Ningependa Kulipwa kwa Bitcoin… Je, TRA Watanifunga?

Ningependa Kulipwa kwa Bitcoin… Je, TRA Watanifunga?

FestoKaguo

Senior Member
Joined
Apr 1, 2022
Posts
128
Reaction score
202
Kama freelancer au mtu unayefanya kazi za mtandaoni, kuna siku inawezekana ushawahi pokea message au utapokea email au message ikisema, "I’d love to pay you in Bitcoin. Are you okay with that?" Na hapa ndipo swali linapojitokeza kwa wengi wetu hapa Tanzania: Kama nikilipwa kwa Bitcoin, JE! TRA watanifunga?
1746041699575.png

SWALI LA KWANZA UNALOPASWA KUJIULIZA NI JE, Bitcoin inaruhusiwa Tanzania?

Jibu la haraka haraka ni Ndiyo inaruhusiwa, lakini sio rasmi.
Kwa sasa, Tanzania haijakataza umiliki au matumizi ya crypto kama Bitcoin, Ethereum na Solana. You can legally own and receive Bitcoin; hakuna sheria inayokupiga marufuku kwenye hilo. Hata hivyo, Bitcoin haijatangazwa kuwa legal tender, yaani sio aina ya fedha inayotambuliwa rasmi kwa malipo kama iliyvo kwa shilingi ya Tanzania.
1746042045624.png
1746041968512.png


Kwa hiyo huwezi kumlazimisha mtu apokee Bitcoin kama malipo ya bidhaa au mshahara kwa mkataba wa kazi. Lakini unaweza kuipokea kama malipo kwa hiari yako tu na hilo ni halali linaruhusiwa, mradi tu ufuate utaratibu wa mapato kutoka mamlaka ya mapato nchini Tanzania.​

Lakini pia mtu mwingine anaweza akauliza swali, Je, unapaswa kulipa kodi endapo ikitokea umelipwa kwa Bitcoin au cryptocurrency?

Absolutely YES, Kwa mujinu wa sheria ya Kodi ya Mapato ya Tanzania (Income Tax Act) inasema wazi ya kuwa mapato yoyote yanayopatikana ndani au nje ya nchi yanapaswa kuripotiwa, bila kujali kama yametoka kwa fiat, crypto, bidhaa, au hata huduma ya kubadilishana. maarufu kama exchange.

Kwa mfano, ikiwa leo umepokea 0.001 BTC kama malipo ya kazi, na siku hiyo thamani ya Bitcoin labda tuseme ilikuwa ni TZS 200,000,000, basi una wajibu wa kuripoti hiyo TZS 200,000,000 kama income. Hiyo ndiyo inayopaswa kukadiriwa kwa kodi.

And yes, even if the client is outside Tanzania and paid you in a non-fiat currency, it still qualifies as income under the law.

Je, TRA watajua kama hutajaza taarifa hizi?

Lakini hapa nikutoe hofu tu; technically, TRA hawana ni njia ya moja kwa moja ya kufuatilia wallets zako (kama unatumia non-custodial wallets like Trust Wallet au cold wallets). Lakini kutokujaza taarifa zako kwa hiari ni kosa la kisheria, na kama ikitokea ukaguzi wa mapato (audit), ushahidi wa malipo hayo ukiwepo unaweza ukajikuta unaingia matatizoni.

The golden rule is this: Mapato si lazima yawe ya mkataba au benki ili yahesabiwe kama taxable. Transparency ni msingi wa uaminifu kati ya raia na mamlaka ya kodi.


Kwani Tanzania ina mwongozo rasmi wa crypto taxation?

Kwa sasa? Hakuna.
TRA haijatoa mwongozo maalum wa crypto taxation kama ilivyo kwa nchi kama South Africa, Kenya, au Nigeria. Hii inasababisha watu wengi kubaki kwenye kiza wakidhani kwamba kama sheria haijaeleza, basi hakuna wajibu wa kutoa ripoti.

Lakini hiyo siyo tafsiri sahihi ya kimamlaka. TRA ina nguvu ya kisheria ya kutafsiri income broadly, na crypto inaangukia hapo. Kwa hiyo, ni bora uwe na record nzuri ya malipo yote, ukiambatanisha screenshots, wallet addresses, na historical exchange rate ya siku ulipopokea malipo.


Kwa nini haya ni muhimu?​


Tukiwa kama sehemu ya kizazi cha kidigitali, tunahitaji si tu kuishi kwenye blockchain, bali pia kuzingatia uwajibikaji wa kodi. Many African creators, developers, designers, and researchers are now earning in crypto — lakini wachache ndio wanafikiria kuhusu compliance.


Ukijenga jina lako kama freelancer anayeaminika na anayejali sheria, unajitengenezea nafasi nzuri ya kufanya kazi na mashirika makubwa zaidi — hata kimataifa.


Kwa kifupi:​


  • Kulipwa kwa Bitcoin si kosa.
  • Kutokulipa kodi juu ya mapato ya Bitcoin, hilo ndilo kosa.
  • Hakikisha unajua thamani ya BTC siku unapopokea malipo
  • Keep records, be honest, and grow your digital career sustainably.



✍️ Imeandikwa na Festo Kaguo – Researcher & Crypto Analyst, founder of Smart Research Academy.
 
Back
Top Bottom