Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Naomba tujiulize vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimeshindwa kuingilia kati huu uchafuzi wakisiasa unaofanywa na viongozi waandamizi wakisiasa?
Hatuwezi kuwa na Taifa ambalo viongozi leo Wana msimamo huu kuhusu rasilimali na kesho wana msimamo ule kuhusu rasilimali zetu na hakuna anayewakemea.
Hatuwezi kuwa na Taifa ambalo kila wanachotaka wanasiasa ndicho kinatokea, kwanini dola isiwadhibiti baada ya chama dola kushindwa kuwadhibiti?
Tunasoma taarifa za wizi kila siku lakini hakuna wanasiasa wanaochukuliwa hatua kuhusu hasara wanayoisababishia serikali na vyombo vya dola vipo kimya.
Nchi inatunga sheria za zakiwawekea kinga wezi na wabadhirifu wa mali za umma, wahujumu Uhuru wa wengine na wakandamizaji wa haki za binadamu lakini hakuna chombo kinachokemea
Vyombo vyetu vinasubiri Rais aseme ndipo wachukue taarifa, wanakwama nini kuchukua hatua jinai inapotendeka?
Ni Siri gani wasizozijua kuhusu mikataba ya nchi? Hii mikataba mibovu inapotungwa wao wanakuwa wapi? Kwanini dola isiwe sehemu ya macho ya mikataba ya nchi? Kama wao ndio macho kwanini wanaruhusu watu wanapotosha taifa na kuuza rasilimali watakavyo just kwa sababu ni wanasiasa?
Vyombo vya dola mnalilindaje taifa na wizi huu wa rasilimali? Mnawafanya Nini majambazi ya kalamu?