Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)

Duh! Kumbe wewe na Baba yako wote mlikuwa viongozi Chama kimoja, kweli CHADEMA mnafanana sana na CCM, undugunisation kama kawa!

hakajamaliza kuwa mama yake ni diwani viti maalum wa CHADEMA, Upendeleo bado kanataka zaidi
 
...ndo mmepanga mkishatoa hiyo video yenu ya ki-china baadae mje na hivi-vihandithi vya kuungaunga?...
 
Wewe si mtu sahihi wa kuleta maelezo yanayohusiana na CHADEMA, DR. SLAA au viongozi wengine wa CHADEMA kwa sababu huaminiki na pia una chuki binafsi na CHADEMA na viongozi wake. Tunahitaji taarifa ya mtu mwingine kuweza kufikiria kama unachokisema ni kweli au la maana tayari kuna mengi, tangu utoke CHADEMA umeyasema kwa chuki kwa nia ya kujipendekeza CCM. Umekosa credibility!! Mtu kigeugeu, asiyeaminika, hata taarifa yake haiwezi kuaminika.

Asante kwakuliona hile. Nimesoma hii post nikaanza kuipa credit kwa kiasi fulani, nilipoangalia imeandikwa na nani nikapata kichefuchefu. Kama anayosema Mtela ni kweli; utamuamini vipi wakati na yeye ni msaliti? Niseme wazi nawachukia sana watu wa aina hii ya Mtela. Sipendi kabisa watu wanaotoka ndani ya chama nakuanza kulialia; inaonyesha wazi sio watu imara wakuweza ku-stand the heat inside the kitchen. Nawaheshimu sana Lowassa, Sita na wengine wote ndani ya CCM kwani wao ndio wanasiasa kamili. Sizungumziii ufisadi; ni kutokana na kwamba pamoja na kuwashiwa moto ndani ya chama, wameamua kusimama huko huko na kupigana huko huko. Mtatiro pamoja na kuwa na tofauti na viongozi wake kipindi fulani, alisimama imara na kutetea anachokiamini. Hawa wote pamoja nakwamba wanaweza kuwa wanatofautiana kimawazo na wewe na mimi; lakini wanaonyesha ni jinsi gani wanaamini wanachokitetea. Hii inaonyesha pamoja na kwamba hawakubaliani na mambo ndani ya chama; lakini wanaamini hasa kwenye itikadi ya chama chao. Same as those people ambao wameamua kubaki CDM,NCCR, CUF etc pamoja na mapungufu yaliyopo, wameamua kupigana huko huko kwani wanaamini kwenye itikadi yao. Sasa hawa watu wa aina ya Mtela, Shibuda and the like, huwa nawaogopa sana maana huwaelewi wanasimamia nini. Wao wanaangalia upepo unakoelekea ndio wanakoenda. I hate this type of people regardless ya chama alichotoka. Hata sikumoja hawawezi kukueleza tofauti za kiitikadi wanazoona kwenye chama au policies, wao ni umbea mwanzo mwisho. Unless useme wazi hukubaliani na itikadi ya chama ulichohama, hayo mengine ni kuwapumbaza watanzania kwani hata wewe Mtela credibility yako ni questionable. Hivi mbona sijawahi kumsikia Prof Safari akielekeza personal attack kwa watu ndani ya CUF? Sijawahi kumsikia yule aliyehama CUF (nimesahau jina) akahamia CCM kipindi kile cha uongozi wa Makamba akitumika insanely kama ninyi vijana? Vijana wa Kitanzania hasa walioko kwenye medani ya siasa, kama vile hawajielewi elewi hivi. Aaargh! Halafu eti vijana ndio wapewe uongozi wa nchi, ili iweje? Kama ni rahisi kuuza utu kiasi hiki utashindwa kuuza nchi au hata kama ni jimbo utakalokuwa ukilisimamia?
 
