Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtela Mwampamba, Mar 19, 2013.

 1. M

  Mtela Mwampamba Verified User

  #1
  Mar 19, 2013
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 537
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kabla ya yote ningependa kuanza na maneno yafuatayo ya Utangulizi wa hiki ninachotaka kukisema hapa kama ifuatavyo:

  USALITI;
  Usaliti ni neno pana sana...,
  Lina madhara mengi sana...,
  Hujuma hukwamisha mambo mengi sana...,
  Tamaa huzaa usaliti...,
  Usaliti huleta maumivu kwa waliokuamini...!

  Baada ya Utangulizi huo naomba sasa nieleze vipi ninavyomfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA nikishabihisha ufahamu wangu huo kwake na matukio yanayoendelea hivi sasa.

  Katika mfululizo wa matukio yanayoendelea hapa nchini hasa yanayogusa medani za siasa za ndani ya nchi pamoja na jamii kwa ujumla wake, katika yote lipo tukio moja ambalo ni kubwa na lenye sura ya kuogofya. Kwa kuwa tukio lenyewe lipo katika mchakato wa kimahamakama sitalizungumza bali nitazungumza nje ya Wigo wa kesi hiyo ili nisiingilie hatua za kimahakama na nisivunje sheria za nchi.

  Nitakachokisema hapa ni namna tu ambavyo nimewahi kumfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA ambae ni mmoja wa washukiwa wa matukio ya kigaidi.

  Nilikutana na LUDOVICK pindi nilipokuwa Mwanafunzi wa Shahada ya kwanza ya Ualimu (BACHELOR OF ARTS WITH EDUCATION "BAED") katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Campus ya DUCE mwaka 2008-9 nikiwa mwanafunzi wa Mwaka wa pili, LUDO akiwa mwaka wa kwanza.

  Nikiwa ni miongoni mwa vijana wana mkakati na wapinaji wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nikiendesha shughuli mbalimbali za kukijenga na kukiimarisha Chama hiko katika maeneo ya Vyuo Vikuu, nikiwa nina wajibu na majukumu ya kuwashawishi vijana kujiunga na CHADEMA na kuwajengea imani na matumaini ya kupata Maisha mzuri na Ajira katika taasisi mbalimbali za kijamii zilizo affiliated na Chama hiko, ndipo nilipokutana na LUDO na kuzungumza nae kisha kuungana pamoja kuijenga CHADEMA. (LUDO akiwa mwaka wa Kwanza akifanya BAED-history & political science).

  Harakati zetu ziliendelea kwa mafanikio ambapo tulikuwa tukipanga na kufanikisha mikakati mbalimbali ya kuandaa matukio na mijadala ambayo tulialika vongozi wakuu wa CHADEMA kuja kuzungumza issues mbalimbali za kitaifa na kichama. Katikati ya Mwaka 2009 nilipata wazo la kuanzisha Jumuiya ya wanafunzi chini ya CHADEMA, ambapo CHASO ilizaliwa, nikiwa ni muasisi na "mwanzilishi pekee" wa Jumuiya hiyo ya CHADEMA STUDENTS ORGANISATION (CHASO), Ilianza kazi rasmi ya kuwaweka pamoja wanafunzi wanachama wa CHADEMA mimi nikiwa ni MWENYEKITI wa kwanza wa jumuiya hiyo.

  Tulipata mafanikio makubwa kwani tuliweza kuwashawishi wanafunzi wengi kujiunga na Chadema, haya tuliyafanya PAMOJA. Hata ilipofika mwaka 2010 niling'atuka kama Mwenyekiti na kuiacha jumuiya hiyo katika mikono salama ya LUDOVICK, ambapo aliendelea nayo jumuiya mpaka Mwaka 2011, alipokuwa Mwaka wa Mwisho naye alikabidhi Uenyekiti kwa Peter John shughuli ambayo ilifanyika katika Ukumbi wa TTC Chang'ombe na mgeni rasmi alikuwa ni Dr. Slaa ambapo aliambatana na Dr. Azaveli Lwaitama-mhadhiri wa UDSM.

  Baada ya kuhitimu chuo, LUDO alikuja Makao Makuu ya CHADEMA kama Volunteer ambapo alijumuika tena na volunteer wengine (mimi nikiwemo tangu mwaka 2008) ambapo LUDO alipewa kazi ya kupambana ndani ya mitandao ya kijamii.

  Ilipofika Mwanzoni mwa Mwaka 2012, LUDO alikuwa amepangiwa TABORA kama Mwalimu wa Sekondari ambapo LUDO alikwenda kuanza maisha mapya ya kufundisha, ambapo Mwezi mmoja tu baadae Dr. Slaa alimuita arudi Makao Makuu na kumuweka katika Idara ya Ulinzi na Usalama, Chini ya WILFRED LWAKATARE.

