Nini kifanyike, ili hii tabia ya kuachwa achwa iishe?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,174
39,936
Kwa nini umeachwa?

Kuachwa ni udhaifu mkubwa sana kwenye mahusiano.

Kuachwa kunamaanisha hauko 'fit' kwenye baadhi ya maeneo.

Ndio maana zamani, vijana walikuwa wanapelekwa jando / unyago kabla ya kuingia kwenye mahusiano.

Lengo kuu lilikuwa ni kuwafunda kila upande ujue wajibu wake katika mahusiano.

Vijana wakiume walikuwa wakifundwa kivyao, na wakike ni hivyo hivyo.

Lakini nyakati hizi, watu wanaachwa achwa hovyo tu; na wengine wanaona sifa kuachwa achwa.

Je, ni nini kifanyike ili hii tabia ya kuachwa achwa iishe?
 
Kuna mahusiano mengine ukiachwa tu unashukuru mungu utadhani umesamehewa Deni la mkopo wa benki
 
Kwa nini umeachwa?

Kuachwa ni udhaifu mkubwa sana kwenye mahusiano. Kuachwa kunamaanisha hauko 'fit' kwenye baadhi ya maeneo. Ndio maana zamani, vijana walikuwa wanapelekwa jando / unyago kabla ya kuingia kwenye mahusiano.

Lengo kuu lilikuwa ni kuwafunda kila upande ujue wajibu wake katika mahusiano. Vijana wakiume walikuwa wakifundwa kivyao, na wakike ni hivyo hivyo.

Lakini nyakati hizi, watu wanaachwa achwa hovyo tu; na wengine wanaona sifa kuachwa achwa.

Je, ni nini kifanyike ili hii tabia ya kuachwa achwa iishe?
Sema unayempenda akikuacha inauma sana
 
Equation x.... ili dhana ya mapenzi ilete maana ya kupenda na kupendwa ni lazima kuna muda penzi lifike mwisho.

Hiyo ndiyo silka yetu sisi wanadamu.

Siyo kila uliyenaye mtafika mwisho kwenye safari yako wengine ni wasindikizaji, wengine wapo kwa ajili ya kukujenga..
 
Equation x.... ili dhana ya mapenzi ilete maana ya kupenda na kupendwa ni lazima kuna muda penzi lifike mwisho. Hiyo ndiyo silka yetu sisi wanadamu. Siyo kila uliyenaye mtafika mwisho kwenye safari yako wengine ni wasindikizaji, wengine wapo kwa ajili ya kukujenga..
Hakika,
Mahusiano mengine Ni shule kuboresha mahusiano yako yajayo
 
Back
Top Bottom