Jamaa_Mbishi
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 10,185
- 7,381
Dream liner ni ndege mbovu zilizokataliwa duniani kote. Hivyo ni janga litakalotuletea mabalaaaaa
Aliyelinunua atapata taaabu sanaaa...
Hakuna siasa hapa kaka mfianchi wewe kama una taarifa za kitaalamu kuhusu mauzo na namna ndege hii itakavyotengeneza faida weka hapa. Usi comment tu kuonekana na wewe ume comment weka data hapa tupate faida sote
Acha akili mgando weweDream liner ni ndege mbovu zilizokataliwa duniani kote. Hivyo ni janga litakalotuletea mabalaaaaa
Aliyelinunua atapata taaabu sanaaa...
mwalimu jkn alipofariki aliletwa nchini na ndege ya Atc ile ilienda wapi? nani alishiriki kuuwa shirika la ndege nani analifufua kama kweli? mpango kazi ni upi ama mwanunua kwakuwa rwanda wanazo. mme scan mazingira?Wana Jukwaa. Ni jana tu tumetoka kushuhudia kuwasili kwa ndege yetu inayoitwa Boeing 787 dreamliner. Wengi wetu nadhani bado hatufahamu kwa kina ni nini hasa kimewasili na mategemeo ni yepi katika kukuza uchumi wa Taifa hili.
Hii ni ndege ambayo imeundwa rasmi na kampuni na Boeing kutoka marekani kwa ajili ya kuruka umbali mkubwa (long haul aka long range) na ina uwezo wa kuchukua abiria kuanzia 242 hadi 335 kutegemea na jinsi utakavyopanga viti. Uzinduzi rasmi wa ndege hizi za dreamliner ulifanyika kwa mbwembwe nyingi mnamo July 8 2007. wadau mbali mbali wa safari za ndege duniani nzima walichangia katika ujenzi wa ndege hizi na mpaka kufika December 15, 2009 Dreamliner ilifanya safari yake ya kwanza na ilipofika mwaka 2011, Boeing walitangaza rasmi kuwa sasa Dreamliner zipo tayari kwa mauzo.
Kufikia October 26, 2011 Shirika la ndege la Japan liitwalo ALL NIPPON Airways walitoa oda yao ya kwanza kununua dreamliner, ndege hizi ziliingia kwenye ushindani rasmi wa kibiashara mnamo August 7 2014 na mpaka kufikia mwezi May mwaka huu 2018 Dreamliner tayari walishapokea oda ya ndege 1,377 nyingi zikinunuliwa na shirika la ndege la Marekani liitwalo American Airlines. Tangu kuundwa kwake na kuanza kuruka ndege hizi zimeshuhudia matatizo kadhaa ikiwemo kuripuka kwa battery (on board fire) wakati zinaruka kibishara. Hio ndio historia fupi ya mgeni wetu huyu dreamliner ambapo imewagharimu Boeing kiasi cha dola za Kimarekani billioni 32 kama gharama za matengenezo.
Kama nilivyoainisha kabla Boeing wamepokea oda zipatazo 1,377, lakini hadi sasa ni ndege 691 pekee ambazo tayri zimefika mikononi mwa wateja tokea kuundwa kwake.
January 8 2013 Shirika la ndege la Japana waligundua uvujaji wa mafuta katika moja ya dreamliner zake, na hivyo kusitisha safari ya kuelekea Boston ghafla wakati abiria wakiwa tayari kwa safari.
January 9 Shirika la ndege la Marekani walilalamika kutokea kwa cheche za moto (wiring problem) karibia kabisa na mahala ilipo battry.
January 13, 2013 ilitokea tena kuvuja kwa mafuta katika moja ya dreamliner.
January 14, 2014, Kuonekana kwa moshi wakati ndege ikiwa angani tena karibu kabisa na mahala ilipo battery. Na kasoro nyingi nyenginezo.
