Ahmed, sisi tulizoea kumwita "Hemed" wakati tulipokuwa watoto. Mimi binafsi namfahamu sana Hemed, alikuwa rafiki yangu wa karibu sana wa utotoni, wakati huo tunaishi Tabora, eneo la Cheyo Road- ilikuwa kati ya miaka ya 1974 na 1976 baadae tulianza shule pamoja, Cheyo Primary School, Tabora. Wakati huo baba yake alikuwa na cheo kikubwa cha polisi pale Tabora (sina kumbukumbu, ila nahisi alikuwa OCD).
By then familia zetu zilikua very close kiasi kwamba siku nilipopata taarifa za kuhusika kwake na issue ya Ulimboka na kumsimulia mama yangu, tulilazimika kukumbuka picha tulizopiga pamoja wakati huo. Hemed ananijua sana, nahisi hata siku akikutana na uzi huu atajua umeandikwa na nani.
Mara ya mwisho nilikutana nae JKT Ruvu mwaka 1989/1990, kama sikosei yeye akiwa E-coy na mimi nikiwa D-coy.