Ijue Eczema (Pumu ya Ngozi): Visababishi vyake, dalili zake na tiba yake kwa watoto

Feb 9, 2023
5
9
Eczema (pumu ya ngozi): ni ugonjwa wa ngozi ,unaofanya ngozi kuwasha sana,ngozi kuvimba,kuweka vipele vingi vidogo vidogo venye rangi nyekundu. Ugonjwa huu huanzia utotoni mara nyingi pia hushambulia watoto na wazima, hushambulia sehemu mbali mbali za mwili na viungo vya mwili kama vile kwenye joints za mikono na miguu,shingoni,juu ya jicho, kwapani, mgongoni, tumboni n.k

Huu ugonjwa hushambulia watoto na watu wazima,lakini mara nyingi huanza ukiwa mtoto na unaweza pia kuwa umerithiwa kutoka kwenye familia (baba au mama).

Watoto chini ya miaka mitano huu ugonjwa upo zaidi kwao kwasababu kinga ya miili yao inakuwa ina pambana zaidi kuzoea vitu ambavyo tuna wapa mfano chakula au mazingira wanayo kulia mfano sehemu yenye baridi sana, joto sana au vumbi jingi.

NINI HUSABABISHA KUPATA ECZEMA(Pumu Ya Ngozi)?
Eczema inasababishwa na mwili kushindwa kuzalisha ceramider (fatty cell) ambayo hutumika kwenye uzalishwaji wa ngozi. Ceramider inaposhindwa kuzalishwa ngozi ya mtoto inapoteza kiwango cha maji maji na kuifanya kuwa kavu (dry skin) na ndipo inapo msababishia kuanza kujikuna, ngozi kuwa kavu na kubadilika rangi kuwa nyekundu

VITU VINAVYOWEZA KUCHOCHEA ECZEMA
Vyakula
Mtoto anaweza kupata allergy ya baadhi ya vyakula na kumpelekea kupata Eczma. Mfano wa baadhi ya vyakula hivyo ni: maziwa, soya, mayai, samaki, Nyama, cheese, karanga

Mazingira
Mtoto anaweza kupata Eczema kutokana na kuwa kwenye mazingira kama vile: Baridi,Hali ya ukavu sana, mazingira yenye upepo sana,kung'atwa na Wadudu wadogo, hali ya unyevunyevu, manyoya ya wanyama tunao wafuga nyumbani kama vile mbwa na paka n.k.

Aina ya nguo zenye material kama vile synthetic material

DALILI ZA ECZEMA KWA MTOTO
  • Ngozi kuwa kavu
  • Ngozi kuwasha
  • Kutokewa na vipele vyenye rangi nyekundu
  • Kufifia kwa ngozi
  • Ngozi kuwa na hali kama ya kusinyaa


NINI HUSABABISHA KUCHELEWA KUPONA KWA ECZEMA KWA MTOTO
Ngozi kukaa kavu, Epuka kumuacha mtoto wako ngozi ikiwa kavu ina msababisha kujikuna sana na kusababisha ngozi kuvimba na vipele

Acha kutumia vitu vyenye harufu kali kama vile
perfume, mafuta, sabuni kwenye mwili wake

Epuka kumuosha mtoto kwa muda mrefu au kumuacha kwenye maji muda mrefu, jitahidi usizidishe dk 10.

Epuka kumvalisha nguo zenye material ya mpira mpira.

Epuka kumzalisha nguo za kumbana sana maana zitamsababishia kujikuna.

Epuka kumvalisha nguo nyingi au nzito wakati wa joto itamsababishia kujikuna

Tumia maji ya uvuguvugu unapomuosha mtoto na tumia sabuni ya sensitive skin isiyo na harufu na wala usitumie shampoo kumuosha

TIBA YA ECZEMA KWA MTOTO
1. Tumia Emollients (moisturizing lotion)itafanya ngozi ya mtoto kuwa na enyevu nyevu muda wote na hii itamkinga na kujikuna kutokana na ngozi kuwa kavu.

2. Cream yenye CORTICOSTEROID as Active Ingredient, hii itasaidia kuondoa tatizo la kuvimba ngozi,kuweka vipele vinavyo ambatana na rangi nyekundu.

3. Kutumia sabuni zenye effect ya kulainisha ngozi na kuipa unyevu nyevu ngozi yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom