Nini husaidia wazungu wanaokaa miaka 3, kujua Kiswahili mpaka lugha za kikabila ila wahindi waliozaliwa hapa wasijue hata kiswahili vizuri?

ryan riz

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
422
675
Hili swali huwa linanishangaza sana! Muhindi ana zaidi hata ya miaka 30 au amezaliwa na kuzeekea hapa ila kuongea kiswahili kwa ufasaha ni shida kubwa.

Ila wazungu wanaokuja kwenye miradi au shughuli zingine kwa miaka mitano tu eneo analofanyia kazi ataijua lugha hiyo kwa muda mfupi, hata kama hapo zinatumiwa lugha zaidi ya moja zote atazijua na kuongea vizuri. Ila wahindi wengi wako mjini tena wana maduka makubwa yaani tunaingiliana sana kupitia biashara lakini kiswahili kwao ni shida.

Je, wewe unaona nini hupelekea hili?
 
Mimi toka bombay kuja hapa fanya biashara..swahili taki jua mimi bhana.

Anyway! Wazungu ni watu wa kujifunza tamaduni za watu muda wote hiyo ipo kwenye damu zao!!watu wa resoning sana..mzungu huwa ana utu sana wengi ambao wamefanya kazi na watu hao wananeemeka.

Mfano; maisha ya mtu anaefanyakaz kampuni ya mzungu yana utofauti wa kiwango cha kimataifa na kampuni za kihindi..
Au mfangizi wa ubaloz wa Marekani, Uholanzi, Norway, e.t.c ana utofauti mkubwa sana na Wa ubalozi wa India

Muhindi anawaza hela muda wote na kunyanyasa waafrika..kuona takataka sio watu wa kujifunza, mara unapita chini kakutemea mate..daah nitoshe kusema wahind ni watu wa kujijali sana kuliko mwingine
 
Penye nia pana njia. Wahindi nao wangeweza tu kama wangetaka. Ila wanadharau kiswahili na waafrika. Wazungu wai wanaweka jitihada nyingi sababu wanakithamini.

Japo sio wote, lakini hao wanaoweza kukijua kwa muda mfupi waliweka jitihada sana. Malengo yao wanapambana sana yatimie. Na huo ni mfano mmojawapo
 
Wazungu wanajichanganya sana na Waswahili! Lau kama shule zetu zingekuwa bora tungesoma hata na watoto wao! Wahindi sasa!!! Shule za Kihindi hindi!!! Kuchanganyika; na Wahindi hindi!! Mitaa wanayoishi; ya kihindi hindi!!!
Mitaa ya uhindini, hata kuoana ni wenywewe kwa wenywewe
 
Hili swali huwa linanishangaza sana! Muhindi ana zaidi hata ya miaka 30 au amezaliwa na kuzeekea hapa ila kuongea kiswahili kwa ufasaha ni shida kubwa.

Ila wazungu wanaokuja kwenye miradi au shughuli zingine kwa miaka mitano tu eneo analofanyia kazi ataijua lugha hiyo kwa muda mfupi, hata kama hapo zinatumiwa lugha zaidi ya moja zote atazijua na kuongea vizuri. Ila wahindi wengi wako mjini tena wana maduka makubwa yaani tunaingiliana sana kupitia biashara lakini kiswahili kwao ni shida.

Je, wewe unaona nini hupelekea hili?
Wee kuwa na aibu kidogo... kiswahili limejaa lugha ya Kiarabu ns kipindi kipo humo...
Usijumuishe wahindi... wapo baadhi ni Waswshili wa mjini.. na wapo Wahindi Expertise!!
 
Back
Top Bottom