha kufanya;
Wazazi ndio wenye kuaminiwa zaidi na watoto wao, kisha walimu. Hivyo hawa ndio wanapaswa kuwafuta huo ujinga watoto wao

Changamoto ya hili;
Wazazi haohao ndio wasioamini chanjo, waliaminishwa unalenga kufunga vizazi vyao na kuwaua. Hivyo wanapata ugumu kubadilisha fikra zao

Mwendazake acha aendezake tu, ametuletea taifa la wajinga
una akili mgando ,uchanjwe usichanjwe utakufa tu,endelea kumuota maghufuli alipokutumia na vyeti feki hautamsahau mpaka unaenda kaburini,
 
una akili mgando ,uchanjwe usichanjwe utakufa tu,endelea kumuota maghufuli alipokutumia na vyeti feki hautamsahau mpaka unaenda kaburini,
Vip baba yako aliyeambiwa apewe 25% ya kiinua mgongo kwa kigezo kuwa akipewa nyingi atakesha baa na vimada!!! Naye mwisho wa kumsahau meco utakuwa lini?
 
Kuna dhana mbili hapa;
1. Wananchi wa vijijini waliaminishwa chanjo inaua na kwa kwakuwa aliyesema n rais wao, wakamwamini na kuiishi imani ile.
Hii inawatesa hadi sasa
2. Ni propaganda zza sasa kuwa chanjo itafanya watu wageuke mazombi. Watoto wanajua wakichanjwa watakuwa zombie wa gwajiboy

Cha kufanya;
Wazazi ndio wenye kuaminiwa zaidi na watoto wao, kisha walimu. Hivyo hawa ndio wanapaswa kuwafuta huo ujinga watoto wao

Changamoto ya hili;
Wazazi haohao ndio wasioamini chanjo, waliaminishwa unalenga kufunga vizazi vyao na kuwaua. Hivyo wanapata ugumu kubadilisha fikra zao

Mwendazake acha aendezake tu, ametuletea taifa la wajinga
Mkuu ina maana mwenda zake aliwalisha wananchi sumu?
 
Mkuu ina maana mwenda zake aliwalisha wananchi sumu?
Haswaa! Tena sumu ambayo kuitoa inahitaji nguvu kubwa zaidi ya ile ya awali.
Watu wa kiwango duni cha maisha ndio waliokuwa wanampenda magu, vijijini na mjini pia. Unaweza tambua hilo hata sasa.
Sasa kwa sumu zile, ni ngumu mno kuwabadilishwa watu overnight

Hata hawa wanaopinga chanjo leo, wengi wao wanatokana na msimamo wa jiwe
 
Nimesikia,Watoto chini ya miaka 18 hawachanjwi,kama ni hivyo,elimu itolewe kwa wananchi.
 
Nashauri wageni watangulize masufuria ya pilau nyama kabla ya kufika eneo la tukio
 
Back
Top Bottom