Nini 787 dreamliner na tugemee nini?

Mtegemee kupata taabu sana kwa umbeya wenu. Mngekuwa na akili za kuangalia financial projections na profitability mngewasaidia dada zenu wanaouza kwa bei ya hasara sasa hivi. Mtapata taabu sana nasema.

Maoni murua kabisa kaka Nduka wewe kweli ndio unaakili na hutopata tabu kabisa.
 
Mimi naomba tupeane moyo sio kuvunjana

Mkuu DJ Sepetu hio kupeana moyo ndio ilipolifikisha taifa hapa lilipo. Mwenyewe alienunua ndege sio mtu wa kupeana moyo huwa anaongea kwa jinsi anavyojua, watu wakifa njaa kwa ukame huwa anawaambia kabisa kufeni lakini hapa hakuna chakula cha bure..... hakuna kupeana moyo kaka, tunaangamia kaka
 

Mkuu umenena vyema,tatizo hataki kutumia wataalam wamshauri, anatumia ukoo kumshauri,watu kama wewe ni muhimu ila nafasi ya kumshauri huwez kuwa nayo kwa sababu ya ubinafsi,
Hyo ndege hata aseme ataninyonga wallah haitafika popote
 
Dharra ni kweli tuna safari ndefu sana, pia changamoto ulizotuonesha. Sasa nini ushauri wako katika hili la kufufua shirika letu la ndege!!!!???

Mkuu eliakeem mimi nilikuwa humo kwenye airlines kwa miaka kadhaa, ninachokisema hapa ni kuwa tutafakari kwa kina ni vipi vipaumbele kwa shirika hili kabla hatujafanya uwekezaji mkubwa. Ndege ya size ya kati zingefanya vizuri sana kwa sasa. Tungewekeza kwenye zile zile ATRs na ndege aina hio, taratibu tunakuwa na kupevuka kiakili katika biashara ya ndege. Karibuni tu hapa jengo la ATC lilitaka kupigwa mnada kwa sababu ya madeni, tena tukasikia tuna matatizo na IATA, kidogo tunasikia ndege moja imekuwa grounded Mwanza kutokana na hitilafu za kiufundi... tungeanza taratibu kwanza haraka hizi za nini?
 
Wana Jukwaa. Ni jana tu tumetoka kushuhudia kuwasili kwa ndege yetu inayoitwa Boeing 787 dreamliner. Wengi wetu nadhani bado hatufahamu kwa kina ni nini hasa kimewasili na mategemeo ni yepi katika kukuza uchumi wa Taifa hili.
Ningeomba sana uendelee na kazi yako ya biashara ya bodaboda au bajaji na hata daladala lakini mambo ya ndege uachie watu wenye upeo wa kuweza kuelezea mambo! Naona sasa kila mtu aki-google na kusoma vi- mistari viwili vitatu kuhusu aina ya hizi ndege basi hapo hapo anajigeuza mtalaam mshauri!
 
Kama kweli umewahi kuwa ''humo kwenye airlines'' kwa miaka kadhaa basi bora unyamaze kwani nyie ndiyo mlioua shirika letu. Ingekuwa busara mkakaa kimya na kuachia wengine waje na mawazo yao na wakishindwa wakishindwe kivyao.
 
"mfano mgeni huyu anatumia lita 6,811 kwa saa" hili jambo unauhakika nalo, kutoka USA mpaka TZ itatumia lita ngapi? kwa muda wa masaa 13 hadi 16? mnapoongea muwe na uhakika. unajua hiyo ni Sh ngapi mafuta tu. hapa kunauongo kabisaaa.

mbogo31 tunasimama kwenye kukoselewa tuambie hapa ukweli ni upi? kutoka Seattle Marekani ilipokuwa assembled mpaka dar es salaam ni mwendo wa masaa 22 na dakika 39 kwa ndege za abiria na ni lazima usimame kwa ajili ya kuongeza mafuta njiani. Ndege yetu labda imetumia 13 mpaka 16hrs sababu haikuwa na mizigo wala abiria kwa hio hakukuwa na sababu ya kujaza mafuta. Kama unajua ukweli weka hapa tupate faida kaka hii ni ndege yetu sote watanzania tunachangia mada ili kupata uhalisia wa nini kinaendelea sio siasa hapa.
 
Kama kweli umewahi kuwa ''humo kwenye airlines'' kwa miaka kadhaa basi bora unyamaze kwani nyie ndiyo mlioua shirika letu. Ingekuwa busara mkakaa kimya na kuachia wengine waje na mawazo yao na wakishindwa wakishindwe kivyao.

Kaka sijawahi kufanya kazi ATCL hata mara moja. Nimekuwa nchi jirani na nje kidogo. Nimeona si busara kukaa kimya wakati ninacho cha kuwahabarishia Watz wenzangu. Kama kuna wengine watakuja na mawazo yao ni vizuri ndio kujifunza.
 
Kuna mambo yanaimiza vichwa sana ila wengi hatuoni, naukisema unaonekana huna uzalendo, anyway let's wait and see
 

Nakubaliana na wewe sana, baadhi ya wataalamu wanahoji kulikoni hadi sasa hawajaweka schedule ya ndege kwenye system ukitegemea wataanza kuruka hivi karibuni? mkuu Umkilo nikuulize umeona popote kwamba ATCL wame merge na Shirika la utalii kujiandaa na kutoa mpango kazi? wapi umeona? tupe data mkuu
 
Kaka sijawahi kufanya kazi ATCL hata mara moja. Nimekuwa nchi jirani na nje kidogo. Nimeona si busara kukaa kimya wakati ninacho cha kuwahabarishia Watz wenzangu. Kama kuna wengine watakuja na mawazo yao ni vizuri ndio kujifunza.
Ulichoandika kwenye post yako hakinishawishi kukubali kweli kuwa wewe unajua undani wa biashara ya ndege! It is too shallow! (Ila siyo kama nasema hakuna mapungufu kwenye ununuzi wa hizi ndege, la hasha. Inaonekana kabisa hakuna maandalizi ya kutosha kwani hata ukiingia kwenye webiste ya shirika bado ni ya kiwango cha chini sana.
 
Routine maintenance huwa inafanyika kila ndege inapotua uwanjani. Si mpaka iharibike, check ups zote zinafanyika kabla ndege haijaondoka na hii inafanyika kila ndege inapotua..
Ni utaratibu wa dunia nzima.

Engineer gani hapa mwenye Ratings za Boeing kutengeneza dreamliner? mtaje. mimi naongelea Check B na Check C siongelei daily preflight checkups mkuu. Hizo ndio za kila siku na zinajuilikana
 
Hii ni ndege maalumu kwa safari za nje na humu nchin zinatumika hizo zilizotangulia acheni kupotosha na kuleta siasa za maji taka,watu wana akili zaidi yako wewe.
 
For sure sijaona na hizi ni vitu za wataalamu wetu sasa kufanya hiyo coodination. ni swala la taaluma
 

Ni nani huyo mwenye upeo? kama wewe unao upeo weka utaalamu wako hapa. Ndege sio ya watu wenye upeo ni ya Watanzania wote, mimi na wewe pia ni watz kaka, wewe kama huna upeo sawa ila mimi nina upeo na ndo maana nikaweka ninayoyajua bayana hapa. Miaka zaidi ya 10 nipo kwenye biashara ya ndege na nadhani nasema ninacho kijua. wewe sio lazima kuchangia msubiri tu mwenye upeo aje aweke upeo wake.
 
Hii ni ndege maalumu kwa safari za nje na humu nchin zinatumika hizo zilizotangulia acheni kupotosha na kuleta siasa za maji taka,watu wana akili zaidi yako wewe.

Hakuna siasa hapa kaka mfianchi wewe kama una taarifa za kitaalamu kuhusu mauzo na namna ndege hii itakavyotengeneza faida weka hapa. Usi comment tu kuonekana na wewe ume comment weka data hapa tupate faida sote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…