Ningekuwa kiongozi Afrika watu weupe/wanjano wangeshika adabu (waafrika wanavo baguliwa nchi za wazungu)

Dreams LLC

JF-Expert Member
Jun 15, 2013
449
513
umofia kwenu,
Bara la Africa nadhani kweli bado tupo gizani,huwa sielewi kwanini wengi wa viongozi wetu huwa wanawakumbatia watu wa rangi tofauti na yetu,licha ya sisi kutendewa mambo ya ajabu na hawa watu tukiwa nchi zao.Sijui ni kuwa huwa tuna chagua na kuweka madarakani watu ambao hawana exposure ama ni huwa wanajitoa ufahamu ili mradi wanapata personal benefit.

Note;Nimesafiri na kuishi nchi mbalimbali,ila nina shida na hii nchi ambayo nipo sasa hivi (china).Kwa mtu ambaye hajafika china anaweza dhani hawa watu ni wastaarabu kweli na wanania ya kusaidia Afrika,ila kiukweli hawa viumbe ni wabaguzi wa rangi kweli kweli,zaid rangi ya mtu mweusi ni ya mwisho kwao.Nimekaa china zaidi ya miaka sita(isingekuwa kupata riziki nisingekuwa hapa).Corona virus ilivoanza walikuwa wakilalamika kweli kubaguliwa USA,ila hali ilivyo sasa kwao wao ndo wabaguzi kuzidi.

Afrika hatuja kumbwa na maambukizi ya kutisha ya corona kama mabara mengine,lakini uchina sasa hivi waafrika ndio watu ambao hawawezi kutembea mtaani kwa amani.mashuleni,mitaani, nk ni waafrika pekee ambao wanapimwa corona virus ,kukataliwa huduma kama taxi,pharmacy nk kisa corona ni kitu cha kawaida.

Najiuliza corona si imeanzia china ,leo mtu mweusi anabaguliwa sababu ya corona kweli tena akiwa sehemu corona ilikoanzia?Nimendika haya sababu binafsi masahibu hayyamenikuta.Nimepigiwa simu na police mara mbili (mara zote wamefika ninapoishi na madaktari kunipima corona virus ) mara mbili,jana na leo,ilihali taarifa zangu zote wanazo na sijasafiri nje ya mji niliopo toka january (nilikosa ndege kurudi nyumbani).waafrika pekee ndio wanao pimwa,tuamke tupinge hizi tawala za kishenzi,nashangaa sana Congo kukubali kuwa sehemu ya testing ya corona virus vaccine.Nimeendika kutokana na experience nimepata mahali nilipo (guangzhou).

Mtu unaachiwa bus zima kisa ni mweusi na wanahofia uko na corona ilihali corona imeanza kwao.Viongozi wetu ama mabalozi wetu nadhani wamelala usingizi wa pono,Nikipata cheo tu Afrika,hizi ngozi waandike wameumia. 😬 😬

nitarudi jukwaani hasira ikiisha:mad::mad:
 
Mbona umeenda mbali kote huko! Sisi wenyewe tunabaguana...wachina hata kama ni wabaguzi lakini kibiashara tukonao njema sana...wametuletea vitu vingi vya kujiendeshea life, upande wa viwanda n.k...Mzungu hafai..
 
Mchina sio kuwa anatupenda,mchina anapenda pesa.Mchina rafiki yako akijua atapata kitu toka kwako,akishapata hahaha atabadilika hadi utaona nyota aridhini 😂
 
Hahaa ila kwa upande wangu mchina ana unafuu mkubwa kuliko mzungu...asilimia kubwa ya watanzania na all africans tunategemea bidhaa zake, magari ya kazi, viwanda, n.k..akiamua kuisusia afrika tumekwisha...
 
Mbona umeenda mbali kote huko! Sisi wenyewe tunabaguana...wachina hata kama ni wabaguzi lakini kibiashara tukonao njema sana...wametuletea vitu vingi vya kujiendeshea life, upande wa viwanda n.k...Mzungu hafai..
Fikra za kitumwa unachagua mkoloni

Hakuna atakaye kusaidia wewe isipokuwa mwenyewe

Mchina,myahudi,muarabu,muajemi,mzungu au mhindi kila mtu ana interest zake hakuna anayekupenda wewe hilo ulijue.

China Africa ndo soko lake kuu amelitawala mwenyewe huku so sio kwamba anakusaidia anafanga biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo nijisaidie bila vitendea kazi! Akili gani hizi mzee mwenzangu 😀 mchina amerahisishia sana watu wenye kipato cha chini
 
Kutegemeana kwa kufanya biashara nilzma kwani unahisi UCHINA Haifanyi Biashara N Wazungu

Ila kunatakiwa kuwepo nahali yakuheshimiana

Sent using My COVID-19
 
Kwahiyo nijisaidie bila vitendea kazi! Akili gani hizi mzee mwenzangu 😀 mchina amerahisishia sana watu wenye kipato cha chini

kuna siku akili zitakukaa sawa.Umewahi panda basi,abiria wote na dereva wanashuka kisa mweusi,unaitiwa police na una wekwa karantini?Biashara au tumbo visifanye ukauza utu wako.
 
