Nini kifanyike ili kuiokoa CHADEMA?

Kinjeketile

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
985
1,656
Salaam Wakuu

Kuna maneno wengi yanaongelewa kwamba ACT ilianzishwa ili kuua upinzani ,na kwamba Membe ametumwa na CCM ili kugawanya kira za wapinzani kupitia ACT.

Inawekana kabisa tuhuma hizi zikawa na ukweli ndani yakr,lskini tunkumbuke ya kwamba CCM inatafuta mtu wa kumfia na kuna uwezekano mkubwa ikamfia Magufuli, Kikwete ilinusurika kidogo tu.

ACT ina balance power bara na visiwani yaani inajengeka kwa muonekano wa kitaifa zaidi ni hybrid ya CUF,CHADEMA na CCM. Sass kama CCM muliitengeza ACT ili kuidhofisha CHADEMA basi inaweza kuja kuimeza CCM baada ya hapo ACT na CHADEMA ndiyo watakuwa Democratic and Republican wa Tanzania

CHADEMA chezeni hii game kwa akili,asimamishwe Membe kupitia ACT kisha achianeni ubunge na udiwani. Ili joka la Kishetani(CCM) tunaliua kidogo kidogo kwa kutumia akili nyingi. Vinginevyo hicho kinachodhsniwa kitatokea kweli,kura zitagawanywa na joka la kijani litaendelea kuwa

Huu ni mwaka kitia pilipili kwenye kidonda cha Joka la Kijani cha 2015. CCM haiwezi kutawala milele idondoke,na itamfia Magufuli maana ana kibri na hashauriki anajiona ana akili nyingi kuliko CCM wote
 
Umeshaambiwa msajili yuko mbioni kutoa adhabu kali kwa ACT..hatujui ataibuka na lipi.

Tatizo siku hizi ubabe na umwamba unabebwa kwenye mfuko wa rambo, hawajali wala kuona aibu. Usishangae likatoka tamko la kustaajabisha.

CDM kwa kilichowapata mwaka jana, maamuzi ya safari hii yanahitaji umakini wa hali ya juu sana. Bora wakose urais lakini walinde heshima ndogo ya chama iliyosalia, wasipoangali wanaweza kupoteza vyote.
 
Hivi mnavyosema CCM inatafuta wa kumfia, unakua upo serious au unafanya utani au akili zinakua zimeruka. Yaani vyama vinavyokufa hamvioni?

Hivi kuna kipindi ambacho CCM imeimarika kuliko sasa? Hivi kuna kipindi ambacho wananchi wamekua na imani na hiki chama kuliko sasa? Hivi hamuoni hatua za maendeleo zilizopigwa mpaka kufikia uchumi wa kati katika awamu hii? Hivi hamuoni lundo la wanachama na viongozi wanaotoka upinzani kuhami CCM?

Hivi hamuoni muamko wa watu wa kaliba mbalimbali wanojitokeza kugombea kupitia CCM? Mpaka sasa CDM imefanikiwa kuweka wagombea kwa 5% katika majimbo yote, na wengi wao wamegombea wenyewe hawakua na upinzani. Hakuna waliojitokeza kugombea huko. Mgombea urais wenyewe mwenye ushawishi wa kushindana na JPM hajulikani. Halafu unadiriki kusema CCM inataka kufa.

Seriously?
 
CHADEMA imsimamishe Lisu. ACT kama hawataki kumsapoti Lisu CHADEMA iachane nao. CHADEMA ifocuss kujijenga kwa sasa. Isimamishe wagombea kwa ngazi zote wazawa wa chama, iachane na shortcuts za kusimamisha watu kutoka ccm kisa umaarufu wao. CHADEMA ijiruhusu kukua kwa kutumia wanachama wake wazelendo. Iwe na malengo ya muda mrefu na sio kufocuss kwenye uchaguzi wa mwaka huu tu. Iwe na mikakati ya hata miaka 10 mbele. Nina imani CHADEMA ikiwa na msimamo itakuja kuchukua nchi.
 
ACT waungane na CDM mgombea awe lisu na mgombea mwenza awe Membe,waachiane majimbo pale chama kinapokubalika, Zanzibar na kusini waachiwe ACT bara yote waachiwe CDM.
 
CDM Safari hii wapeni wanawake nafasi ikibidi zote Hawa ni jeshi tosha ni wahanga wa mifumo dhalimu wanajua ugumu wa maisha, wanaume watauza utu wao tumeyaona haya.Wanawake ndo ukombozi wa Taifa.Watakaepusha nchi kurudi kwenye ukomunist huku ufukara ukitamalaki
 
ACT waungane na CDM mgombea awe lisu na mgombea mwenza awe Membe,waachiane majimbo pale chama kinapokubalika, Zanzibar na kusini waachiwe ACT bara yote waachiwe CDM.
Wazo zuri sana hili ila sidhani kama zito atakubali. Zito kapiga hesabu kali sana. Zito hana shida ya ACT kushinda urais maana anajua ACT haina uwezo wa kushinda. Lengo la zito ni kupata wabunge ili ruzuku ya kuendeshea chama ipatikane. Kwa kifupi zito sio mpinzani ni mvuruga upinzani.
 
Ccm sio imara bali ina uimara fake ulio chini ya madaraka ya urais. Kwakuwa ccm imepata mwenyekiti kwa kupitia kofia yake ya urais, anaweza kufanya lolote na asikutane na kikwazo chochote cha ndani. Rais huyu ana chuki na nongwa ya wazi dhidi ya upinzani hasa cdm, hivyo anatumia madaraka yake vibaya kuagiza taasisi zote za kimamlaka kuua upinzani hasa cdm.