Tutegemee mwanzo mgumu sana. Kuwa na ndege moja inayoruka umbali mrefu (long haul) kuna ugumu wake hasa linapojitokeza suala la technical issues na ikalazimika ndege kutokuruka, kitu ambacho ni cha kawaida sana katika mambo ya ndege, na ndio maana wenzetu Ethiopian Airways wakajenga hoteli zao maalum (ziligharimu Dola milioni 91) kwa ajili ya abiria inapojitokeza kuchelewa kwa ndege kwa sababu za kiufundi (delay) kama hizi nilizoainisha hapo juu, inagwa wenzetu wapo na ndege nyingi za kuwasaidia kuhaulisha abiria na haraka inavyowezekana. Hapo tutegemee Delay, na hili lisipofanyiwa kazi linaweza kutugharimu baadae kibiashara, na pia kujiandaa na kipindi cha matengenezo ambapo ni lazima ndege isafiri (labda Ethiopia) kwa matengenezo ambayo nayo huchukua muda.
Ukifikiria hayo na mengine mengi utaona tuna safari ngumu sana ya kwenda kwa mfano mgeni huyu anatumia lita 6,811 kwa saa, piga hesabu Dar/Mwz ni mwendo wa saa moja na robo kwenda na kurudi masaa mawili na nusu utaona ugumu uliopo katika kuendesha ndege hii. Nilitegemea mapokezi ya kimya kimya na badala yake kutumia muda mwingi kuwaza na kuwazua kutafakari ni kwa vipi mgeni huyu ataleta faida. ITS NOT GONNA BE EASY FELLAS!!!
View attachment 805866
niambie lolote kuhusu yale maduka ya Msd tuliyoambiwa yanafunguliwaNdege ni nzuri na italeta faida
waliouza za mwanzo zile za nyerere ndo wananunua hizi za sasa! sitashangaa siku wakijenga nyumba mpya ummaMtoa mada katoa angalizo based on facts ya hizo dream liner, suala la kutiana moyo ni la kwako, ila hixo ndio baadhi ya changamoto zake. Ikifanya kwa mafanikio ni sawa, ila ikizingua sijui Makonda atapiga risasi wangapi kwani hizo kelele zake sipati picha.
Mada ni ndege mkuun
niambie lolote kuhusu yale maduka ya Msd tuliyoambiwa yanafunguliwa
"mfano mgeni huyu anatumia lita 6,811 kwa saa" hili jambo unauhakika nalo, kutoka USA mpaka TZ itatumia lita ngapi? kwa muda wa masaa 13 hadi 16? mnapoongea muwe na uhakika. unajua hiyo ni Sh ngapi mafuta tu. hapa kunauongo kabisaaa.
ha ha haDream liner ni ndege mbovu zilizokataliwa duniani kote. Hivyo ni janga litakalotuletea mabalaaaaa
Aliyelinunua atapata taaabu sanaaa...
ukisema sema unaambiwa mchawi si mzalendoNdege zinanunuliwa bila kufuata bajeti wala tender process.
Halafu kuna watu wanashangilia.
Uzalendo ni pamoja na kuisema serikali inapotumia fedha za walipa kodi bila kufuata bajeti wala tender process.ukisema sema unaambiwa mchawi si mzalendo
Muda utasema. Hesabu hazidanganyi. Faida na hasara ni hesabu. Hizi ndege si za raisi, wala hazijaandikwa jina lake. Labda kuna mahesabu ambayo wameyaona wewe huyaoni. Hivyo muda utaongea. Wasi wasi wangu tu ni kwamba kama upo sahihi basi taifa tutakuwa tumepoteza muda na rasilimali. Hope haupo sahihi. Kwangu mm nadhani ubinafsishaji ulikuwa ni kosa.Sababu kubwa na ya msingi, ambayo hata serikali yetu iliishaikubali na kuitekeleza katika zoezi zima la ubinafsishaji, ni kwamba, serikali kazi yake kubwa ni kuhakikisha nchi ina mazingira mazuri ya kufanya biashara, si serikali kujiingiza katika kufanya biashara.
Hususan kwa makampuni ambayo yanaleta hasara.
Ndiyo maana tukabinafsisha mashirika mengi ya umma, CCM wakasema wanataka kubinafsisha mashirika, hususan yaliyokuwa yanaendeshwa kwa hasara.
Cha ajabu wamebinafsisha yaliyokuwa yanaendeshwa kwa faida (NBC, Container Terminal ya Bandari) wakati makampuni yanayoendeshwa kwa hasara kama ATC serikali bado inayakumbatia mpaka leo.
Serikali ya Marekani ilishagundua kwamba biashara ya mashirika ya ndege ni biashara kichaa, ni biashara ambayo serikali ikijiingiza, inajiingiza zaidi kwa kujionesha "na sisi tupo duniani" zaidi ya kufanya biashara yenye faida.
Ndiyo maana wenzetu wajanja wakajitoa katika biashara hiyo kama serikali, wakaachia sekta binafsi ipambane, serikali ikawa imeweka mazingira mazuri tu ya ushindani.
Sisi kwetu mpaka leo tunapiga mark time ya Vienna Waltz, one step forward, two steps back.
Leo tunataifisha, kesho tunabinafsisha, keshokutwa tunataifisha tena!
Hata mimi na hope sipo sahihi, lakini maandishi yapo ukutani.Muda utasema. Hesabu hazidanganyi. Faida na hasara ni hesabu. Hizi ndege si za raisi, wala hazijaandikwa jina lake. Labda kuna mahesabu ambayo wameyaona wewe huyaoni. Hivyo muda utaongea. Wasi wasi wangu tu ni kwamba kama upo sahihi basi taifa tutakuwa tumepoteza muda na rasilimali. Hope haupo sahihi. Kwangu mm nadhani ubinafsishaji ulikuwa ni kosa.
Maelezo umeyapangilia vzr! Na changamoto ulizoorodhesha zina uhalisia. Ila kama sijakosea(correct me if am wrong) maelezo ya raisi ni kwamba shirika la ndege inabidi lifufuke ili kukuza sekta ya utalii. Badala ya watalii kutumia ndege za inchi zingine basi watumie za kwetu. Ndo maana nkasema, hesabu hazidanganyi. Mi suala la muda tu. All in all JPM asingenunua ndege angepoteza nini? Na hizi ndege ni za nchi, yeye ataondoka madarakani ataziacha. Labda shirika lijiendeshe kwa hasara life kama mwanzo. narudia tena, hesabu hazidanganyi. Muda utaongeaHata mimi na hope sipo sahihi, lakini maandishi yapo ukutani.
1. Sekta ya ndege dunia nzima iko tricky sana, inahitaji weledi wa hali ya juu kwenda nao, sisi kwa historia yetu ya ATC hatuwezi kusema tumefika hapo. Tulitakiwa kufanya baby steps, kuimarisha technical capabilities, kuimarisha uongozi, kuimarisha viwanja kabla ya kununua midege mikubwa.
2. Tuchukue uzoefu kwa waliofanikiwa, walifanyaje? Nilikuwa namsikiliza CEO wa Ethiopia Airlines anahojiwa na BBC. Akaulizwa, sekta ya usafiri wa anga ni ngumu sana, Ethiopia mmewezaje kufanikiwa hivyo? Akajibu, sababu ni nyingi, ila moja la msingi ni kwamba wataalam tumeachiwa tufanye maamuzi yetu kitaalamu, serikali na wanasiasa hawajatuingilia katika biashara.
Tanzania serikali ya Magufuli haiwezi kufanya hivyo, inaingilia sana wataalamu.
Kama una wasaa na nafasi msikilize mwenyewe hapa (6 minutes clip and worth the insight) --> BBC World News - Africa Business Report, 11/08/2017 GMT, Why is Ethiopian Airlines so successful?
Sisi Tanzania tunafanya tofauti, biashara inaenda kisiasa, maamuzi yanafanywa kisiasa. Serikali inanunua ndege kisiasa. Hata uzinduzi wa ndege ni shughuli ya kisiasa.