  Nitaeleza kwa ufupi kwanini Dr. Slaa alimpa LUDO kazi hiyo:-

  1. LUDOVICK alisoma shule ya seminary na pia alisoma masomo ya Uchungaji kwa miaka minne, hivyo alikuwa ni mtiifu sana kwa Dr. SLAA na pia aliamini amesoma kwa undani mafunzo ya kutunza siri na uaminifu.
  2. Pia LUDO alikuwa akiwa ni mtu anayepeleka taarifa kwa Dr. SLAA kuhusu viongozi wengine ndani ya CHADEMA na pia alikuwa akitumika katika mitandao ya kijamii kuwashughulikia viongozi wengine wa CHADEMA.(Pindi alipokuwa kitengo cha mitandao ya Kijamii)
  3. Credit nyingine aliyoipata kwa Dr. Slaa ni pale alipopeleka majina ya wagombea wa BAVICHA ambao wamekataa kutumika na Dr. Slaa (Mimi nikiwemo) na kupelekea majina yetu kuenguliwa, Uchaguzi wa BAVICHA uliofanyika pale ukumbi wa P.T.A Sabasaba.
  4. Lakini pia LUDO aliaminika pia na LWAKATARE kwa kuwa walitoka Mkoa mmoja wa Kagera.

  Hivyo, Mwaka 2012 LUDO alikuwa miongoni mwa frontline Undercover katika chaguzi mbalimbali, ambapo alitumikia pia kama afisa usalama wa Viongozi wa Juu wa Chama, ambapo aliongozana na DR. SLAA kama mlinzi wake kuelekea kwenye Uchaguzi wa JIMBO la UZINI kule ZANZIBAR.

  Aliendelea na nafasi yake hiyo katika Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya CHADEMA kwa kupanga na kufanikisha mikakati mbalimbali, ambapo nilikutana nae Big Brother mwanzoni mwa Mwaka huu, alikuwa anatoka PACIFIC HOTEL akaniambia kuwa ametoka MBOZI MAGHARIBI ambako alikwenda kuchunguza kama DAVID SILINDE anakubalika jimboni kwake, na hata ilipotokea sakata lililopelekea Mimi na SHONZA na wengineo kuondoka CHADEMA, LUDOVICK ndiye mtu aliyetumwa kwenda MBEYA akiwa na maagizo kutoka kwa DR. SLAA ya kumfukuza UANACHAMA baba yangu Mzazi (MZEE MWAMPAMBA ambae nae alikuwa ni mwanachama wa CHADEMA) na ndiye aliyekuja hapa JamiiForums (JF) kuweka post yenye barua za kufukuzwa kwa Mzee Mwampamba.

  PAMOJA NA HAYA YOTE NA MENGINE AMBAYO AMEIFANYIA CHADEMA AMBAYO MIMI SIYAJUI, VIONGOZI WA CHADEMA WANAKANA KUMFAHAMU………. INAHUZUNISHA..!

  Nimeshtushwa sana na Taarifa nilizoziona kwenye vyombo vya habari, juu ya Dr SLAA kukana kuwa hamfahamu wala hajawahi kumsikia na kufanya nae kazi yeyote NDUGU yangu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA.

  Lakini si hilo tu bali pia Mawakili ambao wamewekwa na CHADEMA ambao idadi yao ni watano, wakiwemo (katika mawakili hao) viongozi waandamizi wa CHADEMA wamekana kumtambua LUDOVICK, ni USALITI KIASI GANI HUU..?

  Mawakili wote watano ambao ni:-

  1. MABERE MARANDO-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA
  2. ABDALLAH SAFARI-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA
  3. NYARONYO KICHERE
  4. TUNDU LISSU-MNADHIMU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI
  5. PETER KIBATALA


  Kwanini wasigawanywe hawa au wote katika hawa hawamtetei LUDO..? Ama kama si hawa kwanini hawatafutwi mawakili wengine kwa ajili ya LUDO na badala yake akaachwa anaangamia pamoja na kujitolea kote kuijenga na kuitetea CHADEMA, pamoja na utiifu wote wa kuwalinda na kutunza siri za viongozi na siri za Chama hicho.

  ANGALIZO:
  Napenda pia kukumbusha kuwa katika umasikini mbaya ni kufikiri chini ya kiwango au utumwa mbaya ni kuruhusu wengine wafikiri kwa ajili yako nawe uwe mfuata mkumbo na upepo wa mawazo yao.

  Naomba vijana wenzangu mfikiri kwa kina juu ya haya yaliyompata LUDOVICK na mjifikirie hatma yenu ndani ya chama na maisha katika ujumla wake.
   
