Heri ya Siku ya Afya ya Akili Duniani!

Heri ya Siku ya Afya ya Akili Duniani!

Ntemi_Ntale

Member
Joined
Aug 23, 2026
Posts
7
Reaction score
3
Kwa nje unaweza ukawa unaonekana mwenye furaha na mafanikio, lakini kwa ndani unapambana na mzigo wa sonoma(depression) na wasiwasi uliopitiliza (anxiety).
Kila siku unaweza ukawa unaamka na uchochoro wa msongo wa mawazo unaotokana na changamoto za maisha na hofu ya kuonekana "dhaifu" kama utaomba msaada.
Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa takribani mtu mmoja(1) kati ya watu wanne(4) hupitia changamoto ya afya ya akili katika kipindi fulani cha maisha yake.
Takwimu za Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa uwiano huo wa mtu 1 kati ya 4 unaakisi pia hali halisi nchini Tanzania, ambapo matatizo kama sonona, wasiwasi, na msongo wa mawazo yanazidi kuongezeka.
Afya ya akili.jpg
 

Attachments

Back
Top Bottom