Nini hukupa faraja pindi unapoishiwa?

Fibanochi

JF-Expert Member
Jun 28, 2018
475
1,015
Kuna kipindi katika maisha hutokea mtu ukafanya jambo ambapo likakufanya siku za usoni ujione shujaa ukikumbuka na kukupa faraja tele lakini katika haya maisha watu wanapita nyakati tofauti tofauti sana kipesa.

Kuna kipindi mtu unakuwa vizuri mfukoni na kufanya mambo kadha wa kadha ya maendeleo kununua unachotaka, starehe unazotaka na kuna kipindi mtu unapigika ile kupigika kweli kweli kiasi hata kukosa hela ya nauli lakini unapata faraja kwa kuona matunda ya assets au matendo mema uliyofanya kipindi uko vizuri kipesa na kujipongeza na angalau unapata nafauu ya katika moyo wako.

Mimi katika vitu vinanipa faraja ni kuwa miaka kadhaa nyuma Kuna mpendwa wangu wa karibu alikuwa katika hali ya kifo na uhai, kiasi kila mtu alikata tamaa, niliweza msaidia kuokoa maisha yake kwa kutoa akiba yangu ya pesa ya boom ili apate tiba, na Mungu mwema alitibiwa na akapona.
 
Mimi sina, ni either nitafute cha kupotezea au huo upepo upite.
 
Hii ni changamoto kubwa sana, rafiki anaepokea Simu zako na kukusikiliza kipindi hauna kitu hakika si wa kumuacha.
Nilipoishiwa mapesa nilifurahi kuwatambua marafiki wa ukweli na batili.Ilinipa faraja sana kuwafahamu.Wale batili siku hizi wakijidai wanarudisha "urafiki" naanza kusingizia sina mapesa kwa vitendo,wanakimbia.Simple!
 
Mimi kitu kinachonipa faraja ni elimu na exposure niliyopata. Nikiwa sina hata senti tano lakini nikumbuka elimu yangu na nchi nilizotembea na kuishi, mambo mageni niliyoona na kujifunza huwa napata faraja sana. Kuna watu wengi wenye fedha lakini hawajabahatika kupata elimu au kuwa na exposure. Kingine ni wanangu.
 
mimi nikikosa hela kama sshv nakuwa mgonjwa pia naota ndoto mbaya mbaya,,mbo haismami asubuhi km nilivyozoea nikiwa na pesa nyingi na uhakika wa maisha...

nachojivunia ni undugu wetu hatubaguani kila muda napigiwa simu.naulizwa km nimekula pia napewa moyo kwamba huu ni upepo utapita tuu..
izi buku5 au ten natupiwa kimtindo!

nitakuwa mchoyo km sitaishukuru JF4U humu hatujuani km nna ela wala sina lakini tunapeana mawazo tunafurahi unasahau shida maisha yanasonga.
 
sijawahi kupata faraja wakati nilipoishiwa, ndio kwanza nilijikuta nazama katika dimbwi la stress, kisirani na unyonge. sikuwa mtu na furaha.

kupata faraja wakati umeishiwa ni sawa na kutaka kuhalalisha kauli ya ufukara ni zawadi kutoka kwa Mungu wakati sio kweli.

kupata faraja wakati umeishiwa ni kujaribu kuzipa uhalali kauli kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wa ccm zikiwemo za yule kubwa lao mwendazake zilizokuwa zinahusisha umasikini na uzalendo na kila tajiri ni mwizi, muuza unga na anakwepa kulipa kodi.

umasikini ni laana na ushenzi, tusiutukuze. tuupige vita kwa namna yoyote ile.
 
Hamna kitu kinaleta faraja kama kupata sapoti kutoka kwa ndugu ukiwa na wakati mgumu huwa inarejesha afya ya moyo haraka sana.Ila siku hizi imekuwa tofauti ndugu hawana time na wewe ila jamaa tu mlokutana ukubwani na kuwa kama ndugu.
 
Faraja yangu ninapoishiwa ni kuwa na chakula + bundle. Kwa maana nitakuwa na uhakika wa kula na kuperuzi mtandaoni.
 
Back
Top Bottom