Vyombo vya dola ndo vilikua vinawalazimisha wananchi waipende CCM? Utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ndo umeifanya CCM iimarike. Mathalani, ujenzi reli ya SGR, Flyovers, Vituo vya Afya na Zahanati, Elimumsingi bila Ada, kupeleka umeme kila kijiji, kudhibiti vitendo vya rushwa na ufisadi n.k. haya yote ndo yamerudisha imani ya wananchi kwa CCM.
Dalili ya chama cha siasa kinachojifia ni pamoja na kukimbiwa na idadi kubwa ya viongozi na wanachama wake, kupoteza imani kwa wananchi na kukosa ajenda na itikadi inayoisimamia. Kuna Vyama tayari vina sifa hizi, sasa nashangaa mnavyosema CCM inakufa sijui mnatumia vigezo vipi? Au mnafanya utani?