Nini huleta Sonona?

20PROFF

JF-Expert Member
Nov 5, 2013
7,961
6,740
Nimekutana na taarifa ya Michele Obama, na tatizo la Sonona.

Hii Chini ni taarifa hiyo.

"Ninaamka usiku wa manane kwasababu nina wasiwasi juu ya kitu fulani au nawaza kuhusu mzigo mzito ninaoubeba moyoni." Mke wa Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama bi Michelle amekiri kuwa anaugua sonona (Depression).

Michelle alisema maneno hayo wakati wa kipindi chake cha pili alipokuwa anamuhoji mwanahabari wa Marekani Michele Norris. "Huu sio wakati mzuri, kiroho," Bi. Obama alisema. "Najua ninakabiliana na kiwango fulani cha sonona. "Sio tu kwasababu ya karantini, lakini kwasababu ya ubaguzi wa rangi, na kushuhudia tu utawala huu wa Donald Trump, na kutazama unafiki ndani yake, kila uchao, kunavunja moyo."

Bi. Obama alisema anapitia matatizo na amekuwa na changamoto ya kuendeleza ratiba yake ya kufanya mazoezi ya viungo na kulala.

Source: BBC Swahili


Je, nini hasa chanzo cha Sonona? Nimetumia Michelle Obama kama Case study.
 
Umewah kutana na mtu wa karibu yako, mwenye hiii, kitu??
Kuna mwanamke flani (mtu wa karnu yangu Sana)aliwah kupata hi kitu, chanzo chake ilikuwa ni stress..aliteseka Sana nusura awehuke sababu ya mapenzi ila alikuja kuwa sawa baadae kutokana na kukaa na wana saikolojia walimjenga sana.
 
Kuna mwanamke flani (mtu wa karnu yangu Sana)aliwah kupata hi kitu, chanzo chake ilikuwa ni stress..aliteseka Sana nusura awehuke sababu ya mapenzi ila alikuja kuwa sawa baadae kutokana na kukaa na wana saikolojia walimjenga sana.
Ktk guessing, unahisi,nina kina muwinda huyu, mama Michelle!!??
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom