Nini hatima ya Nyerere Day? Lini mwisho wake?

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Huwa nakaa chini nafikiria sana juu ya Hatima yaani mwisho wa kumkumbuka au kumbukumbu ya Nyerere.

Leo inatimia miaka 22 bila Mwalimu tangu alipo tutoka tarehe na mwezi kama wa leo mnamo Mwaka 1999.

Maswali yangu juu ya Hatima hii leo imetimia miaka 22 pasipo kuwa na Nyerere.
Je, Mwaka gani utakuwa ni mwisho wa kumkumbuka ya Mwalimu? Je, hata miaka 2000 inayo tutaendelea kuwa na Nyerere Day au itakuja kufa.

Na je, kipi kinaweza kufanya Nyerere Day ikome kuadhimishwa?

Najua hapa wapo wenye IQ kubwa kama Zero IQ na Pia wapo wenye IQ ndogo kama Mimi. Hivyo kwa wenye IQ ndogo kama Mimi huenda wakapuuza nankuponda juu ya andiko hili.

Lakini kwa ndugu zangu mlio salia pengine mnaweza share chochote juu ya Hatima ya Nyerere Day na kuoendekeza je, huenda Mwaka/miaka gani inaweza kuwa Hatima ya Nyerere Day na sababu gani zinaweza fanya Nyerere Day ikome.
Maana sizani kama Nyerere Day itaadhimishwa miaka yote na sizani hata miaka 2000 au 3000 ijayo watu wataendelea kuadhimisha siku hii.

Je, nini Hatima ya Nyerere Day?
 
“I learned that everyone dies alone. But if you meant something to someone, if you helped someone, or loved someone. If even a single person remembers you, then maybe you never really die. And maybe, this isn’t the end at all.”

Person of Interest - Quote by the Machine....
 
Asante hivyo kutokana na aliyo yafanya NYERERE ataendelea kukumbukwa?
 
Hii siku ni muhimu sana, lakini inakuwa ya kuliingiza taifa hasara ya matumizi ya fedha kutokana na ukweli kuwa siku hii imekuwa ya kutoa matamko tu ya kumenzi hayati Mwl Nyerere lakini ikipita tu, kila mtu anaendelea na mambo yake, hakuna vitendo!
 
Nawaza ipo siku itajadiliwa na kusema inatia hasara Taifa hivyo ifutwe.
Ni mawazo yangu tu
 
Nyerere angekuwa anatoka kwenye ukoo wenu sidhani kama ungekuja na uzi kama
Mkuu hakuna kitu Cha faraja familia ya Nyerere inajivunia kama kuona anakumbukwa kama hivi, sasa unataka kuipoka faraja ya watu kwanini.
 
Kwani kuuliza ni kosa lengo ni kujua
Unajuaje sitoki ukoo wa Nyerere?
 
Alikataa mawazo mbadala ya kina kambona na mtei singerpore na Malaysia ilikuwa sawa na Tanzania kiuchumi 1960s lakini kutokana na Nyerere kujiona mungu mtu alikataa sera za nzuri za maendeleo
Shukurani mkuu kwa maelezo yako nimepata kitu
 
Alikataa mawazo mbadala ya kina kambona na mtei singerpore na Malaysia ilikuwa sawa na Tanzania kiuchumi 1960s lakini kutokana na Nyerere kujiona mungu mtu alikataa sera za nzuri za maendeleo
Ni ukilaza/utahahira/upuuzi/wendawazimu/ufyatu wa hali ya juu kumchukia Nyerere eti ndie alileta umaskini.
Tangu ameondoka kiti cha urais kodi anakusanya yeye? Uchaguzi anachaguliwa yeye? Vyuo, bodi, wizara, majimbo, kamati anachagua na kuongoza yeye?

Bajeti ngapi zimepita tangu Nyerere ang'atuke. Nyerere kaongoza Tanzania kwa miaka pungufu ya miaka ambayo marais wengine waliofuata waliongoza. Wao walificha akili zao wapi kuifanya Tanzania tajiri na wakati ndio wamekuta resources nyingi zaidi yake? Kwahiyo tule kashata na kunywa kahawa tukimlaumu Nyerere, yeye mmoja kashindwa hao wengine wanne wamefanyaje?

Umaskini wetu unaletwa na Watanzania wengi kuwa wajinga. Mtu tangu 1985 sio Rais ila analaumiwa kwa umaskini, huwezi enda Ujerumani ukakuta wanajiliza wakimlaumu Adolf Hitler kwa kuwaingiza vitani na hasara kubwa waliyopata.

Mwalimu Nyerere ni underrated hasa na watu wake mwenyewe. Alikuwa na uwezo mkubwa kuliko waliofuata ndio maana vikojozi hadi leo wanalilia kwanini hakuwafanyia nchi tajiri. Kumbe ambacho Nyerere hakufanya hakuna mtu yeyote anaweza, hata katiba aliyoacha bado tunayo. Asingeacha multipartism tusingekuwa nayo
 
Shukurani mkuu kwa zege hiyo
 
Back
Top Bottom