Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)

Eh kweli cdm mmepandikiza vijana wengi kuandika kwenye mitandao ya kijamii kwa malipo (baadhi yao nawafahamu ni rafiki zangu-ajira safi). Acha ccm na wengine waendelee kulala usingizi wa pono. Mmebaini ukweli kuwa mitandao ya kijamii inalipa kwelikweli kisiasa kwa kuwa inalenga vijana wasomi wa .com ambao ni wengi na effectve. Ccm haina habari ghadafi na viongozi wengine hususan wa middle east walivyong'olewaje madarakani. Ni kutokana na vuguvugu zilizoanzia kwenye mitandao ya kijamii. Cdm wamegundua hilo ndo maana wame-plant vijana wengi kutwa wanashinda kwenye internet waki-post andiko ya kuishabikia cdm na kuikandia ccm na vyama vingine. Kweli umakini ccm umekwisha. Wamechoka kabisa. Sijui wana ajenda gani ya kuendelea madarakani uchaguzi ujao maana cdm hawakamatiki kwa mtaji huu. Nchemba alie tu!!! Ni uzembe wao wakutong'amua. Mimi binafsi nawaombeni cdm na ccm wasihusihusishe dini zetu takatifu katika mitego yao ya kisiasa. Wakae mbali kabisa na nyumba zetu za kuabudia na viongozi wetu wa dini. Uchafu wenu wa kisiasa uishie mitaani tafadhali. Fanyeni vurugu zozote lakini mlinde dini zetu (na viongoziwake) msizipake matope ya kisiasa. Siasa ni mchezo mchafu isiwe karibu na dini zetu.
 
yule hana tofauti na wewe,baada ya jitihada zote za kujenga chadema sasa unashiriki kupigana na kushindana na urichoshiriki kukijenga,sasa sijui ni wakati hupi ulikuwa na akili timamu,wakati hule au sasa?.
 
nafikiri hawjakosea kumwacha maana alkuwa natymika na ccm ili kuibomoa cdm so huo ndio ujira wake. kupanda kunde usitegemee kuvuna choroko ndugu. ww lalamika tu lkn LUDO ni msaliti ya nini kumtetea? ili waje aendeleze usaliti? na ww nenda lumumba kachukue ujira wako mkuu.
 
mwa mtela vyovyote utakavyo jiita we ni mpumbav.u.....peleka uma..laya wako huko....
 
ANGALIZO:
Napenda pia kukumbusha kuwa katika umasikini mbaya ni kufikiri chini ya kiwango au utumwa mbaya ni kuruhusu wengine wafikiri kwa ajili yako nawe uwe mfuata mkumbo na upepo wa mawazo yao.

Naomba vijana wenzangu mfikiri kwa kina juu ya haya yaliyompata LUDOVICK na mjifikirie hatma yenu ndani ya chama na maisha katika ujumla wake.

Ndio mtela leo nimekuelewa ulikuwa unasema nini..,na nadhani vijana wa chadema sasa wataanza kukuelewa.
 
From: Said Amour Arfi <said_arfi@yahoo.com>
Date: November 22, 2013 3:45:47 PM GMT+03:00
To: "mbowe2008@gmail.com" <mbowe2008@gmail.com>
Cc: "slaa@chadema.or.tz. zittokabwe@gmail.com" <slaa@chadema.or.tz. zittokabwe@gmail.com>

Subject: KUJIUZULU MAKAMU MWENYEKITI (BARA)

Salaam,

Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki.

Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki -wa kupindukia.

Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi

Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu

Nawasilisha.


Said A Arfi (mb)


Nakala Vyombo vya Habari
 
Huyo naye ni mmoja wao mafarisayo, cdm ipo na masalia wote lazima watoke.wale wote wanaosaliti ukombozi kwa njaa zao na tamaa zao lazima watoke,wakati utawahukumu na kuwaanika tu.CDM 4EVER
 
Back
Top Bottom