Rais huyu anaingilia box la kura, na kuagiza bila hofu kuwa matokeo yawe yale anayoyataka. Hakuna mwananchi mwenye uwezo wa kuhoji, kwani anashurutisha ionekane demokrasia ndio kikwazo cha maendeleo. Wale wote wasiomsujudia wanatekwa, wanabambikiwa kesi, vyombo vya habari vinavyomkosoa vinavyofungiwa. Huo ndio uimara wa ccm. Mtu mjinga tu ndio anaweza kusema ccm ni imara, eti kisa kuna kundi kubwa linajitokeza kugombea uwakilishi. Hilo kundi linajitokeza kama sehemu ya hizi siasa za kishenzi zinazoendelea humu nchini.
 
Mambo yatakuwa mazuri CDM sio chama cha kufa kirahisi, ni chama chenye wapenzi wengi kuliko CCM na kimeenea sana mashinani. Kwa vyovyote kama ccm hawatamzuia Lissu, basi tegemea mtananga wa kufurahisha na kama ACT na vyama vingine vikiungana basi ccm hawana lao.
Salaam Wakuu!!
Kuna maneno wengi yanaongelewa kwamba ACT ilianzishwa ili kuua upinzani ,na kwamba Membe ametumwa na CCM ili kugawanya kira za wapinzani kupitia ACT.

Inawekana kabisa tuhuma hizi zikawa na ukweli ndani yakr,lskini tunkumbuke ya kwamba CCM inatafuta mtu wa kumfia na kuna uwezekano mkubwa ikamfia Magufuli, Kikwete ilinusurika kidogo tu.

ACT ina balance power bara na visiwani yaani inajengeka kwa muonekano wa kitaifa zaidi ni hybrid ya CUF,CHADEMA na CCM. Sass kama CCM muliitengeza ACT ili kuidhofisha CHADEMA basi inaweza kuja kuimeza CCM baada ya hapo ACT na CHADEMA ndiyo watakuwa Democratic and Republican wa Tanzania.

CHADEMA chezeni hii game kwa akili,asimamishwe Membe kupitia ACT kisha achianeni ubunge na udiwani. Ili joka la Kishetani(CCM) tunaliua kidogo kidogo kwa kutumia akili nyingi. Vinginevyo hicho kinachodhsniwa kitatokea kweli,kura zitagawanywa na joka la kijani litaendelea kuwa.

Huu ni mwaka kitia pilipili kwenye kidonda cha Joka la Kijani cha 2015. CCM haiwezi kutawala milele idondoke,na itamfia Magufuli maana ana kibri na hashauriki anajiona ana akili nyingi kuliko CCM wote.
Umeshaambiwa msajili yuko mbioni kutoa adhabu kali kwa ACT..hatujui ataibuka na lipi.

Tatizo siku hizi ubabe na umwamba unabebwa kwenye mfuko wa rambo, hawajali wala kuona aibu. Usishangae likatoka tamko la kustaajabisha.

CDM kwa kilichowapata mwaka jana, maamuzi ya safari hii yanahitaji umakini wa hali ya juu sana. Bora wakose urais lakini walinde heshima ndogo ya chama iliyosalia, wasipoangali wanaweza kupoteza vyote.
CDM hawako katika hali mbaya. Ikumbukwe anayetakiwa kuhesabiwa mshindi au mshimdwa ni mwananchi.

Struggle hii inapaswa kuwa well above self and individuals benefits.

Uzi huu unawahusu sana CDM:

Siasa za Lowassa, Sumaye na Membe - upinzani

Muhimu kufikiria nje ya box.
ACT ni Chama kilichojipanga.angalau kinaweza pata hata wabunge kumi.kuliko nyinyi ufipa na chama chenu mtaambulia wabunge watatu tu.
 
Hili joka lisipokufa mwaka huu halifi tena.

Muhimu Lisu na Membe waingie kazini kwanza wanauzika na kukubalika kimataifa.ACT waungane na CDM Lisu agombee uraisi na Membe umakamu,waachiane majimbo mfano kusini na Zanzibar waachiwe ACT na Bara Kote CDM hii ndo njia pekee ya kuuondosha udhalimu na propaganda za maendeleo.
 
CCM bado ipo sana. Ila ACT ndio inadhoofisha Chadema, lakini kwa sababu Chadema hakuwekeza kwenye vijana critical thinker ndio maana haioni hili.

Kwa Uimara wa Kitaasisi kwa muda huu Chadema ni Imara kuliko ACT, lakini baada ya Uchaguzi huu zitakuwa zimepishana kidogo.

Nina ushauri mzuri lakini ni mgumu sana. Chadema Imuunge Magufuli, ili ipate sifa njema kwa Umma
 
Hili joka lisipokufa mwaka huu halifi tena.
Muhimu Lisu na Membe waingie kazini kwanza wanauzika na kukubalika kimataifa.ACT waungane na CDM Lisu agombee uraisi na Membe umakamu,waachiane majimbo mfano kusini na Zanzibar waachiwe ACT na Bara Kote CDM hii ndo njia pekee ya kuuondosha udhalimu na propaganda za maendeleo.
Katiba ya nchi hairuhusu unachotaka. Pia Lissu ndio mtu wa kumuachia Membe kwenye hii Scenario pia, Lissu anaweza asirejee Tanzania
 
Mambo yatakuwa mazuri CDM sio chama cha kufa kirahisi, ni chama chenye wapenzi wengi kuliko CCM na kimeenea sana mashinani. Kwa vyovyote kama ccm hawatamzuia Lissu, basi tegemea mtananga wa kufurahisha na kama ACT na vyama vingine vikiungana basi ccm hawana lao.
mbeleko za vyama vingine hakuna mwaka huu.kila timu ishinde mechi zake.
 
Back
Top Bottom