Nini huchochea binadamu ku-bet kila wakati?

Nini huchochea binadamu ku-bet kila wakati?

Mwabhleja

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2016
Posts
1,369
Reaction score
2,105
Mimi nachukulia Ku bet ni kama kupiga ramli. Tofauti pekee iliyopo ni kwamba MTU anayebet anafanya hivyo kwa uhalali wakati huo huo mpiga ramli yeye amezuiwa na sheria kufanya hivyo.

Kwa kiswahili chepesi ni sawa na kusema MTU anaye bet in mvuta sigara aliyeruhusiwa na sheria wakati mpiga ramli ni mvuta bangi asiyeruhusiwa na sheria. Mwisho wa siku wote watadhurika.

Kilichonifanya niandike Uzi huu, ni kwasababu nimeona kama kuna kitu kisicho cha kawaida kwenye kubet.
Just Imagine, MTU anataka kuendesha familia kwa pesa za kubet. (In Coyo Voice)

Mtu yupo kanisani lakini anaperuzi mitandaoni kupata dondoo abet upande gani.
Wanafunzi wa vyuo hawaanzi FGD kabla ya kujadili namna ya kubet.
Mtu hajanunua Nguo Mpya mwezi wa sita sasa lakini kila wiki anabet.

What went wrong...what went what...?(In Teacher Mpamire Voice)

Sasa naomba wenye utashi tusaidiane maisha hapa. Je hiki ni kitu cha kawaida?
Mtu ana elfu 2000. Anaamua asile wali maini kwa mama Chausiku ili abet hivyo hushinda njaa. Ni roho gani iliyopo kwenye kubet kiasi kwamba hata njaa isn't there any psychological abnormalities for us to discuss?
 
Addiction imewazidi watu mkuu ila kikawaida inapaswa kubet kistaarabu sio kila siku unabet mpaka unajinyima vitu vingine vya maana
 
Betting/gambling is an addiction that is so strong as drug addiction and sometime it may even be stronger than the drugs,so long as it involves money
 
Wanapambana na hali zao mkuu. Acha wabet tu.
 
Kila siku shukuru Mungu kama maisha hayajakufikisha kwenye mahali pa kufanya vile ambavyo hukuwahi kufikiria kama utavifanya!
 
Usikubali kushindwa kama unataka mafanikio,kanuni ya mafanikio wanayoamini watafutao mafanikio.
 
Japo matajiri wanabet lakini matumaini ya masikini katika kubeti ni makubwa kuliko hata matumaini yao ya kuishi .
 
Back
Top Bottom