Nini kazi ya Jeshi la Ulinzi?

Wakukaya2

Member
Apr 26, 2023
75
87
Wakati wa Merchantalism, Nchi za ulaya zilitumia sana Jeshi kutoa ULINZI kwa wafanya biashara na misafara Yao iliyozinguka duniani kote kukusanya vitu vya thamani ambavyo vilikuwa muhimu kwa ustawi wa mataifa Yao.

Kwenye Colonialism naona Hali ni sawa, wazungu kwalitumia Jeshi lao kupata makoloni na kuyasimamia vilivyo kwa manufaa yao. Na hata Leo wakati wa Neo colonialism nafasi ya Jeshi ni kubwa, Nenda Mali, Afghanistan, Iraq n.k utaona makampuni makubwa ya mafuta yanavyolindwa na Jeshi kuvuna mafuta.

Hali ni tofauti kwa hapa kwetu, mfano Moja ya mazao muhimu ambayo huwa yanaingiza pesa za kigeni Tanzania ni korosho, na hakuna mtu asiejua umuhimu wa pesa za kigeni hasa US Dollar hasa kwenye wakati huu wa uhaba wa dola nchini.

Bila wasiwasi wowote ule zaidi ya robo ya korosho zote zikizouzwa nje ya Tanzania zilikuwa zinatoka Mozambique kupitia mpaka wa mtoruvuma. Kwa muda mrefu Mozambique wamekuwa hawatambuliki kimataifa kama wazalishaji wa korosho, hivyo wakulima wao wanategemea soko Tanzania.

Na sisi tunaziuza nje na kuziita zimetoka Tanzania. Kutokana na ukosefu wa utulivu nchi ya Mozambique serikali ya Tanzania imechukua hatua za kufunga mpaka, which is good and fine. Lakini imefunga na korosho zile zisipite.

Hivyo imeathiri pakubwa korosho tunaziuza nje, na hivyo kuathiri uingizaji wa pesa Dola, kwahiyo kuathiri pakubwa foreign exchange reserve ratio.

Kwa takwimu, misimu mingi kabla ya kufunga mpaka tulikuwa tunazalisha korosho zaidi ya tani 300,000 kwa mwaka, tangu korosho izuiliwe kupita uzalishaji umekiwa chini ya tani 150,000, Yaani karibia nusu ya uzalishaji. Halmashauri zinazotegemea ushuru wa zao hili mapato yameshuka sana.

Kwanini serikali isitafute namna ya kuhakikisha korosho zile zinaingia Tanzania? Hivi serikali Kali haioni kuzuia korosho zile kutaifanya Mozambique kuona umuhimu wa kuwatafutia wanunuzi wakulima wao wa korosho? Na sisi itakuwa tumepata hasara kwa kuwa na mzalishaji mwingine ambae tutashindana nae.

Ukizingatia wao wanazalisha muda ule ule ambao sisi tunazalisha? Duniani ni Tanzania pekee inazalisha na kuuza korosho kipindi uiki Cha October Hadi January, kwa hiyo wanunuzi wote huwa wanakuja huku kushindana, bei inapokuwa kubwa kutokana na kuongezeka ushindani na pia pesa inayoingia inakuwa kubwa.

Kumruhusu Mozambique kutafuta soko, ni kupunguza nguvu yetu ya kupanga bei sokoni kama sole producer wa korosho kwa wakati huo, maana Mozambique nae anazalisha muda sawa na wetu, sema tu yeye anategemea korosho auze Tanzania.

Tunapohangaika kutafuta namna ya kuongeza Dollar reserve tuangalia na hapa, maana msimu umeanza, na tarehe 1 October tunaanza kuuza.

Mipaka ambayo serikali wanayoilazimisha kupitisha bidhaa kwa mfano kilambo ya Mtwara na Mamba wa Swala ipo mbali na maeneo yanayozalisha korosho. Wakulima hao wawawezi kugharamia kupitisha huko.

Kwakuwa tuna vyombo imara vya ULINZI na usalama, basi kwa manufaa ya Taifa kutafutwe namna ya korosho zile kuingia Tanzania.

Wenzetu walifaidika sana na Tanzanite yetu na tukalalamika, Sasa kwanini na sisi tusifaidike na korosho ya Mozambique Hadi pale watavyo lalamika?
 
Wazo zuri.

Ivi lile jopo linakaaga kama vile Pentagon ya marekani kuangalia mustakabali wa sera, ziwe za kijeshi au kiraia si hata Tz tunayo?

Saivi na wahindi nao muvi zao wanapenda sana kuweka scene za hivyo. J9po linakaa Srinagar Airbase wapo siriazi kinyama

Ndio kazi zake sasa hizi yanakaa majitu yenye akili kupangilia ishi fulani tuipeleke vipi.

Kama mzee Trump anavyojisifiaga kwamba kwenye issue ya korona waliji 'mobilize' kijeshi it was incredibly fantastic, anapenda vivumishi sana kwenye speech zake.

Anyway najua ndio inavyofanyika
 
Back
Top Bottom