Nini 787 dreamliner na tugemee nini?

Lengo kubwa la kununua hizi ndege hasa hii kubwa inaonekana ilikuwa ni kujijenga kisiasa na ndio maana imeandikwa hapa kazi tu.

Sidhani kama walijipa muda wa jinsi gani ya kufufua hili shirika kibiashara bali inaonekane waliwaza kulifufua kisiasa zaidi na ndio maana hata hii ndege imepokelewa kisiasa wakiamini wanawakomoa wapinzani na ndio maana pia walielekeza vijembe kwa wapinzani.

Si ajabu sasa ndio wanaumiza vichwa ni namna gani watamudu kuendesha hili shirika na hususani hiyo ndege kubwa na hizo zingine zinazotarajiwa kuwasili siku za usoni.

Wakati wao wanadhani zile mbwembwe zilikuwa ni za kutuma ujumbe kwa upinzani, ni mbwembwe hizo hizo ambazoni wapinzani watakuja kuzitumia kama reference wakati wa kuwasuta na kuwakosoa.

Time will tell.
 
Huo ndio ukweli mtupu. Ndege hutumia lita tano kwa second!!!!
 
Kila kitu kina matatizo madogo madogo ni wakati wa kufanya kazi na kuacha majungu juu ya hili suala tusiwe na mihemko kwenye keyboard zetu. Haiingi akilini hata kidogo mtu hajui chochote kuhusu vyombo vya usafirishaji wa hata nchi kavu lakini anavyoshikilia bango hili swala la ndege tena kwa story za vijiweni utadhani ana uelewa juu yake, haya mambo tuwaachie wenye taaluma zao maana ndege ni ya Tanzania lakini kuna uangalizi uliofanyika kimataifa ili kuepuka madhara.
 
Ndege zinanunuliwa bila kufuata bajeti wala tender process.

Halafu kuna watu wanashangilia.
Ujinga ndio mtaji wa watawala
Mpaka sasa 1.5tl zimepigwa bila maelezo na watu wanaendelea kushangilia ndege
 
Tuwe tunaangalia na mazuri pia ya serikali yetu
Ukilitimba unaweza chelewesha maendeleo
Leo hapa ingefuatwa process huenda hadi magu anatoka tusingenunua hata ndege ya abiria kumi
Nchi inayojiendesha bila kufuata Sheria haina tofauti na Kijiwe
kama Sheria mbovu mko wengi simzibadilishe ni ujinga MTU anaedhani mzalendo kuwa ndio sheria
 
Shida wengi wenu mnadhani biashara ya ndege ni kama Daladala
 
Wadangayika tunapenda sana Maisha yakufiirika na huu ndio mtaji wa watawala
 
Hizo changamoto ni za kawaida. Ni kama zilivyo kwa Airbus na hata aina nyingine za ndege za abiria!

Liliniumiza ni gharama za ununuzi aisee!

Yani dola Bilioni 32?
Hivi hii ni sawa na Bajeti ya wizara gani?
Sina taarifa lakini kutuambia Boeing wametumia dola bil 32 yaani shilingi trillion 64 kutengeneza dreamliner inatia mashaka.
F 35 Stealth fighter yenyewe mbali na kuwa the most expensive fighter jet, haifikii gharama hiyo. Aliyesema haya aweke sawa taarifa zake.
 
Mawazo kama haya ni mtaji mkubwa wa watawala mufilisi wee unashindwa kusema hadi muda ufike Unajua kiliponunuliwa kivuko kibovu na watu kuhoji unajua Kimepelekwa wapi....naleo mnataka watu wasiseme mpaka Financial Statement ipelekwe Jeshini
 
Budget ya Wizara ya Habari na budget ya wizara ya Mazingira! Hatariiii
Hizo changamoto ni za kawaida. Ni kama zilivyo kwa Airbus na hata aina nyingine za ndege za abiria!

Liliniumiza ni gharama za ununuzi aisee!

Yani dola Bilioni 32?
Hivi hii ni sawa na Bajeti ya wizara gani?
 
Budget ya Wizara ya Habari na budget ya wizara ya Mazingira! Hatariiii
Dah aisee...si wangechota kiasi wa visenti warekebisha "ighulu la mwitundah na Kuluzilambwa" na Nyayo za Mguu wa Yesu kule Nkinto Mkalama ili watalii wafike? ...hahahaaa
 
mwalimu jkn alipofariki aliletwa nchini na ndege ya Atc ile ilienda wapi? nani alishiriki kuuwa shirika la ndege nani analifufua kama kweli? mpango kazi ni upi ama mwanunua kwakuwa rwanda wanazo. mme scan mazingira?
Ile ndege iliharibika ikiwa uwanja wa ndege wa mwanza. Damage ilikuwa kubwa mno kiasi kwamba kutengenezeka ilikuwa ni ngumu.
Waliipeleka kwenye karakana iliyoko uwanja wa ndege wa mwanza.

Since then serikal haijawahi kutoa tamko lolote kuhusu hiyo ndege. Wakakaa kimya.

Kilichoua shirika ni sera ya ubinafsishaji.
Sera mbovu kuliko zote.
 
Mawazo kama haya ni mtaji mkubwa wa watawala mufilisi wee unashindwa kusema hadi muda ufike Unajua kiliponunuliwa kivuko kibovu na watu kuhoji unajua Kimepelekwa wapi....naleo mnataka watu wasiseme mpaka Financial Statement ipelekwe Jeshini
Hapa pia ni njia ya kusema. Ulitaka kama sikubaliani/nakubaliana na ununuzi wa ndege niite waandishi? Muda utasema ndio sababu hakuna unaloweza kufanya wewe kama wewe zaidi ya kutoa maoni. Au ulitaka tufanyaje zaidi ya kutoa maoni na kusubiri matokeo?
 
Sawa boss lakini Sasa tufanyaje zaidi ya kusubiri kama upo sahihi tushuhudie hizo hasara? Kwa sababu hakuna la kufanya zaidi ya kutoa maoni, basi we wait and see who was right and who was wrong. Kuna msemo unasema if you don't like what a leader is doing, climb up. Overthrown his/her leadership and do what you blv is right. Kinyume na hapo Toa maoni then relax and watch the show.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…