3. Midege mikubwa hii inafaa zaidi kwa routes ndefu za kimataifa. Tanzania soko kubwa sana la safari za ndege ambalo halina ushindani mkubwa sana ni safari za ndani. Kwenye safari ndefu, ATC haina advantage ya "economies of scale". Haiwezi kushindana na Wa Ethiopia, Waturuki, Qatar etc. Hatujafikia hata standards za kimataifa za kurusha direct flight from Dar to New York kwa mfano. We are setting ourselves for failure either way. Tukiitumia ndege kubwa kwa safari za ndani hatuwezi kuitumia ipaswavyo, kwa safari za nje hatuna competitive advantage.
4. Ndege hizi zinakuja na mikataba ya matengenezo. Unaponunua ndege kutoka kampuni tofauti tofauti,unakuwa na mikataba na makampuni tofauti tofauti. Sijaelewa logic ya kununua Bombardier halafu pia tukanunua Dreamliner. Hususan kwa shirikadogokama letu. Maana yake tutalipa charges fulani kwa kampuni mbili wakati tungeweza kuwa na "economies of scale" kubwa zaidi kama tunge stick na kampuni moja.
5.Kama manunuzi ya ndege hayajafuata bajeti wala a transparent tender process, sina imani sana na muendelezo wa mradi huu. Tutaangaliaje "cost benefit analysis" wakati hata manunuzi yalivyofanyika hatujui? Nasikia Zitto anaomba mkataba, akifanikiwa kuupata na kutujulisha atakuwa kafanya jambo la maana sana.
Inaonekana, kiujumla, kwamba serikali hainunui ndege ili kumaliza tatizo la usafiri walakutengeneza faida (sehemu nyingi hazina hata viwanja vya ndege vya kuweza kui accommodate hii ndege). Inaonekana serikali inanunua ndege kubwa kwa ulimbukeni wa kujionesha "na sisi tumo, tuna ndege kubwa", bila hata ya kuwa na mipango mizuri ya kuhakikisha shirikala ndege linaweza kujiendesha vizuri.
Unasema hesabu hazidanganyi, ni kweli. Mimi pia nakubali hesabu hazidanganyi.Ingawa uhasibu na takwimu vinaweza kudanganya vizuri tu.Maelezo umeyapangilia vzr! Na changamoto ulizoorodhesha zina uhalisia. Ila kama sijakosea(correct me if am wrong) maelezo ya raisi ni kwamba shirika la ndege inabidi lifufuke ili kukuza sekta ya utalii. Badala ya watalii kutumia ndege za inchi zingine basi watumie za kwetu. Ndo maana nkasema, hesabu hazidanganyi. Mi suala la muda tu. All in all JPM asingenunua ndege angepoteza nini? Na hizi ndege ni za nchi, yeye ataondoka madarakani ataziacha. Labda shirika lijiendeshe kwa hasara life kama mwanzo. narudia tena, hesabu hazidanganyi. Muda utaongea
Mkuu kweli watalii watapanda ATC waiache Qatar na Emirates na mashirika mengine ya kimataifa,kwanini Raisi asijiimarishe Zaidi katika ndege za matumizi ya ndani ya nchi,ndege zinazokwenda masafa mafupi,..kama vile Bombardier!?Maelezo umeyapangilia vzr! Na changamoto ulizoorodhesha zina uhalisia. Ila kama sijakosea(correct me if am wrong) maelezo ya raisi ni kwamba shirika la ndege inabidi lifufuke ili kukuza sekta ya utalii. Badala ya watalii kutumia ndege za inchi zingine basi watumie za kwetu. Ndo maana nkasema, hesabu hazidanganyi. Mi suala la muda tu. All in all JPM asingenunua ndege angepoteza nini? Na hizi ndege ni za nchi, yeye ataondoka madarakani ataziacha. Labda shirika lijiendeshe kwa hasara life kama mwanzo. narudia tena, hesabu hazidanganyi. Muda utaongea