Mxiuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!! Yaani kiumbe wewe umenichefua jioni ya leo acha tu!
Yani huto tu upendeleo tunaopewa kwa kunguziwa tu machungu kinukta ndo umekuuuma sanaaaaa!
Ndo tabia gani na unafiki wa hali yajuu kujifanya umesahau/ kujisahaulisha kwa makusudi Ukweli ya kwamba Wanaume na mfumo wenu dume mmetukandamiza karne na karne na bado mnaendelea huko vijijini! Eeeeh!
Ndo nakwambia hivi dawa yenu inachemka! Acha tuchukue chukue Uraisi wa baadhi ya nchi ndo mtapoisoma namba.
Wanaume watu wabaya sanaaaa!
Pamoja na kutusulubu karne na karne ila bado hamjarizika na walivofaidi babu zenu bado na nyie mataka! Kupewe chance ya kuandika Vitabu vitakatifu ndo kutumia huo mwanya kudumisha mfumo dume?????? Na hamjatosheka bado mpaka leo mmedumisha MFUMO DUME MAMBO LEO
1. Mwanamke hana Ubini, lazima achukue wa mwanaume either baba yake au mmewe! Huwezi kuwa Ms. Lara officially! Lazima uwe Miss either baba au mume.
2.Mwanamke aliekamilika ni yule alieolewa na kudumu kwenye huo mfumo dume. Hata upate maendeleo kiuchumi vipi kama huna mume bado naonekana una kasoro.
3. Mwanaume mmoja anatembea na nyie hata 10, either mnajuana, mnahisiana, ama vovote yeye keshafaidi nyie mtajiju.
4.Mke bora si yule anaekuza uchumi bali ni yule mtumwa bora kwa mumewe na kufata matakwa ya binadamu mwenzie wa kiume na kupambana awezavyo kuvumilia coz akibaki nanyanyasika na akiondoka atazaraulika tu. No way out!
5.Mama bora ni yule asijinafasi mshahara wake na kujibanaaa ili atunze familia kuokoa jahazi ilihali mumewe anaweka heshima bar. Wanao wakiwa ovyo mumeo hawamshangai! Wanakula sahani moja na wewe tu mama.
6.Mchumba bora ni yule anaemlea Bf kama mtoto. Ukijitia akili na maarifa mengi utazeekea nyumbani.
7.Mwanamke akipata cheo katanua miguu kwa wazito, hana lolote. Hata mumewe anakuwa na mahaka na hicho cheo cha ghafla!
IFIKE MAHALI WANAUME MKUBALI KUTULIPA FIDIA KWA MAOVU YENU NA BABU ZENU MLIOTUFANYIA NA MNAYOENDELEA KUTUFANYIA. MTU ACHIE POOO! KIDOGO!