Nini husaidia wazungu wanaokaa miaka 3, kujua Kiswahili mpaka lugha za kikabila ila wahindi waliozaliwa hapa wasijue hata kiswahili vizuri?

inatokana na watu waliokuzunguka. mhindi anaishi uhindini mazingira protected asijichanganye na waswahili, anasoma shule ya kihindi na university anaenda nje ya nchi. atajua kiswahili fasaha? ukitaka kujua hilo, kuna watu uwengi tu hapa tz wana miaka zaidi ya 50 au hata 80 lakini hawajui kiswahili. au nyie wenzetu bibi zenu na mashangazi huko vijijini wanaongea kiswahili kizuri? utakuwa umepata jibu sasa.
 
Wazungu wanajichanganya sana na Waswahili! Lau kama shule zetu zingekuwa bora tungesoma hata na watoto wao! Wahindi sasa!!! Shule za Kihindi hindi!!! Kuchanganyika; na Wahindi hindi!! Mitaa wanayoishi; ya kihindi hindi!!!
hili ndio jibu sahihi.

Mhindi hachanganyiki na mswahili,mzungu utakuta yupo na mmasai,mara yupo na mmakonde mara yupo na mzanzibari bichi boi yani anajichanganya
 
Hili swali huwa linanishangaza sana! Muhindi ana zaidi hata ya miaka 30 au amezaliwa na kuzeekea hapa ila kuongea kiswahili kwa ufasaha ni shida kubwa.

Ila wazungu wanaokuja kwenye miradi au shughuli zingine kwa miaka mitano tu eneo analofanyia kazi ataijua lugha hiyo kwa muda mfupi, hata kama hapo zinatumiwa lugha zaidi ya moja zote atazijua na kuongea vizuri. Ila wahindi wengi wako mjini tena wana maduka makubwa yaani tunaingiliana sana kupitia biashara lakini kiswahili kwao ni shida.

Je, wewe unaona nini hupelekea hili?
Mkuu lazima uelewe wahindi so kama hawajuwi kiswahili vzr.

Ile ni lafidhi yao sababu ya kupenda kutojichanganya na watu makabila mengine.
Muhindi atasoma shule ya wahindi,,

Akirudi atakwenda dukani kukaa na family yake nayo itaongea kiswahili cha lafidhi ile,.

Akienda misikiti yao ni kiswahili hicho hicho,,
.atawezaje kujuwa kiswahili fasaha?

Nenda kakutane na wahindi wa mburahati,,au manzese..daresalam.

Huwezijuwa kama ni muhindi,,

Kiswahili kimenyooka kabisa.

Chukulia mfano mtu wa kabila fulan,,

Mfano tanga,

unaweza ukakutana nae yupo mji mwingine ,,
lakini lafidhi ya kiswahili chake kinaweza kisibadilike kama ataendelea kuwa na watanga wenzie..

Au hata warangi,nk

Kuna watu wapo ulaya au wana miaka zaidi ya 20 hawajarudi Tanzania,,

Lakini ukisikia kiswahili chake hukwepi,,kujuwa kama huyu ni tanga line.

Sababu ya kuendelea na kuishi na wenzio wale wale,

Lafidhi haibadiliki hata kidogo.

Wazungu wanajichanganya uswahilini.
 
Wazungu wanapenda kujifunza kila kitu kuhusu watu wengine wanaishi vipi, wanaongea lugha gani wanakula vyakula gani? Wanapenda kujua vitu tofauti na wakiwa sehemu yoyote duniani wanapenda kuishi kama hao watu wanavyoishi.

Ndio maana utaona wazungu wakienda Tanzania kutalii, watavaa kama masai, watataka wafundishwe vitu baadhi kuhusu tamaduni/mila zao na wengine zile ngoma zao wanacheza kabisa. Watanunua zile bracelet zao wanaita "culture " kama sijakosea.

Hata katika nchi zao, wakijua wewe umetoka kwenye jamii fulani, wanapenda kuuliza kuhusu kujua vile mnaishi.
Ataomba umfundishe kiswahili,au lugha mnayotumia akikuona atakusalimia kiswahili /lugha mama yako.

Ila kwa Wahindi sijaona kama hiki, popote wanapoishi lazima wajitofautishe na wengine. Hawapendi kuchukua tamaduni za wengine.
 
Hili swali huwa linanishangaza sana! Muhindi ana zaidi hata ya miaka 30 au amezaliwa na kuzeekea hapa ila kuongea kiswahili kwa ufasaha ni shida kubwa.

Ila wazungu wanaokuja kwenye miradi au shughuli zingine kwa miaka mitano tu eneo analofanyia kazi ataijua lugha hiyo kwa muda mfupi, hata kama hapo zinatumiwa lugha zaidi ya moja zote atazijua na kuongea vizuri. Ila wahindi wengi wako mjini tena wana maduka makubwa yaani tunaingiliana sana kupitia biashara lakini kiswahili kwao ni shida.

Je, wewe unaona nini hupelekea hili?
Kujichanganya na utayari wa kujifunza na kujaribu.
 
Ningekuwa mhindi ningekuwa zaidi ya wahindi, mgumu kujifunza, hata lugha yangu siijui pamoja na kukulia mazingira ya lugha yangu

Nikiishi na jamii yoyote hata miaka 10 siambulii hata salamu

Nafikiri unavyojiweka ndio namna inakuwa rahisi kujua lugha
 
Back
Top Bottom