Utumwa unautafuta mwenyewe, na kujihisi all the time unatengwa...unatakiwa ubadilike ili usijihisi mtu wa kutengwa....unakuwa kama mtoto wa zinaa bwana!
 
kujihisi all the time unatengwa...unatakiwa ubadilike ili usijihisi mtu wa kutengwa....unakuwa kama mtoto wa zinaa bwana!

kwani mkuu wewe akili unayoitumia umeazima?Watu wametoka kwa bus kisa mtu mweusi umeingia,wamepigia police wanakuja kukuchukua na unawekwa karantini afu wewe unasema tunajihisi tu tunatengwa.Kwako maana ya kutengwa ni nini?mtoto wa zinaa ni wewe unayekubali kuwa treated as shit kisa you are not developed as them.Anyway mimi sio mwalimu wako.ova
 
umofia kwenu,
Bara la Africa nadhani kweli bado tupo gizani,huwa sielewi kwanini wengi wa viongozi wetu huwa wanawakumbatia watu wa rangi tofauti na yetu,licha ya sisi kutendewa mambo ya ajabu na hawa watu tukiwa nchi zao.Sijui ni kuwa huwa tuna chagua na kuweka madarakani watu ambao hawana exposure ama ni huwa wanajitoa ufahamu ili mradi wanapata personal benefit.

Note;Nimesafiri na kuishi nchi mbalimbali,ila nina shida na hii nchi ambayo nipo sasa hivi (china).Kwa mtu ambaye hajafika china anaweza dhani hawa watu ni wastaarabu kweli na wanania ya kusaidia Afrika,ila kiukweli hawa viumbe ni wabaguzi wa rangi kweli kweli,zaid rangi ya mtu mweusi ni ya mwisho kwao.Nimekaa china zaidi ya miaka sita(isingekuwa kupata riziki nisingekuwa hapa).Corona virus ilivoanza walikuwa wakilalamika kweli kubaguliwa USA,ila hali ilivyo sasa kwao wao ndo wabaguzi kuzidi.

Afrika hatuja kumbwa na maambukizi ya kutisha ya corona kama mabara mengine,lakini uchina sasa hivi waafrika ndio watu ambao hawawezi kutembea mtaani kwa amani.mashuleni,mitaani, nk ni waafrika pekee ambao wanapimwa corona virus ,kukataliwa huduma kama taxi,pharmacy nk kisa corona ni kitu cha kawaida.

Najiuliza corona si imeanzia china ,leo mtu mweusi anabaguliwa sababu ya corona kweli tena akiwa sehemu corona ilikoanzia?Nimendika haya sababu binafsi masahibu hayyamenikuta.Nimepigiwa simu na police mara mbili (mara zote wamefika ninapoishi na madaktari kunipima corona virus ) mara mbili,jana na leo,ilihali taarifa zangu zote wanazo na sijasafiri nje ya mji niliopo toka january (nilikosa ndege kurudi nyumbani).waafrika pekee ndio wanao pimwa,tuamke tupinge hizi tawala za kishenzi,nashangaa sana Congo kukubali kuwa sehemu ya testing ya corona virus vaccine.Nimeendika kutokana na experience nimepata mahali nilipo (guangzhou).

Mtu unaachiwa bus zima kisa ni mweusi na wanahofia uko na corona ilihali corona imeanza kwao.Viongozi wetu ama mabalozi wetu nadhani wamelala usingizi wa pono,Nikipata cheo tu Afrika,hizi ngozi waandike wameumia.

nitarudi jukwaani hasira ikiisha:mad::mad:
View attachment 1410408
Nina hasira hapa acha tuu naomba mungu nisikutane na mchinkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona umeenda mbali kote huko! Sisi wenyewe tunabaguana...wachina hata kama ni wabaguzi lakini kibiashara tukonao njema sana...wametuletea vitu vingi vya kujiendeshea life, upande wa viwanda n.k...Mzungu hafai..
Wewe ni mtu wa KITU na sio UTU ndio maana hujamuelewa mleta mada.

WODE MAYA kule youtube nimeona akilalamikia na kuonesha videos. Kusema ukweli sio kitendo kizuri kabisa na cha kushangaza balozi zetu zinafanya nini kule kama watu wetu wananyanyaswa?
 
Idd Amini alijaribu kufanya unachofikiria, kilichoikumba nchi yake alishika adabu

Mzee kama wewe ni masikini itabidi uwavumilie tu, maana utarudi kwenye zama za mawe kwa jinsi Afrika isivyo ma teknolojia ya kufuga hata nyuki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umasikini wa nchi nyingi kwenye bara letu ambalo ni tajiri kwa rasilimali ndio unafanya tudhalilike.

Ukiwa kiongozi pambana kuboresha hali za maisha ya raia wako (kiuchumi) na atakaye pokea kijiti cha uongozi yeye pia akitimiza vyema wajibu wake baada ya miongo kadhaa hakuna atakayetudharau.
 
Toeni hoja zenu ni dhaifu sana achana na waafrika tuanze na Watanzani mtu anatamka live"bora ya Corona kuliko mpinzani" ninyi mnakomaa nchina kumbuka dhambi ya ubaguzi haiishii kwa ndugu tu ina tabia ya kuvuka mipaka ya ukoo.Sasa tulieni mnyolewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikubwa ambacho kinatutesa waafrika hatuna umoja,..na hilo linaanzia kwenye nchi husika,unakuta kuna matabaka kati ya serikali na wananchi.waafirika ni wabinafsi sana uroho wa madaraka ndio unawagawa waafrika.
 
kuna siku akili zitakukaa sawa.Umewahi panda basi,abiria wote na dereva wanashuka kisa mweusi,unaitiwa police na una wekwa karantini?Biashara au tumbo visifanye ukauza utu wako.

Tatizo letu tunapenda mno kulalamika, kujinung'unisha na kujiona wenye kutengwa...kule mtwara mzungu aliambiwa "CORONA" kama ni wewe umefanyiwa kwenye nchi yao utajisikiaje!! So, la bus tu limekuuma ila la Mzungu umejifanya kujikausha sio!
 
Back
Top Bottom