Nini hukupa faraja pindi unapoishiwa?

Nini hukupa faraja pindi unapoishiwa?

Kupigika kubaya sana aisee asikwambie mtu tena kama umezoea kuzishika hela halafu zikapotea au zikawa zinakuja nakuondoka...
 
Ni vyema sana kuoa au kuoelewa na kipenzi chako, ukiwa kwenye mpigiko hii inaweza kumsaidia kila mmoja wenu maana mkikaa pamoja mkala dagaa wenu, Mwenyezi Mungu amewatengenezea burudani ambayo haijalishi una hela au huna utaenjoy tu mkiwa ndani wawili.....balaa uwe msela halafu umepigika uko mwenyewe ndani, usiku unakuwa mrefu saaana na hesabu nyingi za kujipa moyo..
 
Mie wtt wangu.

Sio tu kuwa nawapenda lkn na wao wananipenda sana. We are very close. They are my friends.

Nikiwa nmechoka au naumwa au sina kitu lkn nipo nao around nafarijika sana.

My first kid ndio kabisa akiniona nipo down tu anasali na kuniombea dua [emoji23]
 
Hua nafarijika nikiwa bado nasoma nilitamani baada ya shule niwe na kwangu ,usafiri ,vibiashara tofauti tofauti ...Nashukuru vyote hvi vimeshapita mikononi kwangu japo Kuna vingine nilivipata na Sasa Sina kutokana na maisha kubadilika ila hamna ninachojutia mapambano yanaendelea...... Ogopa kuishiwa
 
Mama yangu ndio furaha yangu nikiwa sina kitu, nikiongea nae nasikia faraja Sana.

Ananijua nikiwa na stress na pia anajua kunisaidia ili niwe normal
 
Kuna kipindi katika maisha hutokea mtu ukafanya jambo ambapo likakufanya siku za usoni ujione shujaa ukikumbuka na kukupa faraja tele lakini katika haya maisha watu wanapita nyakati tofauti tofauti sana kipesa.

Kuna kipindi mtu unakuwa vizuri mfukoni na kufanya mambo kadha wa kadha ya maendeleo kununua unachotaka, starehe unazotaka na kuna kipindi mtu unapigika ile kupigika kweli kweli kiasi hata kukosa hela ya nauli lakini unapata faraja kwa kuona matunda ya assets au matendo mema uliyofanya kipindi uko vizuri kipesa na kujipongeza na angalau unapata nafauu ya katika moyo wako.

Mimi katika vitu vinanipa faraja ni kuwa miaka kadhaa nyuma Kuna mpendwa wangu wa karibu alikuwa katika hali ya kifo na uhai, kiasi kila mtu alikata tamaa, niliweza msaidia kuokoa maisha yake kwa kutoa akiba yangu ya pesa ya boom ili apate tiba, na Mungu mwema alitibiwa na akapona.
YESU
 
Huwa nafarijika sana nikiishiwa halafu nipate mtu wa kumlaumu.[emoji41]
IMG_20210704_171159.jpg
 
Ni kipindi cha kutafuta sana matumaini kupitia maneno ya Mungu nikiwasikiliza wahubiri kama kina Mwamposa, chief suguye mahubiri yao univusha sana kipindi hiki, marafiki na ndugu wako mbali sana nami najua sababu nimepigika, Mungu mwema najua milango itafunguka tena.
 
Wapinzani wa nchi hii. Huwa nafarijika sana napoona wapinzani wanabadilisha gia angani. Mwaka 2013 walisema tuna rais dhaifu ambaye mpaka leo nchi haina hata ndege moja. Halafu haohao 2018 wakapinga rais kununua ndege eti akanunue madawati. Huwa nafarijika sana maana haya mambo yanachekesha sana.
 
Back
Top Bottom