Umeeleza vizuri mwanzoni lakini umekuja kumalizia vibaya kwa sababu umepiga kampeni kwa hiyo imani yangu ni kwamba wewe ni muongo ulikuwa na lengo la kuipigia kampeni Chama cha Mabwepande/Majambazi. Ndugu yangu kwa vyovyote vile hakuna ushawishi utakaowafanya CCM waaminike zaidi ya kutekeleza ahadi walizoahidi mwaka 2010. Vinginevyo hata utoke povu mdomoni kwa kuipamba hiyo Chama ulikojihifadhi hutaeleweka. Hata hivyo unatakiwa kuandika kilichotokea mpaka umeenda huko badala ya kupotoshwa, ukweli ni kwamba hujahama CHADEMA bali ulifukuzwa, kwa mtazamo wangu wewe ni reject ya CHADEMA. CCM wameokota makombo.
 
Kama hii mada ya mtela mwampamba inaweza kusaidia kufahamu ni nani walioitengeneza ile video! nikiangalia tarehe za video! matukio yaliyotokea kipindi hicho, wahusika, na michango na mada zinazotolewa kwa sasa na wale wanaozitoa kama napata picha kwa mbaliii! Juliana Shonza ! hebu karibu uchangie kitu hapa.
 
Kama ulikuwa unamjua ni under cover informer mbona haukumlipua mapema?umesubiri apatwe na matatizo ndio unaropoka!? Tunakuamini vipi wakati kila kukicha unamchafua Dr slaa mitandaoni? Kwa nini wewe na babayako mfukuzwe chadema,je mna kasoro gani? Vipi mamako bado ni diwani wa kuteuliwa au na yeye kashafukuzwa? Ndugu yangu wewe sio wakuaminika tena mbele ya jamii simply because you are kigeu geu.
 
Mwambapa Ugonile malafyale!
Uliyoongea ni kweli kabisa. Kijana katumika kama vile mtu anavyokula muwa ukiisha utamu unatupwa na kusahau palepale.
Huyu kijana aliweza kudivert emails zangu na kuzipeleka kwa Slaa. kijana alikuwa mtiifu sana lakini wanaogopa wakimkubali tu watakuwa wamekwisha.
Kesho usishangae wakamkana Ben Saa nane kuwa hawamfahamu mara atakapoamua kuimba
Si na wewe ulikuwa five-0?And u want to be trusted?
 
Bahati mbaya sana pamoja na maelezo yako marefu lakini umeanza kuonyesha kuwa hauwezi kufikiri reasonably and analytically. Hivi wewe unadhani leo huko kwenye ccm ukimtia kiongozi yeyote - nape, kinana etc ama kwa kukusudia ama kwa kutokusudia au kwa hila yoyote ile ili yeye mwenyewe huyo kiongozi au chama chake cha ccm kionekane vibaya ktk jamii, bado kweli ccm watakutafutia mawakili wa kukutetea? wa kutetee kwa lipi? Ngoja sasa wewe nikupe somo. Kwanza waliomfungulia mashitaka wanajua kabisa kuwa Ludovick hawezi akaendelea kushitakiwa hadi mwisho. Na km hili halitatokea basi uje unisute hapa mtandaoni.

Huyu Ludovick hawezi kushitakiwa km 'accomplice' mnisahihishe wanasheria km nimelikosea kuliandika neno hili ila logic nadhani ni sahihi. Huyu bwana lazima atageuzwa kuwa ndiye shahidi wa serikali/waendesha mashitaka, kwa sasa wanazuga tu, ili awasaidie kuwapa picha halisi ilivyokuwa km kesi hii ni genuine. Vinginevyo ushahidi wa video ya mtandao bila collaborative evidence and witness, serikali wanajua kabisa kuwa hawatakuwa na kesi ya ushindi. Kesi yao lazima ishindwe.

Na hili halihitaji usomi mkubwa kulielewa. Wewe subiri utaona atawekwa mahabusu kwa miezi au miaka kadhaa wakati upelelezi unaendelea lakini mwisho wa siku serikali itamtumia huyu huyu Ludovick kuwa shahidi wa upande wao. Mimi kwa maoni yangu sioni km Ludovick ana deserve kusaidiwa kwa fadhila km unavyodai, sijui fadhila ipi? Ya kuwawekea kutengeneza 'filamu' na kuiwekea maneno kisha kui-publish mtandaoni?

Yeye ajiokoe yeye mwenyewe kwani yeye ndiye anajua ukweli km anahusika au hahusiki, amebambikiziwa kesi au la? Sidhani km chama chochote kiwe ccm au chadema wanaweza kumtuma mtu kuweka video ya aina ile mtandaoni na bado wakachekelea! No way! Wanaoweza kuchekelea kwa mambo hayo ni punguani tu ama watu ambao wanania ya kugombanisha watanzania ambao tumeishi kwa upendo. Hata wewe mwenyewe ungekuwa na akili nzuri usingekuwa na sababu ya kutumia hasira za wewe na baba yako kuondolewa chamani kuanza kuporomosha mitusi ktk mikutan ya hadhara.

Kumbuka leo wewe mtamu ccm lakini kesho wakiondoka wanaokupapatikia au ukachuja watakuweka pembeni na maisha yatakugonga. Kumbuka usiache mba chao kwa msala ujao au ukipata chungu kipya usisahau na cha zamani au usitukane wakunga na uzazi ungalipo.

Hebu niambie akina: Msabaha aliyetoka CUF zanzibar unamwona tena kuwa majukwaani baada ya kutupwa kigoma miaka fulani hivi? Hebu niambie yule aliyekuwa mkuu wa propaganda ccm hadi uchaguzi mkuu uliopita aliyetoka CUF taifa na temeke leo yuko wapi? Hebu niambie mganaji wa mashairi mkubwa wa muda mrefu wa ccm sijui tambalizeni yuko wapi?

Nyie vijana mnahitaji kuwa na jicho km la wasoma hali ya hewa msikimbilie kupewa viposho vya kwenye mikutano ya hadhara tu na ahadi za appointments angalia pia credibility na reputation yako in a long run, waambieni ccm wawape ajira ya kudumu ili hata muwe na pensheni mkiwa wazee na msaidie ndugu zetu.
 
Hivi wewe Tela la Pumba bado ujachoka kuiongelea CHADEMA? Hivi kwanini usiangaike na CCM yako? Hivi unadhani kuwa kwa kufanya hivyo wewe na wendawazimu wenzako vijana tutarudi nyuma? Mimi nadhani nitaongeza mapenzi kwa CHADEMA zaidi hata kama watu waseme ni magaidi, mauaji nk. Jana Tundu Lissu kasema, Rwakatare ajashitakiwa dhidi ya kuwavamia, kuwateka na kuwatesa Ulimboka na Kibanda. Sasa watesaji wa hawa wako wapi?
 
Duh! Kumbe wewe na Baba yako wote mlikuwa viongozi Chama kimoja, kweli CHADEMA mnafanana sana na CCM, undugunisation kama kawa!

Mkuu chadema wimbo ni huo huo, Tundu lisu, dada ake ni mbunge wa viti maalu, christina Mughwai, mwenyekiti mwenyewe, mkwe wake nadhani unamjua, a few to mention, mambo yale yale mkuu
 
Ujifikirie na wewe,kumbuka bado uko kwenye SIASA haya yaliyompata Ludovick kama ulivyosema huenda yakakutokea wewe

umenena vema sana, huyu ndugu mtela ajue kwamba anapotoa huo ushauri wake kwa vijana aelewe na yeye anahusika na ushauri huo, na tena unamhusu zaidi kwa sasa akiwa ndani ya ccm!
 
Mwambapa umepoteza na unaendelea kupoteza hata huko ccm maana unaonekana huna jipya na ni msaliliti unayetafuta kutoka kupitia kuua tumaini la watanzania. Potea zako.

Watu wa aina hii ya Mwampamba siwaelewi kabisa. Huyu kama kweli amepata chama kizuri na mbadala kulicho alichokuwepo, kwanini tena anaangalia nyuma nakuanza kulumbana na chama ambacho yeye anaamini ni cha kibabaishaji? Kwanini bado anachuki kiasi hiki? Yeye si afurahi sasa amepata chama kizuri atakachoweza kufanya kazi kwa ufanisi bila kubaguliwa? Hii haina tofauti na mke aliyeachika akaolewa na mtu mwingine lakini bado anazungumzia mabaya ya mme aliyepita. Unapata wapi muda huo ilihali huyo mme mpya anakupatia mahitaji na raha zote ulizokuwa unazitafuta? Unless kuna kitu hakiendi sawa huko uliko na kinakukumbusha machungu yaliyopita. Inshort; wacha malumbano ya siyo na tija kijana; fanya kazi ya kujenga chama na taifa huko uliko.
 
Mkuu chadema wimbo ni huo huo, Tundu lisu, dada ake ni mbunge wa viti maalu, christina Mughwai, mwenyekiti mwenyewe, mkwe wake nadhani unamjua, a few to mention, mambo yale yale mkuu

Dah! nilikuwa sijui, wewe ndio umenifungua macho, mimi nilidhani huko ndio kimbilio kwa maana kuko tofauti, kumbe yale yale full unamjua nani!
Ndio maana kumbe Waswahili tunasema kuku ukimchunguza sana utashindwa kumla
 
Kwa kutumia busara kidogo tuu wewe unafaa kuhojiwa, unajua Ludo kahusika vipi na wewe ndie uliyemponza ukijua haitajulikana na bado unataka kujua kama the other side wanajua kuwa kahusika, sasa hii BAD LIPS technology mliotumia inakunyima usingizi kwamba Ludo atatoa siri, si umesikia polisi wanaendelea kumhoji.

Kwa vyovyote vile, ilikutendeneza cinema ile lazima kuwa na original video, ambayo ilitendenezwa,ilitengenezwa na nani? na ilikuwa kwa nani, Lwakatale na CHADEMA wanajua, sasa sio ajabu kumkana huyu kijana kama kwani inaonyesha ni Malya mngine pandikizi ndani ya chadema kama ulivyokuwa wewe.
 
Dah! nilikuwa sijui, wewe ndio umenifungua macho, mimi nilidhani huko ndio kimbilio kwa maana kuko tofauti, kumbe yale yale full unamjua nani!
Ndio maana kumbe Waswahili tunasema kuku ukimchunguza sana utashindwa kumla

Kwani ukiwa mwanachama wa chadema lazima upate cheo?
 
Mwambapa Ugonile malafyale!
Uliyoongea ni kweli kabisa. Kijana katumika kama vile mtu anavyokula muwa ukiisha utamu unatupwa na kusahau palepale.
Huyu kijana aliweza kudivert emails zangu na kuzipeleka kwa Slaa. kijana alikuwa mtiifu sana lakini wanaogopa wakimkubali tu watakuwa wamekwisha.
Kesho usishangae wakamkana Ben Saa nane kuwa hawamfahamu mara atakapoamua kuimba

Mkuu, mbona unatupa mifupa tu?. Kuna uwezekano tukapata angalau nyama kidogo kuhusiana na hili. Au unasubiri siku muafaka ya kutulisha zaidi kwenye thread yake mpya.
 
Ngoma inogile/

Mungu ni mkubwa, naona wameanza kutoka pangoni, kwajinsi jamaa alivyoandika inaonekana yeye ndiye aliye wasukia mpaka wanakamatwa, sasa kama ni mlinda usalama wa slaa wewe unataka aseme anamfahamu ili kutibua mbinu zao za kiusalama.
Wewe ulisha hamia ccm endelea kuvaa magamba yako waache wanaofanya ukombozi waendelee wewe twambie namna mnavyopanga kubambikizia kesi na utekaji na kungoa kucha
 
Back
Top Bottom