Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Kila kitu kina faida na hasara zake.Moja ya faida ya hizi shule za kisasa ni watoto kujua lugha ya malaika angali wakiwa na umri mdogo na kuwa fluent tofauti na wale wanaosoma shule za St. Kayumba.
Hata hivyo, kuna kasoro naiona na ambayo baada ya muda, tutakuja kuiona huko mbele na hii si nyingine bali ni kuwa na kizazi cha watanzania wasioweza kujieleza vizuri kwa kiswahili bali kingereza huku lugha zetu za asili zikiendelea Kopotea kabisa.
Kwanini nasema hivi?
Mazingira wanayokulia watoto wetu wa leo ni tofauti sana na yale tuliokuia sisi.Siku hizi humu mijini kila mtu akijenga nyumba yake anajitahidi kuweka uzi wa ukuta na geti na matokeo yake watoto wetu hawachezi tena pamoja mitaani kama enzi zetu ambapo tukitoka shule, tunakutana mtaani tunacheza pamoja then kigiza kikianza kuingia tunarejea majumbani.
Nini kinatokea?
Watoto wetu hawa wa leo wakiwa katika hizi shule za kisiasa, ni kuongea kingereza mwanzo mwisho tangu wanapoanza shule tena siku hizi wakiwa na umri mdogo (wanamaliza darasa la saba wakiwa na miaka 12 mpaka 13) na wakirudi majumbani ni kufungiwa kwenye mageti mpaka kesho yake tena watapoenda shale.
Athari inajitokezaje?
Watoto hawa tangu wakiwa wadogo,wana-spend muda mwingi shuleni wakiongea kingerez na wakirudi nyumbani wanafungiwa kwenye magoti na hawapata nafasi ya kuchanganyikiwa na wenzao wa St.Kayumba walioko mtaani, hivyo hawakutani na watoto wenzao wanaozungumza kiswahili na matokeo yake wanakuwa wakijua kuongea zaidi kingereza kuliko kiswahili.
Mazingira haya wanaokulia na kulelewa yanafanana na mazingira wanayozaliwa na kukulia wahindi ambao licha ya kuzaliwa na kukulia humu nchini, wanakuwa hawawezi kuzungumza kiswahili fasaha kwani muda mwingi wanatumia lugha yao na kingereza wanachofundishwa.
Na katika hili, bora hata wahindi kwani mbali na watoto wao kufundishwa lugha ya kingereza, bado wanatumia zaidi kihindi katika mawasiliano yao huku sisi hata wazazi wakiendeleza matumizi ya lugha ya kingereza kwa watoto wao wawapo majumbani na kuona huku ndio kustaarabika.
Kujua kingereza ni muhimu kwasababu hiyo ni lugha ya kimataifa ambayo watoto wetu wataitumia kuombea ajira na kushindana na wenzao kimataifa na pia wataitumia kwa mambo mengine but not to this extent ya kuanza kusahau kabisa lugha yetu ya Taifa.
Tuchukue hatua na mojawapo iwe kuongea na kuandika lugha ya kiswahil kwa ufasaha kama ni added advantage kwenye usaili wa ajira za serikali huko mbeleni iwapo hali hii itafikia hatua mbaya.
Mnaweza msinielewa sasa hivi, ila miaka 15 mpaka 20 ijayo, hali hii itakuwa wazi kabisa, na mpaka sasa teyari kuna watoto ambao wako fluent zaidi katika kuongea kingereza kuliko kiswahili.
Usisahau hata mchicha ulianza kama mbuyu.
Tutakuja tena kulaumu wazungu kwa kuua lugha yetu kama ambavyo leo hii tunawalaumu kwa kuua utamaduni wetu.
Alietuloga alikuwa fundi!!