Ningekuwa sina ajira ningefanya jambo moja ambalo lingenipelekea kuajiriwa haraka na kwa urahisi

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,761
36,350
Hii njia ambayo nitaianika hapa si njia rasmi na si njia ya kuweza kutumiwa kichwakichwa. Hakikisha suala la ajira na sifa kedekede unazitupa mbali, let's say vitakuja automatically.

Ningefanya upelelezi kwa kina, ningeweza hata kufanya jambo kwa muda wa mwaka mmoja ili nikusanye taarifa za kweli na uhakika.
Ningefuatilia mtandao mmoja wa ujambazi kwa kina nipate details zao zote.
  • Ningemjua mkuu wao
  • Center yao kuu
  • Wanapoficha silaha
  • Idadi kamili ya genge lao
  • Muda na wakati wanaofanya matukio n.k, n.k
Kisha naandika barua kwa OCD, RC au kwa Afisa usalama wa wilaya au mkoa kuhitaji kuonana naye. Najua katika watu ambao hawakatai meeting na raia ni watu wa ulinzi na usalama.

Unaweza kutaka kuonana na meneja mkoa TANROADS au dawasa ukazungushwa miezi na miezi ila kwa upande wa ulinzi na usalama haiko hivyo.

Siku nikikutana naye namweleza kukereka kwangu na vitendo vya uhalifu nchini hivyo kwa mapenzi ya dhati nimejitolea kuchunguza uhalifu kama jitihada za kusaidia dola.

Nitampa fuul information za hilo genge.

NB: Mweleze hatua hadi hatua ulizopitia katika investigation yako ili kumwondolea mashaka juu yako asije kuhisi ulihusika kwa namna moja au nyingine.
 
Hakuna jambazi mpumbavu kama unavyofikiria.

Ukifanya hivyo utauawa ndani muda mfupi tu.

Hakuna jambazi asiye na connection na viongozi wa polisi.

Ndio maana ukitaka kuzuia ujambazi, waite hao viongozi wa polisi WAPIGE BITI.

Matapeli tu wa magari wana net work mpaka central huko, sembuse jambazi wa bank.

Labda unaongelea vibaka kama panya road
 
Unapoenda kuonana nae hakikisha ndugu zako wanajua mana utawekwa ndani ili kusaidia upelelezi mpaka hao majambazi wapatikane. Lakini pia majambazi sio wajinga kiasi hcho mpaka wakupe details zao zote hzo.
 
Soma hiki kisa cha ukweli hapa chini ili upate picha ni kwa namna gani hayo majamaa yana OPERATE shughuli zao πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
 
πŸ˜€πŸ˜€ Wazo lako ni zuri lakini halitekelezeki hapa Puerto Rico ninapoishi mimi na wewe, hayo mambo yapo kwenye movies za Magharibi huko.
 
wa magari umeenda mbali hao wa simu tu wana connection huko huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…