MWONA MBALI
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 460
- 610
Nilisha andika mahala kuwa CHADEMA ni chama kikubwa ila idara yake ya uenezi na propaganda ni dhaifu sana.
Ningekuwa mwana CHADEMA labda ningeshauri wasingeiacha tarehe 5 November ipite kama inavyopita.
CHADEMA ni chama cha mawazo ya pili , yaani mawazo shindani leo hii raisi ameitisha kikao na waandishi wa habari kuzungumzia mazuri na changamoto za utawala wake, upande wa pili pia ulikuwa na haja ya kusikika ili kuipa changamoto serikali.
Ni masikitiko yangu kuwa CHADEMA haina watu wa mikakati ya kisiasa, watabaki kudandia matukio wasio weza kuyamaliza kama operation ukuta na sasa wamedandia hoja ya muswada wa habari (ukisoma mazungumzo ya rais na wana habari ) utagundua hoja hii imeshapita tayari na CHADEMA wanapambana kushindwa tu.
Ningetamani kuona CHADEMA inatumia fursa za kisiasa zilizopo kwa mfano ingekuwaje kama CHADEMA wangeandaa dua maalum ya kuliombea taifa na hutuba fupi za ndani wakaalika waandishi na kuipa siku hii ujumbe maalum kama ''Tanzania yetu na uhuru wa kidemocrasia' au 'wakati ukuta' au wakaipa siku jina maalum kama 'maumivu day' ili mradi hii siku isipite bila kuwa na maoni ya upande wa pili.
Nasikitika sana kuona fursa hii hawakuiona kama zilivyopita zingine, kwa kutokufanya hivyo wanaruhusu mashambulizi ya kisiasa yaje upande wao na mwisho wa yote ni CHADEMA kutoaminika kwa jamii.
Badala ku kuandika meseji za kutukana wakuu wa mikoa kama alivyofanya Lema ni vizuri wangetumia akili zao kuimarisha idara yao ya uenezi na propaganda.
Nawasilisha