Nini chanzo cha mahari kuwa juu?

Nini chanzo cha mahari kuwa juu?

Mke akiwa mzuri mkuu, huwezi kupata kitu kizuri kwa bei chee
Acha ww nani kakwambia kuwa kuna mke mbaya? Kila mwanaume anavigezo vyake kwa kila mwanamke ni mzuri machoni mwa mwanume ampendae sharti tu awe ametimiza vigezo stahiki, kwa hiyo mzuri kwako anaweza akawa mbaya kwangu, lakini mzuri kwangu akawa mbaya kwangu pia.
 
Kwanza;Wazazi baadhi ya wazazi wengi wamekuwa wakiongeza mambo ambayo hayana umuhimu sana,utakuta binti ametaja mahar yake ya kawaid tu lkn baada ya hapo kuna vitu hivyoooo vikiorodheshwa hapo kitu kinawezakufika kweny milion 4 na kuendelea that's too bad

Pili;Binti mwenyew kutaka ufahar,watu wajue kwamba ameolewa kwa pesa nyingi kana kwamba yeye ni mzur sana au ana kitu kinachofanya mahari yake ni kubwa

Japo siamini kama binti kuweka mahari kubwa huwa anafanya kwa ajili ya kumkomesha mwanaume Ila tu ni kama mashindano imekuwa baina ya familia,ndugu,majirani

Inapendeza zaid kukubaliana kwanza na mtarajiwa wako kiasi atakachoweza kukitoa then mtu ukifika kwa wazazi unasema tu jmn pesa yenu isizidi kias kadhaaaaaaaaa tofaut na hapo patachimbika

Mwanamke msimamo

Mbna umesahau kuhusu Mkaja wa mama na baba, hv vitu sjui vinatolewa wapi
 
mtoto wa kike anatumia gharama kubwa sana mpaka kuolewa. kwa mfano kibaiolojia mtoto wa kike atahitaji ela ya ziada kipindi cha kubalehe na mzazi makini lazima ataziweka hizo gharama kwenye mahari
Hilo ni jukumu la mzazi kumgharamia mtoto wake
 
Back
Top Bottom