 2. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2013
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Duh! Kumbe wewe na Baba yako wote mlikuwa viongozi Chama kimoja, kweli CHADEMA mnafanana sana na CCM, undugunisation kama kawa!
   
 3. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2013
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,939
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mpaka jana Rwakatare alikuwa anaendelea na uhamasishaji wa chadema huko mahabusu na mda si mrefu wafungwa watapata nao ukombozi wao
   
 4. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2013
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 4,102
  Likes Received: 3,957
  Trophy Points: 280
  Wewe si mtu sahihi wa kuleta maelezo yanayohusiana na CHADEMA, DR. SLAA au viongozi wengine wa CHADEMA kwa sababu huaminiki na pia una chuki binafsi na CHADEMA na viongozi wake.

  Tunahitaji taarifa ya mtu mwingine kuweza kufikiria kama unachokisema ni kweli au la maana tayari kuna mengi, tangu utoke CHADEMA umeyasema kwa chuki kwa nia ya kujipendekeza CCM. Umekosa credibility!! Mtu kigeugeu, asiyeaminika, hata taarifa yake haiwezi kuaminika.
   
 5. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2013
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hujaanza kulia utalia sana, sijui unaendeleza biff na nani? Umepoteza kila kitu Chadema zungumzia CCM tutakuelewa
   
 6. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2013
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,511
  Likes Received: 4,643
  Trophy Points: 280
  Ujifikirie na wewe,kumbuka bado uko kwenye SIASA haya yaliyompata Ludovick kama ulivyosema huenda yakakutokea wewe
   
 7. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2013
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,357
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hapa kunaelekea kumejaa chembechembe za ukweli wa uhalisia!
   
 8. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2013
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,967
  Likes Received: 6,661
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2013
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,515
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Anza wewe kumsaidia, kwa kumtafutia mawakili!
   
 10. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2013
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,898
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  ...umeeleweka kiongozi. acha vyombo vyenye dhamana ya uchunguzi vifanye kazi.
   
 11. Kifaurongo

  Kifaurongo JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2013
  Joined: Jan 18, 2010
  Messages: 2,579
  Likes Received: 677
  Trophy Points: 280
  Hii kali, unafaa kuwa shahidi
   
 12. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2013
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,511
  Likes Received: 4,643
  Trophy Points: 280
  Hizi story zenu (wewe na Shonza) kila siku ni dhidi ya Dr Slaa,inaonekana mlikuwa na ugomvi nae personal.Sijawahi kuwaona mkiikosoa CHADEMA kama chama
   
 13. Open-Minded

  Open-Minded JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2013
  Joined: Mar 17, 2013
  Messages: 278
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kwa unataka tujadili lipi kati ya hayo uliyoeleza?
   
 14. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #14
  Mar 19, 2013
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,808
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Mwampamba kweli ulikwenda UDSM lakini haujui kuandika course uliyochukua? (BACHELOR OF ARTS WITH EDUCATION "BAED") Kwanini haukusema haya kabla la hili na una uhakika gani Ludovick ameshiriki?

  Kutokana na maelezo yako, inaonyesha Wewe na Shoza mmeshiriki katika mpango huu mchafu, Je mmelipwa kiasi gani?
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Mar 19, 2013
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Ngoma inogile
   
 16. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2013
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  We dogo unahangaika kweli. Umeanzia kule facebook naona sasa umeamua kukimbilia huku.

  Wewe kama una uchungu na huyo Ludo mwekee wewe wakili wa kumtetea.

  Unajipa kazi kubwa sana ambayo hutakaa uiweze. Take it or leave it!
   
 17. w

  wikolo JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2013
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ngoja tuendelee kusubiri na uzi wa yule dada yetu juu ya sakata hili. Ninaamini na yeye atajitokeza tu muda si mrefu sana!
   
 18. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2013
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 0
  Iwapo anahusika kweli na vitendo vya kijasusi na kigaidi kama inavyotuhumiwa, basi yaweza kuwa makubaliano ya awali ni kuwa chama kitamruka akikamatwa kwa lolote
   
 19. g

  gakato JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2013
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 832
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mwampamba, huwezi kuonewa huruma eti kwa kuweza kutunga vizuri maneno na kuandika; maelezo yako mengi yanaleta mashaka kuliko majibu. Hii ni kesi iache iendelee tutajua mbivu na mbichi si muda mrefu ndugu; tuache na CHADEMA YETU; ENDELEA NA CCM YAKO WEWE NA BABA YAKO...
   
 20. master peace

  master peace JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2013
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 1,451
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mtela Mwampamba ni huyu huyu pacha wake na Juliana tuliowashuhudia wakicheza kiduku au ni mwingine?

  Na siamini sinema yao iliiishia wapi, hata hii move ya kichina imesha anza kuchuja.
   
Loading...