Nini dira ya Watanzania kwenye Kilimo na Ufugaji?

Jul 29, 2022
21
42
Leo nimekaa na kutafakari sana kuhusiana na suala hili hasa ikichangiwa na baadhi ya video na clip nilizowahi kuona huko nyuma

1. Misri wameanzisha miradi ya kilimo cha umwagiliaji kwenye majangwa yao hivyo wanatarajia mwaka 2025 kuwa miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa ngano duniani

2. Shajrah UAE nimeona wameanzisha kilimo kwenye jangwa zaidi ya hecta 400,000 ili waweze kuzalisha chakula ambacho hakina viwatilifu( no additives) vyovyote vile kwaajili ya UAE na Dubai

Niliona clip mmoja wa wakulima wakubwa S.A akizilalamikia mbegu za GMO kwamba zinaenda kuaharibu mbegu za asili kutoweza kutumika tena kuzalisha kwasababu zitakuwa zimeharibiwa na mbegu za GMO through cross pollination hivyo kuwafanya wakulima kuwa dependent wa makampuni ya uzalishaji mbegu.

1. Je, sisi kama Watanzania tumejipanga vipi na mabadiliko haya makubwa maana 80% ya sisi ni wakulima

2. Sisi ni nchi ambayo kwa kiasi kikubwa tunategemewa kwenye chakula na nchi jirani kama Kongo, Kenya, sudan lakini mpaka leo hii tumeshindwa kuongeza uzalishaji, kudhibiti mfumuko wa bei kwenye nafaka, tumebaki kulalamika tu wakati tuna maeneo mengi yanafaa kwa kilimo.

3. Kipi tufanye tuweze hasa kuzalisha na kulisha hizi nchi jirani na kujipatia pato zaidi?
 
Kuna kitu kinaitwa demand over supply na hicho ndo kitaamua sekta ya kilimo nchini kufifia au kukua na sio serikali.

Amani iwe nawe.
 
Tatizo letu sisi siasa za sifa zinatuponza sanaa.ndio maaana hatuna dira yoyotee.

Imeshajulikana kua kwa tabia nchi za zama hivi, kilimo pekee chenye tija ni cha umwagiliaji, lakini ukiitafuta mikakati inayo tekelezeka haipo. Tumebakiwa na hekaya tuu za kutoa heka 10 kwa vijana.

Tukiacha hekaya tuka amua kweli kuwekeza kwenye kilimo cha vitendo na sio PDF tunaweza kutoboa.

Huwa sielewi,hivi tukiamua kutoa kipaumbele kwenye budget ya kilimo kwa mia mitano tukawekeza huko nchi itafirisika?
 
Sisi tumezungukwa na maji ya bahari, maziwa na mito lakini tunategemea mvua kwa kilimo
Ni ujinga mkubwaa. Leo kutwa nzima wanakimbizana na wanao mwagilia kwa maji ya mito, huku serikali haina mpango mkakati wa kutekelezeka kuhusu kilimo cha umwagiliaji.
 
Taifa ambalo kila kiongozi anapigana kufa na kupona aendelee kuwa kiongozi kwa ajili ya maendeleo yake na si kwa ajili ya kesho yetu kama Taifa.

Hakuna dira kwenye lolote sio tu kilimo, Kiongozi wa leo anaweza kuwa na maono haya na kuanzisha hili na kesho akija mwengine anaacha na kuanzisha yake yatakayompa sifa kwenye uchaguzi au yenye maslahi na yeye.
 
Nkikumbuka zamani mbegu zetu zilikua Bora ila sasa hivi mbegu zetu zinategea mbolea na madawa Ili uweze vuna mavuno.
 
Egyptians walianza umwagiliaji 6000bc kama miaka 8000 iliyopita

Yaani wao walifanikisha mpaka kupandisha maji juu kwa mfalme bila mitambo.

Umwagiliaji kwao ni maisha ya kale sana.

Sisi tunasubiri sana Na tumegoma kutoka na kujifunza kwa wenzetu
Tunaweza kama tutaona mito yetu sio kwenye wimbo wa Taifa tu, hapo ndio tutafanya kitu.

Mito,maziwa, milima na rutuba yote mali yetu na tumeikuta ila tunaitumia kama nyani tu.

Mnisamehe kwa hilo ila ndio ukweli
Tunategemea siku moja tuwe na soko la matunda kama Floating Market ya Bangkok kwenye Mito yetu.

Ila wa kufanya hivyo wako wapi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom