Na uzoefu unaonyesha kwamba CCM haiwezi kutoka pale ilipo kutokana na kwamba Viongozi wengi wa vyama vya upinzani ni wepesi sana kurubunika na hela za Mafisadi kama tulivyoona hivi karibuni na bado naamini tutaendelea kuwaona.
Mbona makampuni ya private yana ufanisi wa juu siku zote, na wafanyakazi wake ni watanzania? Inakuwaje tuko bize kushawishi wenzetu kwamba eti watanzania hawawezi kufanya mambo mazuri, makubwa wakati mifano hai ipo? Uongozi wa CCM unamgusa kila mtu. Mtu akichemsha kazi au akienda kinyume na taratibu na achukuliwe hatua sirias. Litakuwa fundisho kwa wengine kama system yote iko hivyo, na nchi itabadilika.
Makampuni ya private kuwa na ufanisi wa juu si ipo katika kila nchi mzee? Huwezi kutumia kigezo cha private companies kuonyesha kuwa wananchi wana uwezo wa kufanya kazi. Ukiangalia nchi zote duniani, private companies have proven this, maana wao wako katika profit maximisation. Pia private companies wana uwezo wa kutoa ajira kwa mtu hata wa nje ya nchi, kama itabidi kuweza kutimiza lengo lao. Lakini kwa upande wa public entities, hicho hakipo kabisa. Wewe unadhani kwa nini Tz ina-slow down EAC? Sio hofu ya wakenya kukomba kazi bongo?
Swali linabaki pale pale, kutawekwa vigezo gani kuhakikisha kuwa hizi public entities zitafanya kazi kwa ufanisi upinzani ukiingia? Sijasikia wapinzani wakiongelea hilo kabisa.
-- Cha kwanza ni kukubali kuwa CCM have got better strategies katika mambo ya uchaguzi kuliko nyinyi. Hii itawafanya mtafakari na kugundua weaknesses zenu na kujijenga zaidi katika hizo. Ile ya kipesa - ni bora kuiacha, maana hamtowashinda, they've got the rugged muscle. Nevertheless, there's still a room to reshape your position to a better one.
-- Tambueni strongholds zenu kwenye majimbo na kukubaliana wote kuwa huyu anakubalika zaidi huku au kule.
-- Stronghold zenye wabunge wa upinzani tayari ziendelee kuwa na mbunge huyohuyo wa upinzani au mwingine kutoka chama hicho. Vyama vingine vyote vim-support mbunge huyo mmoja. (Kumbukeni CCM na Urais wa kuachiana wa miaka kumikumi - si kwamba hamna ma-aspirants wengine ndani, bali ni makubaliano tu!).
-- Gawaneni majimbo ya uchaguzi. Mkiacha yale ambayo yanawawakilishi tayari yakibakia hivyo.
-- Kule ambako upinzani haukubaliki kwa sana, jimbo liachwe mikononi mwa mmoja kutokana na tathmini mtakayokuwa mmefanya kutambua majimbo yote magumu na kuwa mmegawana nafasi sawasawa za kuyawakilisha. Jimbo la uchaguzi liwe na mwakilishi mmoja kutoka upinzani na siyo multitude of opposition candidates dhidi ya chama tawala.
-- Lakini kama kuungana kutawezekana (maombi ya Watanzania walio wengi), basi kufanyike walau miezi sita kabla ya uchaguzi mkuu. Mkiungana mapema sana, CCM ni ma-guru katika kuwavuruga, they've got the experience. Watapata muda wa kutosha kuweza kuwatawanya muda mchache uchaguzi ukikaribia. Na mkifanya mmechelewa sana, hamtapata muda mwanana wa kuweza kuwafikia wapiga kura vijijini.
Nawatakia utekelezaji mwema wa strategies zenu.
SteveD.
Mzee Mrema alitoa sharti moja:
Wapinzania washirikiane huku chini, kuanzia vitongoji, Udiwani, na hata Ubunge, lakini suala la uraisi kila chama kiende kivyake!
Hata hivyo anawaomba waiachie TLP kwenye uchaguzi mdogo Biharamulo kwani eti ni jimbo lao!
.....i just threw-up in my mouth after reading the above😕😕,huku si kufilisika kisiasa tu bali kimawazo vileX2.MWENYEKITI wa a Tanzania Labour Party (TLP) Bw. Augustino Mrema amesema kuwa endapo vyama vya upinzani vitaendeleza ubinafsi wa kutoshirikiana katika chaguzi mbalimbali havitaweza kukiangusha Chama Cha Mapinduzi(CCM).
Mbali na hilo pia amekitaka Chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuacha rafu wanazotaka kuzifanya katika Jimbo la Biharamulo badala yake wamuunge mkono mgombea wa TLP Kwani ndiye anayepaswa kuchukua nafasi hiyo.
Alisema kuwa tatizo kubwa ambalo limekuwa likiviangusha vyama vya upinzani katika chaguzi mbalimbali ni ubinafsi unaofanywa na baadhi ya vyama kwa kujiona wanaweza zaidi ya vingine.
Alisema kuwa ubinafsi wa CHADEMA ndio unaosababisha kushindwa kuunga mkono TLP katika Jimbo la Biharamulo kiti ambacho kilikuwa kinashikiliwa na TLP.
Unajua TLP ndio wafiwa, hivyo kama ni kurithi mali alitakiwa arithi lakini kwa ubinafsi wa CHADEMA wameonekana wazi kuanza kucheza rafu huko Biharamulo kwa kumurubuni Katibu wa TLP wilaya kutangaza kuwa hatusimamishi mgombea...waache hizo! Mbona mimi sijasimamisha mgombea kwenye chaguzi zingine kwa nia ya kuunga mkono vyama vingine?, alihoji BW. Mrema.
Kwa sasa Mrema atulie tu....ajitibu kisukari chake....
Maana siasa zake ni kwishneeii.........
Hawezi kuheshimika na kusikilizwa na watu kama kipindi kile alivyokuwa Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza Tanzania. Cheo ambacho hakuna mtu aliyeshika mpaka sasa.........
TULIA BABAAA..........